Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bocco aipunguzia ulinzi Simba

Muktasari:

Kocha wa Simba, Didier Gomes ameamua kupunguza mchezaji wa ulinzi kuongeza mashambulizi kwa timu yake.

Kocha wa Simba, Didier Gomes ameamua kupunguza mchezaji wa ulinzi kuongeza mashambulizi kwa timu yake.

Kitendo cha kumtoa beki wa kulia, Israel Patrick na kuingia John Bocco, kimelenga kuongeza nguvu zaidi kwenye eneo la ushambuliaji.

Mabadiliko hayo pia yametokana na wapinzani wao Dodoma Jiji kuwa pungufu uwanjani kufuatia mshambuliaji wake wake Anuary Jabir kutolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza.

Bocco sasa anacheza pamoja na Chris Mugalu wakitengeneza ushirikiano wa washambuliaji wawili wa mwisho huku wakisaidiwa na viungo wengi.

Kocha Dodoma ajilipua

Katika kuonyesha kwamba anasaka matokeo ya ushindi, Kocha wa Dodoma Jiji, Mbwana Makata, amejilipua kwa kuwaingiza washambuliaji wawili kwa mpigo.

Washambuliaji walioingia ni Omary Kanyoro na Seif Karihe ambao wameingia kuwabadili Mcha Khamis na David Ulomi.

Mabadiliko hayo no tofauti na matarajio ya wengi ambao walidhani kocha huyo ataingiza wachezaji wa kukaba zaidi alionao kwenye benchi.

Wachezaji wa kukaba waliopo nje ni Rajab Mgalula na Enrick Nkosi lakini Makata ameamua kuwaingiza wachezaji wa kushambulia zaidi.

Lwanga naye aumia, wawili waingia

Simba kwa mara ya tatu sasa wamelazimishwa kufanya mabadiliko, kufuatia kuumia tena kwa kiungo Tadeo Lwanga.

Lwanga ameumia kufuatia kugonganga na kiungo Salmin Hoza wakati wakiwania mpira wa juu kabla ya kuanguka na kushindwa kuendelea na mchezo.

Kuumia kwa Lwanga ni mwendelezo wa wachsAhi wa Simba kuumia baada ya awali kuumia kwa Ousmane Sakho na Kennedy Juma.

Nafasi ya Lwanga imechukuliwa na nyota mpya wa Simba, Duncan Nyoni huku Meddie Kagere akiingia badala ya Yusuph Mhilu.

Mabadiliko ya Kagere yamelazimika kufanywa kwa wakati mmoja pamoja na Nyoni kutokana na kanuni mpya za baada ya janga la Uviko-19.

Hii inamaanisha kwamba kama asingeingia pamoja na Nyoni, hakukuwa na fursa nyingine ya kufanya mabadiliko kwa Simba