Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam FC, Ibenge kuna kitu

IBENGE F Pict

Muktasari:

  • Na kama huamini, mazungumzo yanayoendelea kwa sasa ndani na nje ya timu za Bara yanatarajiwa kutikisa mara tu dirisha la usajili wa wachezaji litakapofunguliwa, kwani kuna sapraizi kibao.

Unaambiwa kwamba mambo ni moto! Kila timu inasuka kikosi chake kimyakimya, lakini kuna mambo huenda yakashangaza msimu ujao wa Ligi Kuu Bara nje na usajili wa mastaa vikosini.



Na kama huamini, mazungumzo yanayoendelea kwa sasa ndani na nje ya timu za Bara yanatarajiwa kutikisa mara tu dirisha la usajili wa wachezaji litakapofunguliwa, kwani kuna sapraizi kibao.


 



Uongozi wa Azam FC tayari upo kwenye mazungumzo na kocha wa Al Hilal ya Sudan, Florent Ibenge ili kukinoa kikosi hicho kwani jina lake lilianza kutrendi hapa nchini wakati ule akiwa zake AS Vita ya kwao DR Congo.

Kabla ya kufikia hatua hiyo, Juni 13, mwaka huu, Mwanaspoti liliripoti kuwa Azam ipo kwenye mazungumzo na kocha wake Rachid Taoussi kwa ajili ya kuvunja mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Azam FC, kimeliambia Mwanaspoti kuwa wakati wanaendelea na mchakato wa kumalizana na Taoussi tayari wameanza kufanya mazungumzo na baadhi ya makocha kuziba nafasi hiyo.

“Bado tuna mechi mbili kumaliza msimu ambao hata hivyo hatujafikia malengo tuliyokuwa tumejiwekea, hivyo tunasubiri tumalize ndio tutoe taarifa ya kumalizana na kocha wetu. Kwa sasa nguvu zipo kwenye mechi za mwisho,” kilisema chanzo hicho.

“Kuhusu mchakato wa kutafuta benchi jipya la ufundi kwa msimu ujao unaendelea kimya kimya na tunatarajia kushusha kocha mwenye CV kubwa kama mambo yataenda kama tulivyopanga.”

Chanzo hicho kiliongeza kuwa mabadiliko yatakuwa makubwa msimu ujao kuanzia benchi la ufundi hadi wachezaji ambapo wana mpango wa kuunda kikosi bora kitakachotoa chachu michuano ya ndani na kimataifa.

Katika mabadiliko ambayo Azam imeanza kuyafanya ni kumsajili kipa Aishi Manula aliyekuwa Simba ili kwenda kuchukua nafasi ya Msudan, Mohamed Mustafa, pia ikimnasa kiungo aliyekuwa akicheza Misri, Muhsin Malima, huku ikisaka mbadala wa mshambuliaji Gibril Sillah mwenye mabao tisa anayedaiwa kumalizana na Yanga.

Ikumbukwe kuwa, Taoussi alijiunga na Azam Septemba 5, 2024 ambapo aliikuta timu ikiwa tayari imeondoshwa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ilipokuwa ikinolewa na Youssoupha Dabo. Wakati Azam FC ikituma ofa kwa Ibenge, inaelezwa kocha huyo mkataba wake na Al Hilal unatamatika Juni 30 mwaka huu.