Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba hii yeyote anakaa benchi

Muktasari:

STRAIKA wa Simba, Meddie Kagere amevunja ukimya juu ya kelele za kuanzishwa kwake benchi, akisema licha ya kuwa mfungaji bora misimu miwili mfululizo, ila kwa uwekezaji mkubwa wa kuunda kikosi hicho umefanya staa yeyote kuanzia nje na wala sio kwake tu!

STRAIKA wa Simba, Meddie Kagere amevunja ukimya juu ya kelele za kuanzishwa kwake benchi, akisema licha ya kuwa mfungaji bora misimu miwili mfululizo, ila kwa uwekezaji mkubwa wa kuunda kikosi hicho umefanya staa yeyote kuanzia nje na wala sio kwake tu!

Akizungumza na Mwanaspoti, raia huyo wa Rwanda mwenye asili ya Uganda, alisema Simba ya sasa ni moto kuanzia wachezaji wanaoanza kikosi cha kwanza na wale waliopo benchi, hivyo linakuwa ni jukumu la kocha Didier Gomes kufanya uchaguzi wa nani anamtaka na kwa wakati gani.

Kagere, alisema hana wasiwasi na kiwango chake, alitolea mfano kwamba alivyochezeshwa dakika 90 dhidi ya Al Ahly ya Misri, kutokana na kocha Gomes kuona anafaa kuanza kwenye mchezo huo, hivyo kutoanzishwa kwa baadhi ya mechi za Ligi Kuu Bara, hakumnyimi raha bali anaona ni ubora wa kikosi ambao unampa nafasi kila mchezaji.

“Kila mchezaji aliyeopo Simba ni ubora, kikubwa timu ishinde na kufikia malengo ya msimu huu, ndio maana kocha anamtumia anayemtaka katika mechi husika, hilo halina maana nimefulia, hapana najiamini ndio maana hadi sasa nina mabao tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu,” alisema Kagere n kuongeza;

“Uongozi wa Simba umewekeza kusajili wachezaji wenye viwango vya juu, ukiangalia wachezaji waliopo benchi na wale ambao wanaanza wote wanaweza wakaipa timu matokeo, hilo linampa kocha uhuru wa maamuzi ya nani amtumie, binafsi akianza mwingine na mimi nikikaa benchi naona tunakuwa tunafanya kazi moja ya kujenga Simba imara, ama nikianza na mwingine akasubiri sidhani kama atakuwa ana kinyongo, Simba ni nguvu moja,” alisema.

Mbali na hilo, alisema Simba ina nafasi ya kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutetea taji la Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho (ASFC), akisisiza kazi yao kubwa ni kujituma tu.