Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Boban: Nimetumwa kazi Geita

New Content Item (1)
New Content Item (1)

KIUNGO mpya wa Geita Gold, Seleman Ibrahim ‘Boban’ baada ya kuonyesha kiwango bora katika mechi tatu za mwanzo za timu hiyo kwenye Ligi Kuu, amefunguka kutumwa kufanya kazi kikosini hapo.

Boban aliyesajiliwa na Geita Gold akitokea Mbeya City alikocheza kwa muda mrefu amefunguka siri ya ubora wake kuwa ni kujitambua, kupambana na kujua nini anahitaji kufanya ndani ya Geita.

“Ujue sio rahisi kupata nafasi katika timu yenye wachezaji wengi bora kama hii, hivyo ukiipata unatakiwa kuhakikisha unaonyesha kile ulichonacho.

“Nimekuja hapa kufanya kazi ya mpira na si vinginevyo, kwa hiyo nahitaji kuifanya kwa uhakika ili ionekane na hilo nalifanya kwa kushirikiana na wenzangu huku nikufuata maelekezo ya benchi la ufundi,” alisema Boban aliyekulia kwenye akademi ya Simba.

Boban anayemudu kucheza eneo la kiungo mkabaji na mshambuliaji, ndani ya Geita anakutana na ushindani wa namba kutoka kwa viungo kama Kelvin Nashon, Ramadhan Chombo, ‘Redondo’, Yusuph Kagoma, Oscar Maasai, Shivo Shinobu na Offen Chikola.

Kocha wa Geita, Fred Felix ‘Minziro’ alimuelezea Boban kama kiungo mzuri ndio maana yupo katika kikosi chake.

“Ni mchezaji mzuri, ana utulivu akiwa na mpira pia anajua kucheza na wenzake kwa ubora ni miongoni mwa viongo bora tulionao ndani ya timu,” alisema Minziro.

Geita Gold hadi sasa imecheza michezo mitatu, ikipoteza mmoja ugenini kwa kufungwa 3-0 dhidi ya Simba na kutoa sare michezo miwili za 1-1, mbele ya Azam FC na Kagera Sugar na mechi ijayo itacheza Septemba 14 na Singida Big Stars katika Uwanja wa CCM Kirumba.