Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dodoma Jiji bajeti imepanda hadi Sh1.3 bilioni, kuisaka Top Four

DODOMA Jiji msimu uliopita ilimaliza ligi katika nafasi ya nane na kwa vile ilikuwa ni msimu wake wa kwanza tangu wapande daraja, matumaini ya kufanya vizuri ni makubwa zaidi msimu huu.

Benchi la ufundi, wachezaji na viongozi, wameonekana kujipanga kikamilifu kwa ajili ya msimu mpya huku kocha mkuu Mbwana Makata akisema maandalizi aliyoyafanya kuanzia kambi nje ya Dodoma (Morogoro), iliwapa utulivu mzuri ambao anaamini umeijenga zaidi timu yake kwa mapambano ya msimu mpya.

Anasema maandalizi mazuri ya timu kuelekea ligi ndio yatakayoibeba timu yake tofauti na msimu uliopita ambao kutokana na janga la Uviko-19 wakiwa wametokea Ligi Daraja la Kwanza (Championship League), walipata muda mfupi ambao haukutosha kujiandaa lakini bado waliweza kuendana na hali ya Ligi Kuu iliyokuwa mpya kwao na kumaliza nafasi ya nane.

‘‘Tumejiandaa vizuri sana kwa ajili ya msimu huu, kuanzia kambi tuliyokaa kule Morogoro na hata tukiwa hapa Dodoma naamini imetuandaa vya kutosha kabla ya kuanza kwa ligi, pamoja na mechi za kirafiki, tunaamini tutafanya vema tuombe uzima,’’ anasema Makata.

Maneno ya Makata yanasindikizwa na yale ya Afisa Habari wao Moses Mpunga ambaye anajigamba kuwa; ‘‘Kiujumla nimekua sehemu ya maadalizi ya timu, nimekuwa nikiona jinsi wachezaji wanavyofanya mazoezi hayo kwa ari ya juu sana ambayo inaonyesha kabisa wazi kuwa wanautamani msimu uanze ili wafanye kazi wanayosubiriwa kuifanya kwa lengo la timu kufikia lengo letu la kumaliza kwenye nafasi nne za juu wa msimamo.’’

Upande wa viongozi, katibu mtendaji, Fourtnatus Johnson, anakiri kuwa wamejiwekea malengo hayo ya kuwa kwenye timu nne za juu.

‘‘Kwa upande wetu viongozi wa timu tumetimiza mahitaji karibu yote kwa benchi la ufundi na hata wachezaji, hivyo tunaamini kwamba timu yetu itakuwa na nafasi kubwa ya kufikia lengo la kuwa miongoni mwa timu nne za juu kwenye msimamo wa ligi utakapomalizika,’’ anasisitiza Katibu.


BAJETI IMEPANDA

Msimu uliopita, timu hiyo ilitumia Sh 1 Bilioni lakini hivi sasa bajeti yao imepanda na kufika Sh 1.3 Bilioni na ndani ya bajeti hiyo kuna matarajio ya kujenga Hosteli za timu pamoja na uwanja binafsi wa mazoezi.

Dodoma Jiji itaanza mechi zake mbili nyumbani dhidi ya Ruvu Shooting Sept. 28 kabla ya kucheza na Simba Oktoba Mosi, Uwanja wa Jamhuri jijini hapa.