Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Djuma, Makambo, Moloko, live kwa Mkapa

Djuma, Makambo, Moloko, live kwa Mkapa

NYOTA watatu wa Yanga, Wakongomani Djuma Shaban, Herriter Makambo na Jesus Moloko ni miongoni mwa watazamaji waliopo Uwanja wa Benjamin Mkapa kutazama mechi ya Kirafiki ya Kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Afrika ya Kati.

Nyota hao wote wamekaa jukwaa VIP A sambamba na mashabiki wengine huku wakipiga stori wakisubiri mechi ianze.

Katika dakika 45 za kwanza zinazokaribia kuanza muda si mrefu, kina Moloko, Djuma na Makambo watawashuhudia wachezaji wenzao wa Yanga, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, na Feisal Salum ‘Feitoto’ ambao wameanza kwenye kikosi cha kwanza cha Stars.

Hata hivyo katika benchi wapo Aboutwalib Mshery, Farid Mussa, Zawadi Mauya ambao pia wanakipiga Yanga.

Mchezo wa Taifa Stars na Afrika ya kati umechelewa kuanza kwa sababu za kiufundi lakini muda si mrefu utaanza kwani wachezaji tayari wamemaliza kufanya mazoezi ya kunyoosha misuli na viungo na sasa wamerejea vyumbani kwaajili ya maandalizi ya mwisho.