Dodoma Jiji yaigomea Simba

Muktasari:

Kipindi cha kwanza cha mchezo kati ya wenyeji Dodoma Jiji na Simba, kimemalizika kwa suluhu tasa.

Kipindi cha kwanza cha mchezo kati ya wenyeji Dodoma Jiji na Simba, kimemalizika kwa suluhu tasa.

Kipindi cha kwanza kimemalizika kwa matokeo hayo huku kikitawaliwa na rabsha kadhaa kabla ya mchezo kumalizika.

Licha ya Simba kutarajiwa kuwa na nafasi kubwa ya kusaka matokeo ya ushindi kwa kufunga bao, hali imekuwa ngumu kwani hakuna nafasi nzuri waliyotengeneza langoni mwa Dodoma Jiji.

Mipira mingi ambayo inapelekwa mbele kwa Simba imekua ikiishia njiani ama kutowafikia washambuliaji na zaidi kipa wa Dodoma Jiji, Hussein Dotto.

Ni nafasi moja tu ambayo alipata mshambuliaji Chris Mugalu ambayo haya hivyo shuti lake lilikwenda pembeni mbali kabisa kulia mwa lango la Dodoma Jiji


Simba yajeruhiwa tena

Baada ya kuumia kwa Ousmane Sakho, Simba wamepata pigo lingine la kuumia kwa beki wake Kennedy Juma.

Juma ameumia dakika za mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya kugongana na mshambuliaji Anuary Jabir wakati wakiruka kuwania mpira wa juu.

Kuumia kwa Kennedy kumekuja wakati ambao mapema aliumia Ousmane Sakho aliyegonganga na David Ulomi.

Beki Hennock Inonga ndiye ameingia badala ya Kennedy Juma ambapo sasa anacheza pamoja na Pascal Wawa.

Mwamuzi Joackim Akamba hata hivyo safari hii amemtoa kwa kadi nyekundu Anuary Jabir kwa kitendo cha kumuumiza Kennedy Juma.

Wachezaji wa Dodoma Jiji walionekana kutoridhishwa na uamuzi wa refa Akamba, ambapo walimzonga na kumsukuma wakipinga kumuonyesha kadi nyekundu mchezaji mwenzao.