Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kashfa ubakaji: Polisi Marekani yajitosa kumchunguza Ronaldo

Muktasari:

Ronaldo kwa sasa ni baba wa watoto wanne kati yao watatu mama zao hawajulikana kutokana na usiri mkubwa uliofanywa na nyota huyo.

Las Vegas, Marekani. Mambo yaanza kumuharibikia mshambuliaji mahiri wa Juventus, Cristiano Ronaldo baada ya Polisi mjini Las Vegas, kukabidhiwa jalada na Mahakama ili kufanyia upepelezi tuhuma za nyota huyo kumbaka Kathryn Mayorga.

Kashfa hii mpya ya ubakaji iliyoibuliwa inaonekana kama mpango ulioandaliwa  kuyavuruga mafanikio ya Ronaldo ndani na nje ya uwanja kwa sababu inamuhusisha Kathryn Mayorga mwananmke kutoka nchini Marekani, ambako kesi za aina hiyo hubebwa na wanasiasa wa nchi hiyo kutaka umaarufu wa kisiasa kwa kujitia watetezi wa usawa na wapinga dhulma za kingono.

Taarifa hiyo ya Polisi imekuja siku moja baada ya mwanamke huyo kujitokeza hadharani na kudai kuwa alibakwa na Ronaldo mwaka 2009 walipokutana hotelini mjini Las Vegas, Marekani na kuthibitisha hilo ameweka mitandaoni picha alizopiga na mwanasoka huyo.

Kathryn mwenye miaka 34 amefichua madai hayo baada ya mwanasheria wake kufungua kesi Mahakamani akisema tukio hilo la ubakaji lilitokea bafuni kwenye hoteli ya Palms and Casino mjini Las Vegas, Juni 13, 2009.

Baada ya taarifa hizo kutolewa jana Ronaldo alijitokeza kukanusha akimshutumu mwanamke huyo kutaka kujipatia umaarufu kupitia jina lake, huku pia mwanasheria wake Christian Schertz, akisema wanajiandaa kulishitakia gazeti la Der Spiegel la Ujerumani ambalo ndilo lililoibua kashfa hiyo kwa mara ya kwanza, akisema linatumika kumchafua mwanasoka huyo.

Imearifiwa kuwa Mwanasheria wa Kathryn amefungua kesi kwenye Mahakama ya Wilaya ya Clark County tangu Ijumaa na katika maelezo yake anadai kuwa alibakwa mara kadhaa kitendo kikianzia bafuni na baadaye chumbani ambako walikuwa wawili tu.

Tofauti na maelezo yake ya awali aliposema kuwa alikaa kimya kwa sababu ya kutakiwa kuficha siri na kuahidiwa fedha na Ronaldo, katika maelezo aliyoyawasilisha Mahakamani na jalada kukabidhiwa Polisi kwa uchunguzi mwanamke huyo anadai wakati akibakwa alikuwa mwalimu wa wanamitindo, alisema alikaa kimya kwa muda mrefu kwa kuhofia aibu.

Alisema kuwa ameamua kuanika kila kitu baada ya kuona wito ukizidi kuwataka wanawake na watoto waliopitia mateso na manyanyaso ya kijinsia kujitokeza na kueleza hadharani ili waweze kusaidiwa kupata haki zao kisheria na kukomesha vitendo hivyo.