Azam FC yajisalimisha zake CAF mapema

Basi la Azam
Muktasari:
Kwa mujibu wa meneja wa Azam, Jemedari Said, timu hiyo imepeleka majina ya kikosi kilichoshiriki michuano hiyo msimu uliopita na kufanya marekebisho madogo ya kuwapunguza wachezaji wasiokuwepo kikosini sasa.
AZAM FC imetuma majina ya kikosi chake kitakachoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika huku ikitema wachezaji watano na kuongeza wengine sita katika timu iliyoshiriki mwaka jana.
Kwa mujibu wa meneja wa Azam, Jemedari Said, timu hiyo imepeleka majina ya kikosi kilichoshiriki michuano hiyo msimu uliopita na kufanya marekebisho madogo ya kuwapunguza wachezaji wasiokuwepo kikosini sasa.
Wachezaji walioongezwa ni Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Said Moradi, Kone Ismail Mohamed, Joseph Kimwaga na Farid Mussa.
Walioachwa ambao pia hawamo katika kikosi cha Azam kwa sasa ni Uhuru Selemani, Abdulhalim Humoud, Humphrey Mieno, Jockins Atudo na Abdi Kasim ‘Babi’.
Msimu uliopita wa michuano hiyo, Azam haikuwajumuhisha Aggrey, Nyoni na Moradi baada ya kuwatuhumu kupokea rushwa katika mchezo dhidi ya Simba. Azam itacheza mechi yake ya kwanza ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Ferroviario Da Beira ya Msumbiji Februari 9, mwaka huu kwenye Uwanja wa Chamanzi, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Majina ya kikosi kamili yaliyotumwa CAF ni makipa: Wandwi Jackson, Mwadini Ally na Aishi Manula. Mabeki: Waziri Salum, Aggrey, Nyoni, David Mwantika, Malika Ndeule, Lackson Kakolaki, Himid Mao na Moradi. Viungo: Joseph Kimwaga, Ibrahim Mwaipopo, Kipre Bolou, Salum Aboubakary ‘Sure Boy’, Jabir Azizi, Khamisi Mcha, Samir Haji, Kone na Farid Mussa. Washambuliaji: John Bocco, Abdallah Seif, Kipre Tchetche, Gaudence Mwaikimba na Brian Umony.