Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

21 kupigwa msasa Arachuga

Muktasari:

Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku tano kwenye uwanja wa Royal uliopo Sinoni ambapo yameandaliwa na Chama Cha Soka mkoa wa Arusha (ARFA) kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) idara ya ufundi

Arusha. Jumla ya wadau 21 kutoka mikoa ya Arusha na Morogoro wanaendelea kupatiwa mafunzo ya awali ya ukocha wa Mpira wa miguu (Grassroot) ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kufundisha soka la vijana.

Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku tano katika uwanja wa Royal uliopo Sinoni ambapo yameandaliwa na Chama Cha Soka mkoa wa Arusha (ARFA) kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) idara ya ufundi.

Katibu wa Arfa, Emmanuel Antony ameipongeza TFF katika juhudi zake za kuhakikisha wanapatikana makocha wengi ambao wataenda mitaani kuibua vipaji vingi vya vijana na kupata wachezaji watakao kuja kuiwakilisha taifa katika michuano ya kimataifa.

Amesema mafunzo hayo yamekuja kwa wakati muafaka na katika sehemu sahii ukizingatia vijana wengi wapo mtaani na wanakosa watu sahii wa kuweza kuwashika mkono hivyo mafunzo hayo yamekuwa ni fursa kwao katika kuendeleza Soka la Tanzania.

“Kozi hizi ni chache na hazifanyiki kila wakati kikubwa tunapotangaza wadau wajitokeze kwa wingi ili kushiriki tuache tabia za kukaa na kulalamika mpira haukui wakati fursa zikijitokeza watu hawashiriki”,

“Washiriki kutoka kwetu hapa Arusha ni 20 na mmoja anatokea huko Mvomera mkoani Morogoro ambapo pia tunatarajia baada ya kumaliza Jumamosi hii tutaendesha tena kozi ya CAF Diploma D”, amesema Antony

Mkufunzi kutoka TFF, Raymond Gweba amesema toka wameanza kutoa kozi ya awali kwa makocha mwitikio umekuwa mkubwa kwa makocha na mabadiliko makubwa yameonekana kwani vituo vingi vya kukuza vipaji vimeanzishwa na wengi wanaohusika ni hao waalimu ambao wamewafundisha.

“Washiriki watendee haki mafunzo pili wafanye mawasiliano na ofisi za FA mikoa kujua makocha na aina wanaohitajika kulingana na vituo vyao”, amesema Gweba

Emmanuel Shayo ni mshiriki anasema kupitia mafunzo hayo ataenda kuibua vipaji vingi na kuviendeleza ikiwemo watoto wake wenyewe ambao wameonyesha nia ya kutaka kutimiza ndoto zao za kucheza soka.

Kwa upande wake mkufunzi wa waamuzi Tanzania, Soud Abdi anasema kutengeneza ngazi nzuri kuwapata watu ambao wataenda kuibua vipaji kuanzia chini ni jambo nzuri hasa katika maendeleo ya soka hapa nchini.