Bangala hatihati kucheza kesho

Saturday May 14 2022
bangala pic
By Ramadhan Hassan

Dodoma. Yanga inatarajia  kuwakosa Yacouba Sogne na Chico Ushindi kutokana na kuwa  majeraha huku kiungo  Yanick Bangala  akiwa katika hati hati ya kucheza kutokana na kufiwa na Kaka yake.

Timu hiyo inatarajia kucheza kesho saa 10 jioni dhidi Dodoma mtanange unaotarajiwa kufanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini hapa.

Kocha wa Yanga, Nesreddine Nabi amesema Yacouba amekuwa kwenye majeruhi kwa  muda mrefu huku  Chico bado hajapona vizuri.

Kuhusu Bangala amesema jana alipata taarifa ya msiba wa kufiwa na kaka yake hivyo watashauriana acheze ama la.

“Tutaongea nae tuone jinsi anavyojisikia maamuzi ya kumtumia yatatokana na kikao cha leo  cha sisi na yeye akijisikia vizuri tunaweza tukamjumuisha kama hatajisikii tunatakiwa kumheshimu kwani tangu ameanza  ligi ameonesha mfano mzuri,”amesema.


Advertisement
Advertisement