Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Timu 25 kuibeba AFC Chuga

ARUSHA.  ZAIDI ya timu 25 zinashiriki bonanza maalumu la soka kuichangia timu ya AFC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Bonanza hilo lililoandaliwa na uongozi wa timu hiyo, linafanyika kwa siku mbili - Jumamosi na Jumapili hii - katika Uwanja wa General Tyre mjini hapa.

Katibu msaidizi wa AFC, Bertha Ismail alisema kuwa timu hiyo iliingia kambini tangu Septemba Mosi na bado ina mahitaji mbalimbali, ndio maana wamefanya mchakato huo.

“Bajeti nzima ya msimu huu tuna uhitaji wa zaidi ya milioni 150, ambazo tumekwishapeleka barua za kuomba udhamini katika taasisi mbalimbali tukisubiri majibu, lakini bado na sisi wenyewe tunatafuta namna ya kupunguza makali ya gharama za kambi kama chakula, malazi, na vifaa vya mazoezi na malipo ya awali ya wachezaji na mwalimu kwa kufanya miradi,” alisema Bertha.

Alitaja timu za taasisi zinazoshiriki bonanza hilo kuwa kuwa ni RAS FC, B.O.T, TRA, Arusha Jiji FC, Watumishi FC (Monduli), Burka Coffee, Open University of Tanzania, Arusha All Stars, Executive Ngaramtoni, Wazee Club, Kitambi Noma na Nelson Mandela.

“Timu zingine ni Chuo cha Ufundi (ATC), Idara ya Maji (AUWSA), Tanesco, Polisi Arusha, TPRI, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Arusha DC, Tanapa, Bus Stand, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Chuo cha Maendeleo ya Jamii (TICD), Morani Monduli, Masai Rangers, Mto wa Mbu Veterani na Lambalamba FC.”

Berta alisema kuwa bado wana matumaini ya kupata mdhamini kwa msimu huu kutokana na majibu mazuri waliyoyapata kutoka kwa wadau waliowapelekea barua huku akilishukuru Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuwapatia kiasi cha Sh5 milioni ambazo wanaamini zitawasogeza.

Ofisa habari wa AFC, Yasinta Amos aliwataka wadau wa soka mkoani Arusha kujitokeza kuidhamini timu hiyo ili iweze kufanya vizuri huku akiwaahidi kuwafanyia matangazo kwa kupachika nembo ya taasisi husika katika jezi zao watakazozitumia.

AFC imekuwa ikipambana kurejea Ligi Kuu kwa muda sasa.