Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbape, Maurice, Ngoda waongoza jeshi Uturuki

Muktasari:

  • Kikosi cha Serengeti kiliweka kambi jijini Arusha na kuchanganyishwa na wachezaji wengine waliofanyiwa usaili na Mkurugenzi wa Ufundi Ammy Ninje, hata hivyo benchi la ufundi liliamua kutoa wachezaji 20 kwenda kuiwakilisha Tanzania

WACHEZAJI Kelvin John ‘Mbappe’ na Maurice Abraham wanaongoza msafara wa wachezaji 20 wanaoenda kucheza mashindano ya Uefa Assist nchini Uturuki yanayotarajia kuanza Machi 3.

Kikosi cha Serengeti kiliweka kambi jijini Arusha na kuchanganyishwa na wachezaji wengine waliofanyiwa usaili na Mkurugenzi wa Ufundi Ammy Ninje, hata hivyo benchi la ufundi liliamua kutoa wachezaji 20 kwenda kuiwakilisha Tanzania katika Mashindano hayo.

Katika kikosi ambacho kinaenda nchini Uturuki chote ni kikosi ambacho kilikuwa na kocha Oscar Milambo katika Mashindano yaliyofanyika awali.

Wakati huo wale ambao wamesalia nchini watakuwa wapo chini ya uangalizi maalum na kuungana na wenzao pindi watakaporejea.

Wachezaji wanaoondoka kwenda Uturuki ni; Alphonce Msanga, Mustapha Nankuku, Charles Masenga,Dominick William, Amir Njeru, Kelvin John, Ladack Juma, Ally Hamis na Edmund Godfrey.

Pia wamo; Maurice Abraham, Mwinyi Abdallah, Said Zanda, Tepsi Evance, Mohammed Omar, Benard Castory, Agiri Ngoda, Shaaban Kimwaga, Edson Mshirakandi, Jefferson Mwaikambo na Pascal Msindo.

Baada ya mashindano ya Uturuki, Serengeti Boys watarejea Machi 23 na siku mbili baadaye watakwenda Kigali, Rwanda kwenye mashindano ya vijana yatakayoanza Machi 29 hadi Aprili 3 na watarejea Aprili 5, siku tisa kabla ya kuivaa Nigeria fainali za Afrika kwa U-17.