Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Prisons yahamia kwa Azam

Muktasari:

  • Kwa misimu mitatu mfululizo Tanzania Prisons haijapata ushindi wowote kwa Azam ambapo kesho itakuwa ni rekodi na kisasi kwa wapinzani hao watakapokutana uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mbeya. Tanzania Prisons imekiri kuwa inapokutana na Azam huwa inachezea vichapo sasa kesho Ijumaa, inaenda kufuta uteja kwa kupata ushindi licha ya kuwakosa nyota wake saba wenye sababu mbalimbali.

Prisons haijapata ushindi kwa Azam kwa misimu mitatu mfululizo, ambapo mara ya mwisho kushinda ilikuwa April 2, 2019 kwa bao la Jumanne Elfadhil.

Kesho Septemba 30 timu hizo zitakutana kwenye uwanja wa Sokoine ambapo Azam inajivunia rekodi kwa Wajelajela hao ambao msimu uliopita iliwanyuka jumla ya mabao 5-0 ikianza kuwachakaza 4-0 ugenini kwenye uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa kisha kuwatungua 1-0 kwenye uwanja wa Chamazi Dar es Salaam.

Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Shaban Mtupa amesema kesho hawakubali kupoteza mechi ya pili mfululizo lakini kutokubali tena kuwa wateja kwa wapinzani hao kwani vipigo vimetosha.

Amesema pamoja na maandalizi na matumaini makubwa waliyonayo kufanya kweli, watawakosa nyota wake saba ambao wana sababu mbalimbali ikiwamo majeruhi, kadi nyekundu na majukumu kwenye timu ya Taifa ya Vijana (U20).

"Nurdin Chona, Salum Kimenya na Mussa Mbisa hawa ni majeruhi, Oscar Paul na Edwin Balua wako timu ya Taifa, Michael Masinda ana kadi nyekundu, lakini waliobaki wako tayari kwa mapambano na tunaamini kesho ni ushindi." amesema Mtupa.

Kocha huyo ameongeza kuwa kwa muda waliokaa mapumziko kwa takribani wiki mbili, wamefanyia kazi mapungufu yote hususani sehemu ya ushambuliaji ambao mechi iliyopita na Simba walishindwa kufanya vizuri na kujikuta wakipoteza mechi hiyo kwa bao 1-0.

Naye Nahodha wa timu hiyo, Benjamin Asukile amesema mchezo huo utakuwa wa kisasi kwani wapinzani hao waliwafanyia kitu mbaya msimu uliopita na kwamba baada ya mechi na Simba, kwa sasa stori kubwa kwao kambini ilikuwa ni Azam.

"Itakuwa mechi ya kisasi, Azam walitufanyia kitu kibaya, tumekuwa tukifungwa sana tunapokutana nao, hivyo kesho tunaenda kulipiza, kukosekana kwa baadhi ya wachezaji haiwezi kutuathiri sisi wengine kwa sababu wachezaji wote wa Prisons wanaweza kuanza kikosi cha kwanza" amesema Asukile.