Hatma ya AS Roma na Smalling kujulikana leo

Friday October 02 2020
roma pic

ROMA inataka kuwasilisha ofa ya mwishoi ya Pauni 10 milioni ambayo itakuwa na ongezeko la Pauni 2 milioni kwenda Manchester United ili kuipata saini ya beki wa kati wa miamba hiyo ambaye msimu uliopita aliwatumikia kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Roma inataka kukamilisha dili hilo kabla ya siku ya leo Ijumaa kumalizika na ikishindikana itajaribu kutafuta mchezaji mwingine, ingawa Chris Smalling ndio chaguo la kwanza kwa sababu alionesha kiwango kikubwa msimu uliopita.

Man United inataka kumuuza Smalling kwa sababu haonekani kuwa kwenye mipango ya kocha, Ole Gunnar Solskjaer ambaye anataka kutengeneza timu  kupitia vijana.

Mbali na Roma na Inter Milan pia inaimezea mate saini ya mchezaji huyo alicheza mechi 30 za Seria A, msimu uliopita, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2022 thamani yake katika soko la usajili ni Euro 20 milioni na tayari ameanza kutafuta mlango wa kutoka.

Advertisement