Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msauzi ashikilia hatma ya Aziz KI Wydad

Muktasari:

  • Wydad ilicheza mechi tatu za michuano hiyo na kuondolewa hatua ya makundi bila ushindi ikianza na kichapo cha mabao 2-0 kutoka Man City ambapo Aziz KI alicheza kwa dakika saba, Juventus iliwachapa 4-1 Aziz KI akicheza dakika nne na ililala 2-1 dhidi ya Al Ain huku Aziz KI akiwa hakucheza kabisa mchezo huo wa mwisho.

BAADA ya kucheza dakika 11 kwenye mechi mbili za Kombe la Dunia la Klabu dhidi ya Manchester City na Juventus, kiungo mshambuliaji wa Wydad, Stephane Aziz KI huenda asiwe sehemu ya kikosi hicho msimu ujao huku ikielezwa ili abaki kuna ishu anaisikilizia.


Wydad ilicheza mechi tatu za michuano hiyo na kuondolewa hatua ya makundi bila ushindi ikianza na kichapo cha mabao 2-0 kutoka Man City ambapo Aziz KI alicheza kwa dakika saba, Juventus iliwachapa 4-1 Aziz KI akicheza dakika nne na ililala 2-1 dhidi ya Al Ain huku Aziz KI akiwa hakucheza kabisa mchezo huo wa mwisho.


Mchango wake ndani ya klabu hiyo bado haujaonekana kwa kiwango kilichotarajiwa huku kwenye michuano ya Kombe la Dunia la Klabu akitanguliwa na Thembinkosi Lorch na Nordin Amrabat ambao wanacheza nafasi moja uwanjani.

Lorch ambaye alicheza mechi zote tatu za Kombe la Dunia la Klabu akifunga bao moja, ndiye anayetajwa kushikilia hatma ya Aziz KI kwani Msauzi huyo anacheza hapo kwa mkopo akitokea Mamelodi Sundowns. Mkataba huo wa mkopo unamalizika Julai 31, 2025 huku kukiwa na ripoti kwamba Wydad imeridhishwa na uwezo wake, hivyo inatak kumsajili moja kwa moja.

Kwa mujibu wa jarida la Kiarabu la Al-Botola, Aziz KI anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wa kigeni wanaoweza kuachwa na klabu hiyo kabla ya kuanza kwa msimu mpya. 

Hii ni kutokana na shinikizo la kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni hadi watano ili kutokukiuka kanuni za Ligi Kuu ya Morocco (Botola Pro 1), wakati sasa Wydad wana jumla ya wachezaji 11 wa kigeni, hivyo kocha Mohamed Benhachem ametakiwa kuwasilisha majina ya wachezaji wa kupunguza ili wabaki watano.

Ikiwa Wydad watakamilisha usajili wa Lorch kama inavyodaiwa, basi nafasi ya Aziz KI itazidi kuwa finyu, hali inayoweza kumfanya aondoke labuni hapo mapema kuliko ilivyotarajiwa.

“Usajili wa Aziz KI una vificho vingi hadi sasa ukiniuliza alisaini mkataba wa muda gani siwezi kukupa jibu kwani haijajulikana kutokana na Wydad kushindwa kuweka wazi tofauti na Mwalimu (Selemani) ilivyokuwa, lakini ninachofahamu ni kwamba kocha hajaridhishwa na uwezo wa kiungo huyo anaweza akaondoshwa kikosini,” kilisema chanzo cha taarifa hiyo.

“Wakati baadhi ya vyanzo vikizungumza nyota huyo alisajiliwa kwa mkopo akitokea Yanga kukiwa na kipengele cha kumnunua na kuna vyombo vingine vinaripoti alisaini mkataba wa miaka mitatu, hivyo hii ni shida.” 

Wakati ikielezwa hivyo, kwa mujibu wa Transfermarkt - tovuti inayojihusisha na soka ikiwemo usajili wa wachezaji, Aziz KI alisaini mkataba wa miaka miwili Wydad unaomalizika Juni 2027.

Kuhusu suala la Mtanzania Mwalimu, chanzo kilidai huenda akarudishwa timu ya vijana moja kwa moja kwa ajili ya kuendelea kukuza uwezo tofauti na awali ilivyokuwa ambapo alikuwa anapata nafasi ya kucheza timu ya wakubwa.

Awali, ilielezwa Aziz KI aliyeitumikia Yanga kwa misimu mitatu tangu Julai 2022 akitokea Asec Mimosas ya Ivory Coast ameuzwa Wydad kwa Sh2 bilioni.

Aziz KI alitambulishwa na Wydad Mei 24, 2025 sambamba na nyota wengine wawili wapya waliojiunga kujiandaa na michuano ya Kombe la Dunia la Klabu inayoendelea nchini Marekani.

Wachezaji wa kigeni waliopo Wydad ni mabeki wa kati Guilherme Ferreira (Brazil) na Bart Meijers (Uholanzi), kiungo mkabaji Mickal Malsa (Ufaransa), viungo washambuliaji Arthur Wenderroscky (Brazil), Pedrinho (Brazil), Stephane Aziz Ki (Burkina Faso) na Thembinkosi Lorch (Afrika Kusini).

Wengine ni washambuliaji Omar Al-Somah (Syria), Samuel Obeng (Ghana), Seleman Mwalimu (Tanzania) na Cassius Mailula (Afrika Kusini) anayecheza kwa mkopo akitokea Toronto FC ambapo mkataba wake huo unatarajiwa kumalizika Agosti 1, 2025.

WASIKIE YANGA
Wakati sintofahamu ikiwa kubwa juu ya hatma ya Aziz KI ndani ya Wydad, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema kiungo huyo alipelekwa huko kwa mkopo. 

“Mkataba ambao Aziz KI aliusaini na Wydad wakati tunamuuza ni wenye vipengele viwili - miezi mitatu ya kwanza wanamuangalia, wakijiridhisha na kiwango watamuongeza kwa miaka miwili,” alisema Kamwe.

Alisema kwa mujibu wa makubaliano, Julai 10, mwaka huu Wydad wanatakiwa kuwasiliana na Yanga juu ya ishu ya Aziz KI kuendelea kusalia huko.

“Aziz Ki bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Yanga. Endapo watashindwana naye basi atarejea nchini na atakuwepo kwenye mchezo wetu wa kwanza wa kufungua msimu ujao kwenye Ngao ya Jamii.”