Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sheikh Amri Abeid kufumuliwa upya

Sheikh Amri Abeid kufumuliwa upya

ARUSHA. CHAMA Cha Mapinduzi ambao ndio wamiliki wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kimesema kinatarajia kutumia muda wa miezi mitatu kuufunga uwanja wao kwa ajili ya kufumua na kuotesha nyasi mpya za kisasa ili kubadili mwonekano wa uwanja huo eneo la kuchezea.

Akizungumzia hilo ofisini kwake, Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Gerald Munisi alisema wameona umuhimu wa kufanya hivyo baada ya nyasi hizo kuonekana kuzeeka hali inayochelewesha kurudisha ukijani wake hata ukimwagiwa maji baada ya kutumika.

“Tathimini kuwa tutatumia shilingi ngapi bado hatujafanya, kikubwa bado tunamalizana na mhusika wa kufumua nyasi hizo na baadae tutakuwa na vibarua wa kuotesha nyasi mpya tunazoamini zitapendezesha uwanja na kuwa mpya tena, maana nyasi hizi za miaka ya sabini kiukweli zimechoka,” alisema na kuongeza pia wanatarajia kurekebisha miundombinu yote kwa jumla.

“Huu uwanja una jina kubwa sana Tanzania na nje ya Tanzania lakini bila marekebisho na maboresho ya mara kwa mara utapoteza sifa zote, sisi kama chama tawala na wamiliki wake hatutaki hilo litukute hivyo niwaombe wadau watuelewe kwa hili.”

“Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wametupa dhamana ya kuwa wenyeji wa mchezo wa nusu fainali ya Kombe la AFSC hivyo tunashukuru kwa sifa hiyo na hii inaonekana wana imani kubwa na uwanja wetu, na sisi hatutaki kupoteza heshima hii, ili tupate michezo mingine mikubwa ya ndani na ile ya kimataifa,” alisema