Amrouche kuchukua wengine Zanzibar

SHIRIKISHO la Soka Zanzibar (ZFF) limeandaa michezo miwili maalum ya mchanganyiko wa wachezaji wanaofanya vizuri kwa sasa katika Ligi kuu Soka Zanzibar.
Lengo la Michezo hiyo ni kumpa nafasi kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Adel Amrouche pamoja na benchi lake la ufundi ambalo litakuwepo uwanjani kwaajili ya kuchagua wachezaji ambao watajumuishwa moja kwa moja kwenye kikosi cha Taifa Stars.
Michezo hiyo miwili itafanyika leo, Novemba 23 na kesho Novemba 24 katika Uwanja wa Mau A, kuanzia saa 1:00 usiku.
Kikosi cha Taifa Stars kinakabiliwa na michezo ya AFCON yanayoanza mwakani.
Tanzania imepangwa kundi F ambalo watakutana na Morroco ambayo imetoka kuwacharaZA mabao 2-0 kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, pia wapo Zambia na DR Congo.
Kocha Adel Amrouche amekua ni muumini ya kuwapa nafasi vijana kwenye kikosi chake, hivyo anaamini Zanzibar pia kuna vipaji ambavyo vitaweza kuleta tija kwenye kikosi chake.