Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barka kinda bora wa mwaka 2021 Ajax

KINDA la Kitanzania, Barka Mpanda ameteuliwa kuwa Kinda Bora wa Mwaka 2021 baada ya kufanya vizuri katika kliniki aliyohudhuria kwenye shule ya soka ya klabu hiyo.

Agosti mwaka jana, 2021 miamba ya soka la Uholanzi, Ajax ilitoa nafasi kwa wachezaji wenye vipaji maalum kuhudhuria kliniki iliyolenga kuwapa mafunzo vijana hao kwa lengo la kuviimarisha vipaji vyao ili kuwa bora zaidi kwa miaka ijayo.

Miongoni mwa vijana ambao walikuwa sehemu ya kliniki hiyo ni pamoja na Barka Mpanda ambaye alifuatana na mjomba wake, Hemed Tawah.

Tawah alisema wamepokea kwa furaha taarifa ya Barka kuwa ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka kwa wachezaji wote ambao walihudhuria kliniki ile wiki mbili hivyo ni kama milango ya neema kwa kijana huyo inaendelea kufunga zaidi na zaidi.

“Kama msimamizi wake ambaye nilipewa jukumu hilo na mzazi wake ambaye alikuwa bize kutoka na majukumu mbalimbali, imenifanya kuona ni kwa namna gani safari yetu ilikuwa ya ushindi maana tukiwa kule alichaguliwa kuwa MVP, mjuzi bora wa wiki,”

“Hii ya kuwa mchezaji bora wa mwaka wa kliniki ambazo zimefanywa na Ajax ina maana kuwa kipaji na jitihada zake zimeheshimiwa,” alisema mjomba wa Barka.

Ndani ya wiki mbili za kliniki ya Barka, Hemed ndiye aliyekuwa anatoa usaidizi kwa kijana huyo kutokana na udogo wa umri wake, “Nakumbuka vile ambavyo wazazi wa wachezaji wengine walivyokuwa wakimsifia Barka wakati wa kliniki,”

“Alikuwa tofauti kabisa na vijana wengi na ndio maana ilikuwa rahisi kwake kutwaa tuzo mbalimbali ambazo naamini zinailetea sifa Tanzania pamoja na heshima.”

Kufanya vizuri kwa Barka kwenye kliniki hiyo kumeibua matumaini kibao kwa Watanzania mbalimbali na kumtazama kinda huyo kuwa huenda akawa miongoni mwa wachezaji wakubwa na wa kutegemewa kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa miaka ya baadaye.

Wapo ambao wanaamini kuwa huenda Barka muda wowote ndani ya mwaka huu, akajiunga na akademi ya Ajax kutokana na kile ambacho alikifanya kwenye kliniki ya wiki mbili na miongoni mwao ni pamoja na kocha wa timu za vijana za Azam FC, Mohamed Badru.

“Hakuna kikwazo kwake nadhani ni suala la muda maana anaonekana kuwa na kipaji kikubwa sana na kwa umri wake ndio wenyewe kabisa kwa mtoto kuanza kutengenezwa na kulelewa kwenye misingi bora ya kuwa mchezaji wa daraja la juu,” alisema.

Kwa upande wake Baba wa Barka, Mpanda alisema: ”Kwenye hili mimi mzazi kiukweli nimefurahi sana, nimefarijika kiukweli kwa sababu hii inaleta heshima kubwa sana kwenye taifa na familia, naona mafanikio makubwa sana huko mbele.”