Vikosi vya thamani kubwa Big Six

LONDON. ENGLAND. JURGEN Klopp na Pep Guardiola wanamiliki vikosi vyenye thamani kubwa zaidi kwenye soka la dunia.

Ligi Kuu England, inaripotiwa kuwa ni mahali ambako kuna wachezaji wengi wenye thamani kubwa sokoni kwa sasa kwa mujibu wa Transfermarkt.

Wachezaji watano kati ya wanane wenye thamani inayozidi Pauni 100 milioni wapo kwenye Ligi Kuu England jambo linalofanya timu za ligi hiyo kumiliki vikosi vyenye thamani kubwa zaidi duniani. Kwa kuzingatia mtandao huo, hivi hapa vikosi vya vya kwanza vyenye mastaa wenye thamani kubwa kwenye Big Six, huku Liverpool ya Klopp na Manchester City ya Guardiola zikishika nafasi ya kwanza na ya pili mtawalia. Hawa hapa mastaa wenye thamani kubwa sokoni wanaounda vikosi vya Big Six kwenye Ligi Kuu England.

Arsenal - Pauni 360.45 milioni

Usajili mpya kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, beki Gabriel na kiungo Thomas Partey wanaingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza chenye thamani kubwa zaidi katika chama la Arsenal. Granit Xhaka (Pauni 25.20 milioni), Gabriel Martinelli (Pauni 22.50 milioni) na Eddie Nketiah (Pauni 18 milioni) ni wachezaji waliokosekana kwenye kikosi hicho cha wakali wenye thamani kubwa katika kikosi hicho cha Emirates kinachonolewa na kocha Mhispaniola, Mikel Arteta.

KIKOSI CHA KWANZA;

Kipa: Bernd Leno (Pauni 28.80milioni)

Beki wa kulia: Hector Bellerin (Pauni 28.80milioni)

Beki wa kati: William Saliba (Pauni 20.25milioni)

Beki wa kati: Gabriel Magalhaes (Pauni 25.20milioni)

Beki wa kushoto: Kieran Tierney (Pauni 28.80milioni)

Kiungo wa kulia: Nicolas Pepe (Pauni 36milioni)

Kiungo wa kati: Thomas Partey (Pauni 45milioni)

Kiungo wa kati: Dani Ceballos (Pauni 28.80milioni)

Kiungo wa kushoto: Bukayo Saka (Pauni 36milioni)

Mshambuliaji: Pierre-Emerick Aubameyang (Pauni 45milioni)

Mshambuliaji: Alexandre Lacazette (Pauni 37.80milioni)

Tottenham -

Pauni 429.30 milioni

Tottenham Hotspur inashika namba tano kwenye orodha ya timu zenye vikosi vyenye thamani kubwa kwenye Big Six katika mikikimikiki ya Ligi Kuu England wakiwazidi mahasimu wao wakubwa wa huko London, Arsenal. Supastaa, Gareth Bale mwenye thamani ya Pauni 22.5 milioni ni jina kubwa kabisa ambalo limekosekana kwenye kikosi hiki cha kwanza cha Spurs cha wakali wenye thamani kubwa sokoni, huku staa mwingine mpya anayekosekana ni Pierre-Emile Hojbjerg, naye ana thamani ya Pauni 22.5 milioni.

KIKOSI CHA KWANZA;

Kipa: Hugo Lloris (Pauni 10.80milioni)

Beki wa kulia: Matt Doherty (Pauni 18milioni)

Beki wa kati: Davinson Sanchez (Pauni 40.50milioni)

Beki wa kati: Eric Dier (Pauni 19.80milioni)

Beki wa kushoto: Sergio Reguilon (Pauni 25.20milioni)

Kiungo wa kati: Tanguy Ndombele (Pauni 36milioni)

Kiungo wa kati: Giovani Lo Celso (Pauni 31.50milioni)

Kiungo wa kulia: Steven Bergwijn (Pauni 25.20milioni)

Kiungo mshambuliaji: Dele Alli (Pauni 46.80milioni)

Kiungo wa kushoto: Heung-min Son (Pauni 67.50milioni)

Straika: Harry Kane (Pauni 108milioni)

Chelsea -

Pauni 482.40 milioni

Matumizi makubwa ya Chelsea kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi hayakutosha kuwaingiza kwenye tatu bora ya timu yenye kikosi chenye thamani kubwa zaidi kwenye Big Six ya Ligi Kuu England. Viungo Mateo Kovacic (Pauni 40.50milioni) na Hakim Ziyech (Pauni 36milioni) wanathaminishwa kwa thamani ya chini kuliko Jorginho na Mason Mount. Kocha, Frank Lampard ameboresha kikosi chake ili kuhakikisha kinaleta upinzani mkali kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

KIKOSI CHA KWANZA;

Kipa: Edouard Mendy (Pauni 18milioni)

Beki wa kulia: Reece James (Pauni 27milioni)

Beki wa kati: Antonio Rudiger (Pauni 27milioni)

Beki wa kati: Kurt Zouma (Pauni 27milioni)

Beki wa kushoto: Ben Chilwell (Pauni 45milioni)

Kiungo wa kati: Jorginho (Pauni 45milioni)

Kiungo wa kati: N’Golo Kante (Pauni 63milioni)

Kiungo wa kulia: Mason Mount (Pauni 40.50milioni)

Kiungo mshambuliaji: Kai Havertz (Pauni 72.90milioni)

Kiungo wa kushoto: Christian Pulisic (Pauni 54milioni)

Straika: Timo Werner (Pauni 63milioni)

Man United -

Pauni 524.70 milioni

Beki wa kushoto, Alex Telles na kiungo Danny van de Beek wanaingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza chenye thamani kubwa zaidi Manchester United, huku mastaa Bruno Fernandes, Mason Greenwood na Anthony Martial thamani zao zikiwa zimepanda zaidi baada ya kufanya vizuri kwenye msimu wa 2019/20. Kitu cha kushangaza, kipa David De Gea, Harry Maguire na Victor Lindelof viwango vya thamani zao zikishuka kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo, wameingia kwenye kikosi cha mastaa wenye thamani Man United.

KIKOSI CHA KWANZA;

Kipa: David de Gea (Pauni 31.50milioni)

Beki wa kulia: Aaron Wan-Bissaka (Pauni 36milioni)

Beki wa kati: Harry Maguire (Pauni 45milioni)

Beki wa kati: Victor Lindelof (Pauni 21.60milioni)

Beki wa kushoto: Alex Telles (Pauni 36milioni)

Kiungo wa kati: Paul Pogba (Pauni 72milioni)

Kiungo wa kati: Donny van de Beek (Pauni 39.60milioni)

Kiungo wa kulia: Mason Greenwood (Pauni 45milioni)

Kiungo mshambuliaji: Bruno Fernandes (Pauni 72milioni)

Kiungo wa kushoto: Marcus Rashford (Pauni 72milioni)

Straika: Anthony Martial (Pauni 54milioni)

Man City -

Pauni 682.20 milioni

Kwenye kikosi cha Manchester City, mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi kwenye Ligi Kuu England ni kiungo wa kushoto, Raheem Sterling. Kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya Etihad inayonolewa na Pep Guardiola inashika namba mbili kwa kuwa na thamani kubwa kwenye Big Six, licha ya kwamba wachezaji kama Riyad Mahrez (Pauni 43.20milioni), Ferran Torres (Pauni 40.50milioni) na Sergio Aguero (Pauni 37.80milioni) hawakuwekwa kwenye orodha ya mastaa waliongia kwenye kikosi cha kwanza.

KIKOSI CHA KWANZA;

Kipa: Ederson (Pauni 50.40milioni)

Beki wa kulia: Kyle Walker (Pauni 36milioni)

Beki wa kati: Aymeric Laporte (Pauni 54milioni)

Beki wa kati: Ruben Dias (Pauni 45milioni)

Beki wa kushoto: Nathan Ake (Pauni 36milioni)

Kiungo wa kati: Rodri (Pauni 57.60milioni)

Kiungo wa kati: Phil Foden (Pauni 54milioni)

Kiungo wa kulia: Bernardo Silva (Pauni 72milioni)

Kiungo mshambuliaji: Kevin De Bruyne (Pauni 108milioni)

Kiungo wa kushoto: Raheem Sterling (Pauni 115.20milioni)

Straika: Gabriel Jesus (Pauni 54milioni)

Liverpool -

Pauni 760.50 milioni

Si kitu cha ajabu kabisa kwa kikosi cha Jurgen Klopp kuongoza kwa kuwa na thamani kubwa kwenye Ligi Kuu England kwenye orodha ya Big Six. Kitu kinachoshangaza zaidi, safu ya mabeki ya Liverpool thamani yake imezidiwa kwa Pauni 15 milioni tu na thamani ya kikosi kizima cha Arsenal. Dharau hizi. Kikosi cha Liverpool thamani yake ni zaidi ya mara mbili ya kikosi cha Arsenal, tena hapo wachezaji Gini Wijnaldum (Pauni 36milioni) na Diogo Jota (Pauni 36milioni) hawajahusika.

KIKOSI CHA KWANZA;

Kipa: Alisson Becker (Pauni 72milioni)

Beki wa kulia: Trent Alexander-Arnold (Pauni 99milioni)

Beki wa kati: Virgil van Dijk (Pauni 72milioni)

Beki wa kati: Joe Gomez (Pauni 36milioni)

Beki wa kushoto: Andrew Robertson (Pauni 67.50milioni)

Kiungo mkabaji: Fabinho (Pauni 54milioni)

Kiungo wa kati: Thiago Alcantara (Pauni 43.20milioni)

Kiungo wa kati: Naby Keita (Pauni 36milioni)

Winga wa kulia: Mohamed Salah (Pauni 108milioni)

Straika: Roberto Firmino (Pauni 64.80milioni)

Winga wa kushoto: Sadio Mane (Pauni 108milioni)