VIDEO: Nandy ajihami video ya utupu kuzagaa mitandaoni, aibua gumzo
Video ya msanii Faustina Charles’Nandy’ inayomuonesha akiwa faragha na mwanaume leo imezua gumzo mitandaoni ambapo mwenyewe amefunguka na kueleza ukweli wote.
Akizungumza na MCL Digital, Nandy anayetesa na kibao chake cha Kivuruge muda mfupi uliopita amekiri kwamba video hiyo ni ya ukweli japo ni ya mwaka 2016 na kuwaomba Watanzania na serikali msamaha kwa walichokiona.
Akielezea zaidi amesema video hiyo ilichukuliwa akiwa katika mahusiano na mmoja wa wasanii wa Bongo Fleva (jina tunalihifadhi), ambapo walikubaliana mahusiano hao yawe ya siri.
“Sielewi ana maana gani kuitoa video hiyo kwa sasa na kufika kwenye mitandao, kwani ni vitu kama hivi vinafanyika kwa mtu yoyote anayekuwa kwenye mahusinao.
“Nimesikitishwa sana na kitendo kama hicho na ilishutiwa kwa mtindo wa snapchat na sijui kwa nini ameamua kuirushia sasa hivi, yaani sielewi nifanye nini.
“Naomba radhi kwa mashabiki wangu, familia yangu, kanisani kwangu, serikali kiukweli video imenichafua sana ila adhabu ya maamivu haya ninyoyapata sasa hivi ni kutokana na kumuamini mtu.
“Sina cha kusema kwani hiki sio kitu cha kwanza kwani nishakuwa na mahusiano na mtu huko nyuma na akatishia kutoa picha zangu mpaka pale nilipoenda kuripoti polisi.
Hata hivyo Nandy amewaasa vijana kuwa waangalifu wanapokuwa katika mahusiamo kwani tukio hilo wengi wamechukulia kama ni ‘kick’, ila waelewe hii sio hivyo na kueleza kuwa dhamira yake inajutia jambo hilo.
mwisho.