Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki awahenyesha Msimbazi Dar

Beki wa JKT Ruvu Mohammed (Jezi ya njano) akiwajibika

Muktasari:

Mmoja ni beki la shughuli la JKT Ruvu, Mohammed Faki na mwingine ni kiraka, Samir Haji Nuhu ambaye ni Mzanzibari aliyekuwa akicheza Uarabuni.

SIMBA jana Jumatano jioni ilikuwa kwenye mazungumzo mazito na majembe mengine mawili ya Kibongo ambayo wanataka kuyasajili.

Mmoja ni beki la shughuli la JKT Ruvu, Mohammed Faki na mwingine ni kiraka, Samir Haji Nuhu ambaye ni Mzanzibari aliyekuwa akicheza Uarabuni.

Faki ni miongoni mwa mabeki wenye nguvu, akili ya mpira pamoja na ubishi uwanjani na huwa hakubali kupitwa kirahisi. Licha ya kwamba Yanga na Simba zilishinda mechi zao dhidi ya JKT msimu uliopita, lakini Faki aliyekuwa anavaa jezi namba 26 aliwatoa jasho akina Mrisho Ngassa na Haruna Niyonzima.

Kwenye mechi za Simba, Jonas Mkude na Emmanuel Okwi wanajua shughuli yake. Vigogo wa usajili wa Simba wamefuatilia ufanisi wa Samir kupitia mikanda ya video pamoja na rekodi zake wakajiridhisha na kumsainisha.

Wachezaji hao huenda wakasaini mikataba rasmi leo baada ya kushindwa kuafikiana dau jana licha ya mazungumzo na vigogo wa Simba kuchukua muda mrefu. Mmoja wa Vigogo wa Simba alidai kwamba jana hakikueleweka lakini itakuwa freshi tu kwavile wanakomaa na wamepania.

Usajili wa straika wa Mgambo, Malimi Busungu mpaka jana usiku ulikuwa umewekwa kando na imeelezwa kwamba mchezaji huyo ameponzwa na kigogo mmoja wa juu kwenye uongozi wa Simba. Simba wamemkaushia kwa sababu ya dau kubwa lakini wanadai anachochewa na kiongozi huyo na ni mtu wake. Busungu alitaka apewe Sh40 milioni na sasa mabosi wa Simba wenye misimamo mikali wamemwambia kiwango chake ni Sh10 hadi 15 milioni kama hataki aondoke.

Awali Busungu alikuwamo katika mapendekezo ya usajili wa wachezaji wapya wa Simba, lakini walimkaushia zaidi baada ya kujihusisha na usajili Yanga na imeelezwa kwamba kigogo huyo ndiye anayeshinikiza Busungu asajiliwe Simba.

Busungu aliamua kugeukia usajili wa Simba baada ya kuona Yanga hawaeleweki na hawajamwambia chochote juu ya usajili wake ingawa kuna taarifa kuwa kama watamsajili basi atakuwa mchezaji wa mwisho kabisa.

Habari kutoka ndani zinaeleza kuwa wanachama wawili wa Simba juzi Jumanne walikwenda kumchukua Busungu maeneo ya Mbagala alikokuwa amefichwa na kigogo huyo na kufanya naye mazungumzo.

“Tunajua fedha anayoitaka ameelekezwa na kiongozi mwenzetu jambo ambalo hatuwezi kukubaliana nalo, dau letu tumemwambia, akitaka achukue vinginevyo aache.

“Kwa kiwango tulichomopangia akikichukua ni sawa lakini si hicho kingine.”

Kwa upande wa Busungu ambaye amemamliza mkataba wake na Mgambo, alisema: “Kwa sasa nimemwachia Mungu katika suala langu la usajili, nipo tayari kwenda popote nitakapofanikiwa kusajiliwa.”