Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pamba Jiji yaendelea kusajili kimya kimya

PAMBA Pict

Muktasari:

  • Pamba Jiji iliyomaliza nafasi ya 11 katika Ligi Kuu Bara ikivuna pointi 34 imeanza kuboresha kikosi kwa msimu ujao hasa eneo la ushambuliaji lililomaliza na mabao 22 tu na beki lililofungwa mabao 33, na eneo la kiungo na inaelezwa imeshamnyakua Bwalya waliyemkosa dirisha dogo.

BAADA ya kumalizana na kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba aliyekuwa Napsa Stars ya Zambia, Larry Bwalya, Pamba Jiji imeendelea kufanya yake kimyakimya ikidaiwa inazungumza na mshambuliaji Umar Abba, huku ikimpa mkataba wa miaka mwili John Mbise aliyekuwa Geita Gold.

Pamba Jiji iliyomaliza nafasi ya 11 katika Ligi Kuu Bara ikivuna pointi 34 imeanza kuboresha kikosi kwa msimu ujao hasa eneo la ushambuliaji lililomaliza na mabao 22 tu na beki lililofungwa mabao 33, na eneo la kiungo na inaelezwa imeshamnyakua Bwalya waliyemkosa dirisha dogo.

Chanzo kiliambia Mwanaspoti, kwa sasa Pamba ipo katika mazungumzo mazuri na pengine muda wowote kuanzia sasa nyota huyo wa Bugesera FC ya Rwanda atasaini mkataba wa miaka miwili.

Umar Abba raia wa Nigeria aliibuka mfungaji bora wa Ligi ya Rwanda baada ya kufunga mabao 18 kwenye mechi 12 alizocheza.

"Kama tutafanikiwa, nafikiri utakuwa usajili wa pili wa kimataifa, ni mchezaji mzuri na takwimu zake zimewashawishi viongozi wa Pamba, Ligi imebadilika, unahitaji kuanza maandalizi mapema ili kushindana," kilisema chanzo hicho.

Mbali na Mnigeria huyo, pia Pamba inadaiwa imempa mkataba wa miaka miwili kiungo wa Geita Gold, John Mbise.

"Tunaendelea kuimarisha kikosi chetu ijapokuwa tuna wachezaji wengi wazuri ila ushindani ni mkubwa hivyo lazima kikosi kiwe kipana.

"Ndio maana tumemsainisha Mbise mkataba wa miaka miwili ili aongeze nguvu hasa katika eneo la kiungo ili kwa pamoja tuzidi kuiweka timu katika mikono salama," mmoja wa vigogo wa Pamba alilihakikisha Mwanaspoti.

Hata hivyo, akizungumzia juu ya usajili, Ofisa Mtendaji wa Pamba Jiji, Peter Juma Lehhet, alisema kwa sasa wanajipanga kwa ajili ya kufanya usajili wa nguvu utakaoongeza tija na kuleta ushindani kwa msimu ujao.

"Kwa sasa tumeanza mchakato wa kusajili nyota wapya na kukaa chini na wale ambao mikataba yao imeisha, tunaendelea na mazungumzo nao. Kama kuna kitu kinaendelea cha usajili mtajulishwa," alisema Peter.

Kama Pamba Jiji itafanikisha dili hilo la Umar Abba, hii itakuwa mara ya kwanza kwa mshambuliaji huyo kuichezea Ligi ya Tanzania, akicheza zaidi nchini kwao Nigeria na Rwanda.

Kabla ya Bugesera aliyojiunga nayo msimu huu, alipita Gombe ya Nigeria msimu mmoja (2023/24), Lobi Stars (2022/23), Katsina United (2021/22), Plateau United (2019–21) na nyinginezo.

Kijumla, Abba amecheza mechi 110 za timu zote alizopita na kufunga mabao 40.