Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baada ya Mkude ni zamu ya Maxi

Muktasari:

  • Maxi kama mambo yataenda sawa msimu ujao atavaa uzi wa njano na kijani ambapo taarifa za kupenyezewa zinadai Yanga watalazimika kutumia zaidi ya Sh400 milioni kununua mkataba wake wa mwaka mmoja uliobakia kwenye klabu yake ya AS Maniema.

Nahodha wa AS Maniema Union ya DR Congo, Maxi Mpia amewasili nchini wa leo Julai 12, 2023 kukamilisha dili la kujiunga na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga.

Maxi kama mambo yataenda sawa msimu ujao atavaa uzi wa njano na kijani ambapo taarifa za kupenyezewa zinadai Yanga watalazimika kutumia zaidi ya Sh400 milioni kununua mkataba wake wa mwaka mmoja uliobakia kwenye klabu yake ya AS Maniema.

Winga huyo anatajwa kuja kuchukua nafasi ya Mkongomani mwenzake Twisila Kisinda aliyeimaliza mkataba wake wa mwaka wa mkopo akitokea RS Berkane ya Morocco.


HUKU KWA MKUDE KIMELEWEKA

Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kumsajili kiungo, Jonas Mkude kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Simba.

Huu unakuwa ni usajili wa tatu wa Yanga msimu huu baada ya kumsajili Nickson Kibabage kutoka Singida FG na Gift Fred kutoka SC Villa ya Uganda.