Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Darren Fletcher: Ni kama ingizo jipya Man United

Muktasari:

  • Baada ya kutumika kama mchezaji wa akiba alipoingia akitokea benchi kwenye mechi ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Aston Villa kwenye Ligi Kuu England wikiendi iliyopita, kiungo huyo mpambanaji alipata nafasi ya kuanzishwa dhidi ya Hull City katika mechi ya ushindi wa mabao 3-2.

MANCHESTER, ENGLAND

KIUNGO, Darren Fletcher, amerejea na kuanzishwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Manchester United baada ya kuwa nje ya uwanja kwa siku 390.

Mskochi huyo alianzishwa kwenye mechi ya ugenini dhidi ya Hull City iliyofanyika kwenye Uwanja wa KC juzi Alhamisi.

Baada ya kutumika kama mchezaji wa akiba alipoingia akitokea benchi kwenye mechi ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Aston Villa kwenye Ligi Kuu England wikiendi iliyopita, kiungo huyo mpambanaji alipata nafasi ya kuanzishwa dhidi ya Hull City katika mechi ya ushindi wa mabao 3-2.

Kitendo cha kurejea uwanjani na kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza, kinatazamwa kama ni muujiza baada ya mchezaji huyo kusumbuliwa na maradhi yaliyokuwa yakiwapa wengi hofu juu ya kwamba hatarudi tena kwenye uwanja wa mpira.

Akaa nje ya uwanja

Mara ya mwisho Fletcher kuanzishwa kwenye mechi kabla ya juzi Alhamisi ilikuwa Desemba 1, 2012 kwenye mechi ya ushindi wa aina yake wa mabao 4-3 dhidi ya Reading.

Baadaye mchezaji huyo alipatwa na maradhi yaliyogundulika miaka miwili iliyopita na hivyo kumfanya ashindwe kutimiza wajibu wake ndani ya uwanja kutokana na kuguua.

Wengi walikata tamaa na kuamini staa huyo asingerejea tena ndani ya uwanja kutokana na aina ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua. Lakini, sasa amerejea uwanjani na kuipa ahueni kubwa safu ya kiungo ya Manchester United inayoonekana kukosa uimara msimu huu.

Mastaa wampongeza

Kitendo cha kupambana na maradhi hatari na kisha kurejea uwanjani,  kimewafanya mastaa wa zamani kwenye Ligi Kuu England kumpongeza kiungo huyo kwa sababu haikuwa kazi rahisi kwake. Fletcher alirejea uwanjani na kucheza kwa kiwango kizuri licha ya kuwa nje kwa muda mrefu.

Baada ya filimbi ya mwisho, kiungo Joey Barton, Kevin Kilbane na wengine wengi walitumia fursa hiyo kutuma ujumbe wa pongezi kwa Fletcher kupitia kurasa zao za mitandao ya Twitter.

Ukiwaweka kando mastaa hao, makocha pia walimtumia pongezi zake huku mashabiki wakimwonyesha heshima ya kumshangilia kwa kusimama kwenye Uwanja wa KC wakati alipofanyiwa mabadiliko juzi Alhamisi.

Mpambanaji Man United

Tangu enzi za kocha, Alex Ferguson, Fletcher, aliyezaliwa Februari 1, 1984 huko Dalkeith, Uskochi, alikuwa akitumika kwenye mechi ngumu na zinazohitaji nguvu kubwa uwanjani.

Kutokana na kumudu kucheza mechi za aina hiyo, staa huyo alijijengea jina kwenye kikosi hicho pamoja na kuwa na uhakika wa namba wa mechi zote ngumu labda kama atakuwa majeruhi.

Umahiri wake huo wa kiuchezaji ulimfanya apewe unahodha wa timu ya taifa ya Scotland na kwa muda ambao alikuwa nje ya uwanja haikuwa pigo kwa Manchester United pekee, bali kwa nchi yake pia kwa sababu ilikosa mpambanaji wa kweli ndani ya uwanja.

Akosolewa na Roy Keane

Fletcher wakati anaanza kuichezea Manchester United mtu wa kwanza ambaye alikuwa hamkubali kabisa ni nahodha wa zamani wa timu hiyo, Roy Keane.

Kwenye mechi ya kipigo cha mabao 4–1 dhidi ya Middlesbrough, Oktoba 2005, mtu wa kwanza kuonyeshewa kidole na Keane alikuwa Fletcher. Keane alidai kuwa kwamba Fletcher hakuwa mchezaji mwenye hadhi ya kuichezea Manchester United na anawashangaa watu wa Scotland kwa kuwa na imani na mchezaji huyo.

Lakini, Fletcher hakujibizana na Keane kwa maneno, badala yake alionyesha kiwango cha juu kwenye mechi dhidi ya Chelsea na tangu hapo akawa mmoja wa wachezaji wanaowapa shaka mashabiki wa Man United huenda wakafanya vibaya kama anapokosekana uwanjani.

Kurejea kwake uwanjani kwa sasa kunampa David Moyes nguvu mpya kwenye safu ya kiungo kwa sababu atakuwa na nafasi ya kuwabadilisha nyota wake bila ya hofu yoyote. Fletcher na Michael Carrick wamecheza pamoja kwa muda mrefu hivyo Moyes anaweza kuwa mwenye bahati kwa upande wake kama mastaa hao wawili wote watakuwa fiti.

Maisha binafsi

Fletcher ni baba wa watoto wa kiume pacha; Jack na Tyler, waliozaliwa mwaka 2007 na mkewe, Hayley Grice. Wawili hao, Fletcher na mrembo Hayley walifunga pingu za maisha Juni 2010.

Fletcher ni mmoja wa wachezaji wengi wa klabu za Manchester na Liverpool ambao nyumba zao huvamiwa na wezi pindi wanapokwenda kwenye mechi za ugenini.

Februari 2009, mkewe alivamiwa na watu waliotishia kumchoma kisu, tukio ambalo lilitokea wakati Fletcher alipokwenda Milan, Italia na kikosi cha Manchester United kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Inter.

Staa huyo pia ana mradi wake wa kuhudumia viziwi ambao anapewa sapoti kubwa na Manchester United.