Bangala, Moloko wachenjiwa

Monday October 25 2021
bangala pic
By Clezencia Tryphone

KUTAMBUA ugumu wa mchezo ujao dhidi ya Azam FC, umemfanya kocha mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi awabadilishie ratiba ya mazoezi mastaa wake kina Yannick Bangala, Fiston Mayele, Jesus Moloko na wengineo ili kujiandaa na mchezo huo wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo huo wa raundi ya nne unatarajiwa kupigwa Jumamosi ijayo na rekodi zinaonyesha timu hizo zinapokutana hakuna dogo na kocha Nabi ameamua kubadili ratiba akiwapelekea wachezaji wake gym na jana kuwapa mapumziko kabla ya leo kurudi asubuhi.


Advertisement