Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aucho agusia ishu ya Yanga kukata upepo, anamkubali Kagere

TUNAENDELEA pale tulipoishia jana na mahojianoa ya kiungo wa Yanga, Khalid Aucho ambaye katika toleo lililopita aliishia kuzumzia ubora wa Yanga ya sasa.

Akizungumzia utani wa jadi na kiwango cha Simba anasema; “Nilikuwa nacheza Kenya kule kulikuwa na ushindani wa watani kati ya Gor Mahia na FC Leopard nilicheza bila wasiwasi na sasa nipo hapa Tanzania na Yanga nafahamu kwamba watani wao ni Simba hilo mimi wala halinipi shida kitu muhimu ni kufanya kazi yangu vile unavyotakiwa kufanya, mimi sio mchezaji ninayeogopa mechi au ushindani nawaheshimu Simba ni timu nzuri lakini naamini Yanga tuko bora zaidi yao.

“Kuna kitu kama mazoea hapa Tanzania kwa kipindi kifupi naona ukimuona shabiki wa Yanga utakuta anafuatilia nini kinaendelea Simba na ukiona shabiki wa Simba atakuwa naye anafanya hivyohivyo kufuatilia maisha ya Yanga hii sio nzuri hasa unapotaka ufanikiwe.

“Kama una ndoto za kushinda mataji hututakiwi kuiangalia Simba peke yake tuangalie mechi zetu zote na tupambane kwa ajili ya timu,huwa napenda kuelekeza akili yangu katika timu ambayo tunapambana nayo mbele na nikimaliza hiyo naachana nayo nafuata nyingine iliyo mbele.


JAMAA NA MIKWARA

Akizungumzia madai ya mashabiki kwamba Aucho ana nguvu nyingi Aucho anasema kama watu wanadhani ametumia nguvu zake sana mpaka sasa wanakosea kazi ndiyo kwanza inaanza

“Mimi bado sijaanza kuonyesha ubora wangu ninaoujua,kweli bado sijafanya kile ambacho najijua kwamba sasa niko katika kiwango bora ndio kwanza tumeanza ligi ninachoshukuru Mungu sijapata majeruhi yoyote tangu nimefika maisha yakiendelea kuwa hivi naamini watu watafurahi zaidi wasiwasi wangu ni mambo ya majeruhi ambayo huwa yanarudisha nyuma sana lakini kama hiyo hali haitakuwepo na nikaendelea kucheza kila mechi nafikiri kutakuwa na mambo yanaongezeka kuhusu ubora.


ANACHUKIA KUSIKIA YANGA WANAKATA UPEPO

Ambacho mashabiki wengi walikuwa wanapiga kelele katika mechi mbili za kwanza za Yanga ni kwamba kikosi hicho kinakata upepo kipindi cha pili Aucho amewajibu hapa.

“Huwa nasikia hizo kelele kwamba watu wanadai Yanga huwa inapoteza pumzi kipindi cha pili huwa nashangaa unaona tunaongoza goli mbili lakini bado unataka tukimbizane bila hesabu mpira hauko kama hivyo,sijui kama huwa wanaangalia Barcelona wakati ule kabla haijapoteza ubora cha hii ya sasa, Barcelona kama wakiwa wanaongoza mabao manne huwa hawakimbizani tena huwa wanatulia na kucheza kwa hesabu wakimfanya mpinzani kutoleta madhara kwao.

“Ni kama pia klabu za Uarabuni unaposikia timu imeshinda tano sio kwamba walikuwa wanakimbizana muda wote kuna wakati ndani ya mchezo unakuwa na uhakika sasa umekaribia kushinda baada ya hapo unatuliza wapinzani wakose madhara na ukipata nafasi mnapiga pasi za kwenda kuongeza ushindi,hutakiwi kukimbizana na mpira unachotakiwa ni kuufanya mpira ukimbie badala yako.


DIARRA KIPA HASA

“Yanga kutoruhusu kwetu bao mpaka sasa sio kwamba tuna mabeki bora pekee, sawa nakubaliana na hilo tuna mabeki wazuri wanaocheza kwa utulivu lakini acha niwaambie siku zote timu bora yenye safu bora ya ulinzi lazima iwe na golikipa mzuri kama una kipa mzuri mtafanikiwa kwa hiyo hapa Yanga tuna kipa bora sana (Diarra Djigui) na niseme tu sio tu Diarra waona hata wale wengine wawili Rama (Ramadhan Kabwili) na Eric (Johola) nao ni bora sana kwahiyo hiyo ndio siri kubwa angalia jinsi anavyokuwa na hesabu nzuri pale langoni mkicheza naye anacheza mkitaka kuokoa naye anakuwa sehemu ya kusaidia.

“Kitu bora ambacho Yanga wamekifanya msimu huu ni kuwa na watu bora watatu katika kila nafasi hii kitu ndio inatuongezea ubora kutokana na ushindani wa nafasi,ukiwa peke yako katika nafasi ni rahisi kiwango chako kushuka kwa kuwa unakosa kitu cha kushindana na wewe,nitolee mfano nafasi yangu kuna Bangala,Mukoko na Mauya utaona wote tuko bora sana sasa kila mmoja anajituma sana kuanzia mazoezini na hata kwenye mechi ili ule ubora wake ndio utakaomsaidia kupata nafasi ya kuanza.


MPANGO WA ULAYA

“Kabla sijasaini Yanga nilikuwa na ofa tano mbili kutoka Ubelgiji na zingine Misri,narudia kuna maisha niliyapitia nikiwa Misri nilikuwa nacheza karibu kila mechi lakini maisha yangu yalikuwa magumu sana pale unapambana kila mechi lakini hulipwi nilichofanya nikawashtaki kwa Fifa na wakazuiwa kusajili mchezaji yoyote mpaka wanilipe sasa sidhani kama ni rahisi kwangu kurudi kwenye aina hiyo ya maisha tena.

“Nilimuonyesha hata injinia (Hersi Said) ofa ambazo nilikuwa nazo wakati tunazungumza na viwango vya fedha ambazo walikuwa wanataka kunipa ni nyingi kuliko zile za Yanga lakini nilisema acha nirudi huku na sasa nataka kutulia kwanza.”


KUOGELEA, MUZIKI

“Napenda sana kuogelea hiki ndio kitu kikubwa kwangu ninapokuwa kwenye mapumziko lakini pia napenda kusikiliza muziki mzuri.”


ANAMKUBALI KAGERE

“Nilikuwa namtumia jezi kama kumbukumbu na yeye aliwahi kunipa jezi yake ya Simba niliona kuna wakati nataika kuja hapa watu waliizungumzia sana lakini mimi sio mtu ninayependa kufuatilia vtu vya mitandao.”


FAMILIA YAKE VIPI?

“Sijaoa lakini nina watoto watatu kati ya hao wakiume ni wawili na wa kike mmoja na nafurahi nawalea watoto wangu lakini sikai na mama zao bado sijaamua. Mmoja wa kiume ni Mtanzania.