Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beka Ibrozama achomoka na Kangaroo

Beka Ibrozama

BAADA ya kimya cha miaka mitano iliyopita msanii wa muziki wa kizazi kipya, Beka Ibrozama amerudi tena katika sekta hiyo na kuwaomba wasanii walinaochipukia na kutumia jina lake waache kwasababu mwenyewe karudi tayari kwa mapambano.

Msanii huyo ambaye alishawahi kutamba na vibao kama Natumaini na Narudi nyumbani zilizomtambulisha vyema katika soko la muziki amerudi na kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la Kangaroo anayotarajia kuiachia hivi karibuni.

Akizungumza na Mwanaspoti Beka alisema kumekuwa na mlundikano wa wasanii wengi ambao wameweza kutumia jinalake kuingia katika tasnia hiyo na kuweka wazi kuwa hakuna aliyeweza kufanya kazi nzuri kama alizokuwa anafanya yeye hivyo kawaomba watafute majina mengine waachane na jina hilo kwasababu mwenyewe karudi.

 

Akizungumzia ujio wake mpya alisema utaonyesha utofauti mkubwa kwani alikaa kimya kwa muda kwaajili ya kulisoma soko la muziki na kujua nini wanakikosa mashabiki zake sasa ameibuka kuwapa burudani waliyoikosa kwa muda mrefu.

 

"Muziki wala soko la muziki halozoeleki hivyo kukakaa kwangu kimya kwa muda nilikuwa nawasoma wasanii wenzangu nini wanafanya na wanakosea wapi ili namimi niyafanyie kazi mapungufu yaokwa kutoa kazi nzuri ambayo itawashtua wengi," alisema.

 

Pia alitumia nafsi hiyo kuwaomba mashabiki wa kazi zake kukaa tayari kwa ujio huo mpya ambao anaamini utarudisha jina lake katika nafasi ileile aliyokuwanayo tangu anaanza muziki.