Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bocco kuagwa kwa heshima JKT

BOCCO Pict

Muktasari:

  • Bocco alijiunga na timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Simba alikokuwa anafundisha timu ya vijana, licha ya kufunga mabao mawili akiwa na JKT Tanzania, ilielezwa sababu ya kupewa nafasi ya kuagana na mashabiki ni mchango wake kwa wachezaji wenzake, ikiwemo kuonyesha nidhamu ya hali ya juu katika majukumu aliyokuwa anayafanya.

MSHAMBULIAJI wa JKT Tanzania, John Bocco imeelezwa huenda ukatumika mchezo dhidi ya Mashujaa utakaopigwa Juni 22, Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma kuagana na mashabiki wa timu hiyo. 

Bocco alijiunga na timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Simba alikokuwa anafundisha timu ya vijana, licha ya kufunga mabao mawili akiwa na JKT Tanzania, ilielezwa sababu ya kupewa nafasi ya kuagana na mashabiki ni mchango wake kwa wachezaji wenzake, ikiwemo kuonyesha nidhamu ya hali ya juu katika majukumu aliyokuwa anayafanya.

“Bocco amekuwa mfano wa kuigwa katika nidhamu ya kazi na mshauri kwa wachezaji ambao ni wadogo kwake namna ya kuhakikisha wanafanya kazi kwa kiwango cha juu kwa muda mrefu,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Kila kitu Bocco anapenda kufanya kwa wakati na muda sahihi mfano kufika mazoezini, muda wa chakula, wakati mwingine bidii ya mazoezi yake binafsi ni kubwa kuliko wachezaji wanaojitafuta na wanaojitafuta wakiwa wameridhika.

“Licha ya mafanikio aliyonayo Bocco ya rekodi ya mabao mengi ya Ligi Kuu, maisha yake kiuchumi ila anavyopambana utadhani ndiyo anaanza kusaka maisha yake upya, nidhamu kwa kocha kiukweli wachezaji wanapaswa kujifunza mengi ili waweze kufanikiwa.”

Alipotafutwa Msemaji wa timu hiyo, Masau Bwire ili kuthibitisha hilo alisema: “Sina taarifa hizo, kikubwa timu inafanya maandalizi ya mechi mbili zilizosalia dhidi ya Pamba na Mashujaa.”