Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carlinhos atajwa Yanga

UREJEO wa kiungo Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ ndani ya Yanga umeelezwa kma utaongeza kitu kutokana na namna mchezaji huyo alivyokuwa na mchango kipindi alipokuwa akitumika kwenye mechi za vinara hao wa Ligi Kuu Bara.

Carlinhos alikuwa nje ya uwanja baada ya kuwa na adhabu ya kadi nyekundu iliyotokana kumpiga ngumi mchezaji wa Kengold katika mchezo wa Kombe la Azam, hata hivyo adhabu hiyo imeisha na baadhi ya wachambuzi wamedai kama atatumika kwenye mechi za timu hiyo huenda akaibeba.

Kama kocha Juma Mwambusi hatakuwa na hiyana naye, huenda mchezo huo akaanza kuonekana tena uwanjani katika mechi ya keshokutwa ya Ligi Kuu dhidi ya Biashara United itakayopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, kwani huko mazoezi gari lake limewaka.

Baadhi ya wakongwe na wachambuzi wa soka nchini wamemchambua kiungo huyo kutoka Angopla na kudai bado ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kama akipewa muda wa kucheza.

Mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga, Zamoyoni Mogella alisema mchezaji huyo ni mzuri na anaweza kuisaidia klabu yake kama akipewa nafasi.

“Carlinho ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na kila mmoja anajua hilo, kama yupo fiti na akipewa mechi anaweza kuisaidia timu, lakiniu wacheze kitimu na sio mchezaji mmoja mmoja,” alisema Mogella, wakati mchambuzi mahiri, Ally Mayay alisema urejeo wa mchezaji huyo una maana kubwa kwa Yanga.

Mayay alisema mchezaji huyo amekuwa na msaada mkubwa katika mipira yote ya adhabu ambayo muda mwingine Yanga wamekuwa wakipata tabu.

“Carlinho ni mchezaji ambaye akili yake inakuwa inawaza mbele, muda wote anapokuwa na mpira huwa anawaza kwenda mbele,” alisema Mayay na kuongeza;

“Mikimbio ya Tuisila ni mizuri lakini upande wa Carlinhos yeye ana uwezo hata wa kupiga mipira mirefu kwenda langoni kwa wapinzani.”

GARI LIMEWAKA

Kiungo huyo licha ya kwamba alikuwa yupo nje ya uwanja, Mwanaspoti ambalo limekuwa likihudhuria mazoezi ya Yanga na kumshuhudia mchezaji huyo akiwa na ufiti uliopitiliza na kufanya udambwidambwi ambao ulikuwa burudani kwa mashabiki wanaohudhuria mazoezi hayo.