Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Al Ahly, Berkane zatangulia makundi Afrika

Muktasari:

  • Al Ahly ndio watetezi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya msimu uliopita kutwaa kwa mara ya 11, ikiwan ni kati na mataji 24 ya michuano yote ya Afrika.

WAKATI kikosi cha Yanga kikijiandaa kushuka uwanjani usiku wa leo kurudiana na Al Merrikh ya Sudan katika mechi ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, timu tatu za Pyramids, Al Ahly zote za Misri na Jwaneg ya Botswana zimekuwa za kwana kundi makundi ya michuano hiyo kwa msimu huu.

Pyramids iliyolazimishwa suluhu ugenini na APR ya Rwanda katika mechi ya kwanza, usiku wa kuamkia leo ikiwa nyumbani ilishinda mabao 6-1 na kutinga makundi baada ya kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Mostafa Fathi kufunga mabao manne, huku Walid El Karti na Mohamed Chibi wakiongoza moja moja.

Wageni APR ilipata bao la kufutia machozi dakika nne kabla ya pambano hilo lililopigwa Cairo, Misri kumalizika, huku ikishuhudiwa straika wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele akiendelea kuwa na ukame wa mabao kwani hajaanza kucheka na nyavu. Mayele ndiye aliyekuwa mfungaji bora wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na Yanga kwa kufunga mabao saba, pia akinyakua tuzo ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara akilingana mabao 17 sawa na Saido Ntibazonkiza wa Simba.

Katika mechi nyingi iliyopigwa jana usiku, Orlando Pirates ya Afrika Kusini iling'olewa kwa mikwaju ya penalti 5-4 na Jwaneg Galax, licha ya ushindi wa bao 1-0 iliyopata nyumbani, kwani awali ilipoteza ugenini pia kwa bao 1-0 ndipo ikaamuriwa timu hizo zikipigane penalti na Wasauzi wakaaga mapema.

Jwaneg ndio waliowahi kuing'oa Simba katika Ligi ya Mabingwa misimu miwili iliyopita na Wekundu kuangukia Kombe la Shirikisho ilipopenya kwenye play-off na kwenda kukwamia Robo Fainali ikitolewa na Orlando.

Watetezi wa michuano hiyo, Al Ahly ya Misri haikuwa na kazi kubwa kwenye mechi ya marudiano ikiwa nyumbani dhidi ya St George ya Ethiopia kwani iliifumua mabao 4-0 na kufanya itinge makundi kwa kishindo kwa ushindi wa jumla wa mabao 7-0, kwani mechi ya kwanza ugenini ilishinda 3-0. Timu hizo tatuz zimejihakikisha hadi sasa kuvuna Dola 700,000 (zaiidi ya Sh 1.8 Bilioni za Kitanzania) kwa kutinga hatua hiyo, huku ikizisubiri timu nyingine 13 zitakazoungana nazo baada ya mechi za leo na kesho.

Kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika timu ya SuperSport United ya Afrika Kusini iliungana na RS Berkane ya Morocco kutangulia makundi kwa msimu huu baada ya kuifumua Gaborone United ya Botswana kwa mabao 3-0 na kutinga kwa jumla ya mabao 4-1 kwani awali ililazimishwa sare ya 1-1 ugenini.

Mabao mawili ya Mnigeria Etiosa Ighodaro katika dakika za 57 na 72 pamoja na lile la Bradley Grobler dakika za lala salama ziliwabeba wenyeji SuperSport, huku kwenye mechi nyingine mabingwa wa Shirikisho misimu miwili iliyopita, Berkane ilitakata nyumbani kwa kushinda bao 1-0 baada ya awali kulazimishwa sare ya 2-2 ugenini na Bendel ya Nigeria. Timu hizo mbili zimejihakikisha kuvuna Dola za Kimarekni 400,000 (zaidi ya Sh 1 Bilioni za Kitanzania).