Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nafasi za Mnguto, Kasongo zajazwa TPLB

Muktasari:

  • Juni 13, 2025, TFF ilitangaza kuwa Steven Mnguto amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) huku Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo Almas Kasongo akisimamishwa.

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imepata viongozi wawili wa kukaimu nafasi za Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu ambao Juni 13, 2025 waliondoka katika nafasi hizo kwa sababu tofauti.

Mwenyekiti wa Azam FC, Nassor Idrissa ‘Father’ anakaimu nafasi ya Mwenyekiti wa TPLB ambayo imekuwa wazi kufuatia kujiuzulu kwa Steven Mnguto.

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu, anayekaimu nafasi hiyo kwa sasa ni Ibrahim Mwayela ambaye awali alikuwa Meneja Fedha wa TPLB.

Nafasi ya Mtendaji Mkuu wa TPLB imekuwa wazi kufuatia kusimamishwa kwa Almas Kasongo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

Mwananchi Digital imethibitisha uteuzi wa vigogo hao wawili wanaokaimu nafasi hizo nyeti za TPLB kupitia barua ambayo Bodi imeandika kwenda kwa klabu kwa ajili ya kuwatambulisha.

“Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inakujulisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Nassor Idrissa amekaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo kwa mujibu wa ibara 33:5 ya Kanuni za Uongozi za TPLB.

“Nassor Idrissa ambaye ni mwenyekiti wa klabu ya Azam anakaimu nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Mwenyekiti, Steven Mnguto kuandika barua ya kujiuzulu mwishoni mwa juma lililopita.

“Katika hatua nyingine Meneja Fedha wa TPLB, CPA Ibrahim Mwayela ameteuliwa kukaimu nafasi ya Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), baada ya Almasi Kasongo kusimamishwa kazi mwishoni mwa juma lililopita . Bodi inatarajia ushirikiano wa dhati wa klabu yako kwa viongozi hao,” imesema barua hiyo.