Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bao sasa mwendo wa kimataifa

Muktasari:

  • Likwepa aliliambia Mwanaspoti kuwa, kwa mara ya kwanza wamepokea mualiko kutoka Kazakhstan iliyoko Asia ya Kati, wakitaka Tanzania ikautambulishe mchezo huu wa asili katika shindano la Michezo ya Kitamaduni duniani.


NDOTO za Rais wa Awamu ya Kwanza wa Tanzania, Mwl JK Nyerere kutaka kuona mchezo wa bao ukifika anga za kimataifa sasa imetimia, hayo yakisemwa na Rais wa Shirikisho la mchezo huo, Monday Likwepa.

Likwepa aliliambia Mwanaspoti kuwa, kwa mara ya kwanza wamepokea mualiko kutoka Kazakhstan iliyoko Asia ya Kati, wakitaka Tanzania ikautambulishe mchezo huu wa asili katika shindano la Michezo ya Kitamaduni duniani.

Alisema licha ya serikali kutoupa kipaumbele mchezo huo, lakini yapo mataifa ambayo yamewaona na kutambua uwepo wao ndio maana matunda haya yameanza kuzaliwa.

"Mwaliko huu umetufikia na tumepewa tiketi sita na watalipia kila kitu, hivyo kwa sasa tunahitaji Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuonyesha ushirikiano ikiwezekana tupate kiongozi wa kwenda naye kama ilivyo kwenye maeneo mengine," alisema Likwepa na kuongeza;

"Hii ni fahari kwetu, sisi kama Watanzania ambao ni waanzilishi wa mchezo huu kupata nafasi ya kushiriki na mimi kama kiongozi nitapewa nafasi ya kuzungumza katika shindano hilo, jambo ambalo litaitambulisha nchi na sisi kwa ujumla."

Mashindano hayo ya Kazakhstan yatafanyika kati ya Septemba 8-15 na hii itakuwa mara ya kwanza kwa Tanzania kushiriki.