Prime
Wazawa waongoza kwa mabao Bara

Muktasari:
- Ukiachana na hilo, Mwanaspoti linakuchambulia kwa njia ya data, kipindi cha kwanza cha mechi zote yamefungwa mabao 17 na cha pili 21, jambo ambalo wadau wa mchezo huo, wanaiona Ligi Kuu ya mwaka huu itakuwa ngumu na ushindani, ambao utazalisha mabao mengi, kwani hadi sasa zimechezwa jumla ya mechi 16
MSIMU huu (2023/24) unaonekana timu zimejipanga kulingana na jinsi mabao yalivyopatikana kabla ya Ligi Kuu Bara kusimama kupisha ratiba ya Fifa ya mechi za kimataifa. Hadi sasa yamefungwa jumla ya mabao 38, wazawa wakiongoza kwa kufunga 20 na wageni 18.
Ukiachana na hilo, Mwanaspoti linakuchambulia kwa njia ya data, kipindi cha kwanza cha mechi zote yamefungwa mabao 17 na cha pili 21, jambo ambalo wadau wa mchezo huo, wanaiona Ligi Kuu ya mwaka huu itakuwa ngumu na ushindani, ambao utazalisha mabao mengi, kwani hadi sasa zimechezwa jumla ya mechi 16. Kwa wastani ni sawa na yamefungwa mabao 2.4 kwa kila mechi.
KIPINDI CHA KWANZA
Agosti 15, 2023
Ihefu 0-1 Geita Gold
(Elias Maguri 5’).
Namungo FC 0-1 JKT TZ
(Martin Kigi 43’).
Agosti 16, 2023
Mashujaa 2-0 Kagera Sgr
Adam Adam dakika ya 15
Azam FC 4-0 Tabora Utd
(Feisal Salum ‘Fei Toto’ 3’, 9’, 13’, Prince Dube 5’).
Agosti 17, 2023
Mtibwa 2-4 Simba
(Matheo Anthony 20’, 22’) (Jean Baleke 5’, Onana 9’, Fabrice Ngoma 45’.
Agosti 20
Simba 2-0 Dodoma Jiji
Jean Baleke dakika ya 43.
Agosti 23, 2023
Yanga 5-0 KMC
Job dakika ya 17.
Agosti 28, 2023
Azam 3-1 Prisons
Prince Dube dakika 11.
Agosti 29, 2023
Yanga 5-0 JKT Tz
Aziz Ki dakika ya 45+.
JUMLA NI MABAO 16
KIPINDI CHA PILI
Dodoma Jiji 2-1 Coastal (Raizin Hafidh 53’, Meshack Abraham 60’ na Haji Ugando dakika 46 (Agosti 15).
Ramadhan wa Mashujaa dakika (73) dhidi ya Kagera iliyofungwa mabao 2-0 (Agosti 16).
Clatous Chama wa Simba dakika 81 dhidi ya Mtibwa (Agosti 17).
Agosti 19, 2023
Ihefu 1-0 Kagera Sugar (Moubarack Amza ‘79’).
Namungo FC 1-1 KMC
(Fabrice Ngoy (P) ‘80’) (Rashid Chambo ‘69’).
Agosti 20, 2023
Mtibwa Sugar 1-1 Coastal
(Kassim Haruna ‘84’) (Ibrahim Ajibu ‘70’)
Simba 2-0 Dodoma Jiji
Moses Phiri dakika 55
Agosti 23, 2023
Yanga 5-0 KMC
Aziz Ki 59’, Hafiz 70’, Mudathir 76’, Pacome Zouzoua 80’.
Agosti 28, 2023
Azam 3-1 Prisons
Idd Nado 47’, Nathaniel Chilambo 82’, Zabona Khamis wa Prisons 90’.
Agosti 29, 2023
Yanga 5-0 JKT Tz
Dickson Kibabage 54’, Yao Attohoula 65’ na Max Nzengeli (79’, 88’).
JUMLA MABAO 22
MITAZAMO YA WADAU
Nahodha wa zamani wa Simba, Mussa Hassan Mgosi ambaye kwa sasa ni kocha wa Simba B, ameeleza anavyoiona ligi hiyo:
“Ukiona yanapatikana mabao mengi kipindi cha kwanza na cha pili, inaonyesha fitinesi ya wachezaji ni kubwa, hivyo wanaweza wakafunga muda wowote ule,” alisema Mgosi aliyesifika kwa kutupia mabao enzi zake wakati akiitumikia Simba.
Kwa mtazamo wa kocha wa timu ya taifa ya ufukweni, Boniface Pawasa alisema kulingana na aina ya mabao hayo (38), ambayo kwa idadi bado hayatofautiani kwa kiasi kikubwa katika ya yale ya kwanza na cha pili, hiyo ni ishara kwamba msimu huu unaweza ukawa na mabao mengi; “Nikiangalia yamepishana idadi ndogo ya mabao kipindi cha kwanza na cha pili, hiyo inamanisha jinsi ambavyo timu zimejiandaa na kadri muda unavyokwenda ndivyo itakuwa ngumu zaidi.”