Aveva, Kaburu wiki mbili zingine ndani

UPELELEZI wa kesi inayowakabili vigogo wa Simba akiwemo Rais wake, Evans Aveva bado haujakamilika kesi imeahirishwa hadi Desemba 14, 2017.
Kesi inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Victoria Nongwa. bali na Aveva, mshtakiwa mwingine ni makamu wa rais wa klabu hiyo,
Geofrey Nyange ‘Kaburu’, ambao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ikiwa na mashitaka matano.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka ya kughushi, kuwasilisha
nyaraka ya uongo na kutakatisha wa Dola za Marekani 300,000.
Kwa upande wa kesi inayowakabili vigogo watatu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), akiwemo aliyekuwa rais wake, Jamal Malinzi nayo imeahirishwa hadi Desemba 14,2017 kwa sababu upelelezi bado haujakamilika. Kesi inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Washitakiwa wengine ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine na Mhasibu, Nsiande Mwanga.