Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz KI asaini Yanga kwa sharti hili

Muktasari:

  • Aziz Ki amewaambia viongozi kwamba liwake inyeshe wamhakikishie kama watasaini straika  wa maana kwenye dirisha lijalo na walipomthibitishia ndio akasaini mkataba ambao ni suala la muda tu atatangazwa  kumaliza tetesi za yeye kutakiwa na Mamelodi Sundowns, Orlando Pirates za Afrika Kusini na Esperance De Tunis.

Yanga imeshinda vita nyingine kubwa ya nje ya uwanja kimyakimya baada ya kumuongeza mkataba wa miaka miwili kiungo wake mshambuliaji, Stephanie Aziz Ki lakini Mwanaspoti limeambiwa amesaini kwa kuwa masharti moja kwa viongozi.

Aziz Ki amewaambia viongozi kwamba liwake inyeshe wamhakikishie kama watasaini straika  wa maana kwenye dirisha lijalo na walipomthibitishia ndio akasaini mkataba ambao ni suala la muda tu atatangazwa  kumaliza tetesi za yeye kutakiwa na Mamelodi Sundowns, Orlando Pirates za Afrika Kusini na Esperance De Tunis.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ambazo Mwanaspoti imejiridhisha ni kwamba Aziz Ki ataendelea kusalia ndani ya klabu hiyo na amewaambia lengo lake ni kuhakikisha msimu ujao timu inapiga hatua zaidi kutoka hapo ilipo kwani kwasasa wanatumia nguvu kubwa zaidi kushinda mechi kubwa haswa za kimataifa.

Aziz amewaambia mabosi wa Yanga kuwa sio kipaumbele chake kutaka kuwa mfungaji bora lakini angependa kuona kikosi hicho kinaletewa mastaa wa maana zaidi hasa eneo la ushambuliaji ili aje awatengenezee nafasi za kufunga.

Mwanaspoti linajua viongozi wamemhakikishia Aziz kwamba watashusha mastaa akiwewo mshambuliaji Prince Dube aliyeikimbia klabu yake akishinikiza kuondoka anakuwa mali yao kwa msimu ujao.

Dube bado yuko Salasala jijini Dar es Salaam akiishi kwenye jumba moja la kifahari wakati akiendelea kushikilia msimamo wa kutaka kuachana na klabu yake ya Azam akidai hana furaha ya kuendelea kuwatumikia matajiri hao na tayari ameshakwenda kwenye mamlaka za soka kuukana mkataba wake.

Nyuma ya Aziz KI mtu anayemfuatia kwa ufungaji ni washambuliaji Kennedy Musonda mwenye mabao 6 ambapo matatu akiyafunga kwenye ligi na matatu ligi ya mabingwa huku Clement Mzize mwenye mabao kama hayo akifunga manne kwenye ligi na mawili ligi ya mabingwa wakati Joseph Guede aliyesajiliwa na Yanga dirisha dogo akiwa na bao moja pekee alilofunga kwenye Ligi ya Mabingwa.

Kabla ya kiwango kikubwa cha Aziz KI msimu huu Yanga ilibebwa na aliyekuwa mshambuliaji wao Fiston Mayele aliyeuzwa Pyramids ya Misri ambaye alifunga mabao 17 kwenye ligi msimu uliopita.

Yanga inapiga hesabu za kuongeza washambuliaji wawili kwenye dirisha lijalo la usajili, beki mmoja, kiungo mmoja na kipa mmoja katika kukiboresha zaidi kikosi chao.

Aziz KI amewaambia mabosi wa Yanga kuwa endapo kikosi hicho kitajazwa watu wa maana zaidi kwa kukiongezea nguvu timu hiyo inaweza kuchukua taji la Afrika akiridhishwa pia na namna mabosi hao wanavyoisimamia timu yao ndani ya miaka miwili aliyodumu hapo.

Katika mahojiano yake na Mwanaspoti hivikaribuni Azizi alisema; “Sina nia ya kuondoka hapa nimeletwa kwa sababu maalumu kama mpango huo hautokamilika nitaendelea kusalia kuitumikia timu ninayoipenda kwa moyo wangu wote hata fedha haitaweza kujaza upendo nilionao kwa timu hii,” alisema Aziz KI na kuongeza;

“Rais Hersi Said alinisainisha hapa kwa sababu ana malengo ya kuona timu hii inatwaa mataji ya kimataifa hili sikuwashirikisha kuwa nitakuwa hapa kwa kufanya hayo naomba mfahamu kwanini aliniamini na kunileta hapa yeye pamoja na kamati yake.”

Aziz Ki alisema; “Nina deni kubwa na timu na nitapambana kwa kusaidiana na wenzangu tuweze kufikia malengo hasa kutwaa mataji ya kimataifa, Yanga ni maisha yangu. makubwa ambayo naweza kuyaeleza lakini ambayo yanapiga sana moyoni mwangu sisi sote ni familia ya Rais Hersi ambaye ninaweza kumuelezea kama baba na washiriki kadhaa,” alisema Aziz KI na kuongeza;

“Katika klabu hii lazima nipambane ili niwe katika kiwango cha klabu hii ambapo inastahili kiwango cha juu na nitakaa hapa mpaka nifike huko ambao ninawiwa na nyinyi mashabiki wote kwa sababu mapenzi yenu kwangu hayana thamani kamwe ni makubwa sana.

“Natumai kupona kutoka kwa tamaa hii ya kibinafsi haraka iwezekanavyo na nipe yaliyo bora zaidi katika siku zijazo na tuonane mwaka ujao.”

GAMONDI KUHUSU USAJILI

Gamondi alisema wakati timu yake inaelekea mwisho wa msimu moja ya eneo ambalo litakwenda kutazamwa kwa umakini ni kutafuta mshambuliaji ambaye atakuja kuongeza kitu kikubwa zaidi kulinganisha na vijana alionao.

“Tunaweza kufurahia kazi ambayo inafanywa na Clement (Mzize), Musonda (Kennedy) na hata Guede (Joseph) lakini kwangu mimi bado tunahitaji kitu kikubwa zaidi endapo mambo yataendelea kuwa kama ambavyo tulivyo sasa, tunatakiwa kuwa na ubora wa kumaliza mechi kubwa.”

Gamondi alisema atatumia dirisha lijalo mara baada ya kumalizika kwa msimu kushirikiana na wenzake kuleta mshambuliaji wa maana wa kuibeba timu kama ilivyokuwa kipindi Fiston Mayele akiichezea kabla hajaja na kiuifikisha timu fainali ya Kombe la Shirikisho msimu uliopita. Endelea kutufuatilia kupitia mitandao yetu ya kijamii.