Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Muktasari:

Shirikisho la Soka Afrika (Caf), limeipa nafasi Tanzania kuandaa fainali hizo baada ya kukidhi vigezo vikiwemo ubora wa viwanja na masuala ya usalama.

ACHANA na nafasi iliyopewa Tanzania kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Vijana ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) chini ya umri wa miaka 17 yaliyopangwa kuanza kutimua vumbi Aprili mwaka huu. Inshu kubwa kwa sasa ni namna nchi na wachezaji watakavyojitengenezea mazingira mazuri ya kutangaza vipaji.

Shirikisho la Soka Afrika (Caf), limeipa nafasi Tanzania kuandaa fainali hizo baada ya kukidhi vigezo vikiwemo ubora wa viwanja na masuala ya usalama.

Fursa hii kwa Tanzania kupewa uenyeji wa mashindano haya imekuja kwa bahati ya aina yake kwa kuwa nchi mbalimbali zilituma maombi ya kuandaa fainali hizo kabla ya Caf kutoa uamuzi.

Mashindano hayo yanayotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Taifa na Chamazi, Dar es Salaam, yatashirikisha nchi nane ambazo ni Morocco, Guinea, Senegal, Nigeria, Cameroon, Angola, Uganda na wenyeji Tanzania.

Mbali na Tanzania kunufaika kiuchumi kupitia mashindano hayo, faida nyingine ni kujitangaza katika soka la kimataifa kwa kuwa idadi kubwa ya mawakala watakuwa wakifuatilia michuano hiyo ili kubaini vipaji.

Idadi kubwa ya timu zinazoshiriki tayari zimeanza maandalizi ya mashindano hayo zikiamini hakuna njia ya mkato zaidi ya kujiweka sawa lakini kwa upande wa Tanzania ni giza nene kwani hadi sasa haijajulikana ni lini timu itakaa pamoja.Ni mataifa manane yanatatarajia kushiriki mashindano hayo huku Tanzania akiwa mwenyeji lakini hadi sasa haionyeshi kama kuna mashindano mbele, kwani hakuna hamasa zozote zinazotolewa wala matangazo katika vituo mbalimbali vya redio kuyapromoti mashindano hayo.

Muda hausimami unakimbia kama mshale wa saa, Aprili sio mbali sana kama inavyodhaniwa na waandaaji wa mashindano hayo ambayo kwa jumla yana tija kwa nchi kwani yataongeza kipato kwa serikali kutokana na kodi. Pia, yatatoa fursa kwa Watanzania waliowengi katika biashara zao kutangaza vipaji vya soka kwa vijana wanaotarajia kushiriki.

UKATA

Tanzania ndio ilikuwa mwenyeji wa mashindano kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa Vijana U-17, Kanda ya Cecafa na kufungwa mabao 3-1 na Uganda.

Mashindano hayo kwa namna moja au nyingine yalikuwa na chachu kwani yalianza kutangazwa mapema na timu iliandaliwa vizuri lakini huwezi kuamini hadi sasa timu imeshindwa kuingia kambini kujiandaa na mashindano makubwa yaliyombele yao.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Oscar Milambo amekiri ni kweli kuna tatizo katika uandaaji wa kikosi chake kwani alikuwa na mpango wa kuhakikisha anakiingiza kambini mapema ili kiweze kuwa cha ushindani lakini kutokana na kukosekana kwa fedha ameshindwa kufanya hivyo.

MAANDALIZI OVYO

Asilimia kubwa ya wawakilishi wa mataifa yanayotarajia kushiriki mashindano hayo yameanza maandalizi kwaajili ya kuonyesha ushindani katika kuwania ubingwa wa AFCON mapema mwaka huu.

Serengeti Boy hadi sasa haijulikani itakusanya nyota wake lini ili iweze kuanza maandalizi kwaajili ya kuiwakilisha nchi vizuri ikiwa mwenyeji.

Tangu imetoka Botswana ilikotwaa Kombe la Michuano ya Vijana kwa nchi za Kusini mwa Afrika (Cosafa) haijakutana pamoja kufanya maandalizi yoyote kwaajili ya mashindano hayo.

Achilia mbali kukutana, nyota hao hawana timu za kuchezea ambazo zinaweza kuwaweka fiti zaidi na kuweza kuonyesha ushindani katika mashindano yaliyombele yao. Hapo kuna jambo linatakiwa lifanywe na Watanzania kwa ujumla ili kuiwezesha timu yao iweze kubakiza ubingwa nyumbani.

KOCHA MPYA

Hili sio jambo geni kwa Watanzania, kubadilisha kocha baada ya viongozi kupanga kumleta kocha mwingine kutoka mataifa ya nje ili aweze kukinoa kikosi cha Serengeti. Jambo hilo limewaibua wadau wengi ambao hawakuelewa nia ya serikali kutaka kufanya hivyo wakati kocha aliyepo ameiwezesha timu kutwaa mataji mengi.

WAPINZANI WAO

Serengeti ina mtihani mgumu katika kundi lake, inatarajia kukutana na kigingi cha timu kutoka Nigeria ndio timu inayoogopwa zaidi na mashabiki wa Tanzania, kutokana na ubora iliyonao mbali na hilo pia historia ya taifa hilo inawabeba vijana wao ambao mbali na kuwa na utamaduni wa kuwakuza pia ndio nchi ambayo imetoa wachezaji wengi kucheza zoka la kulipwa nje ya taifa lao.

Tanzania inaonekana kuwa na vipaji vingi vya vijana wenye muunganiko mzuri kutokana na kuelewana zaidi hasa baada ya kutamba katika mashindano mbalimbali waliyoshiriki.

Lakini tatizo kubwa ni kutokuwa pamoja kwa muda mrefu na kushindwa kuingia kambini mapema kwa ajili ya kujiandaa tayari kubakiza kombe nyumbani.

Kutakuwa na kazi kubwa sana kwa Serengeti Boys kulibakisha kombe kama Watanzania na Serikali kwa jumla watashindwa kuona umuhimu wa mashindano hayo kwa kuiandaa timu mapema.

Itakuwa jambo la maana kama wachezaji hao wangekaa pamoja kwa muda mrefu na kupata timu za kuwapa maandalizi mazuri. Lakini kama timu hiyo itachelewa kuingia kambini na kupata mechi za majaribio tutarajie aibu kubwa mbele ya safari.

Ni nyota wachache ambao wapo katika timu zao na wanapata maandalizi ya kutosha wakiwa huko lakini wengi wapo majumbani wakifanya mazoezi wenyewe jambo ambalo linaweza kuwawia vigumu kufanya maandalizi kitaalamu.

Katika mazoezi tunajua kuna vitu vya kuzingatia ammbavyo vinapaswa kwa wakati mwafaka chini ya uangalizi wa kocha. Makocha wamekuwa wakitoa muda wa kufanya mazoezi ya nguvu na viungo kwa vyakati tofauti na baadaye hutoa mazoezi kwa ajili ya mbinu za kiuchezaji ndani ya dimba kwaajili ya mashindano yaliyo mbele yao. Mchezaji hasa wa U-17 hawezi kujipangia mazoezi hayo mwenyewe.