Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ambundo, Anuary kumpima Kabwili

Muktasari:

  • Dodoma Jiji imejihakikishia kucheza msimu ujao kufuatia kuwa na alama 43 ambazo hazitafikiwa na timu zilizopo kwenye eneo la kushuka daraja.

Dodoma. WACHEZAJI Dickson Ambundo na  Anuary Jabir wa Dodoma Jiji, ndio wamepewa jukumu la kuongoza mashambulizi dhidi ya Yanga.

Ambundo, ambaye anatajwa kuwa kwenye rada za Yanga kwa msimu ujao, amekuwa mwiba mkali kwa mabeki wa timu pinzani msimu huu, akihusika kwenye mabao 12 kwa timu yake.

Kasi yake kutokea pembeni, imekua na madhara kwa timu pinzani, ikiwalazimu mabeki wa Yanga leo kutakiwa kumchunga.

Anuary Jabir, ambaye alichangia kupanda kwa timu hiyo ligi kuu, majeraha yaliyomuweka nje kwa muda mrefu raundi ya kwanza ya ligi, yalimnyima fursa ya kung'ara msimu huu.

Hata hivyo, mshambuliaji huyo amefunga mabao matano kwa timu yake, huku akiwa mmoja ya wachezaji walioshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, aliyobeba mwezi Februari.

Mbali na nyota hao wawili hatari, wengine waliopewa nafasi ya kuanza mchezo huu ni Cleophas Mkandala, Mcha Khamis na Jamal Mtegeta, wanaocheza sambamba na Anuary na Ambundo kwenye eneo la ushambuliaji.

Wengine ni kiungo Enrick Nkosi, mabeki Justine Omary, Mbwana Kibacha,  John Wawa na Abubakar Ngalema.

Kocha Mbwana Makata wa Dodoma Jiji pia ameendelea kumuamini kipa chaguo la tatu, Hussein Dotto, ambaye huu ni mchezo wake wa tatu mfululizo anacheza.