Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anuary awageukia Bocco, Kagere

MSHAMBULIAJI matata wa Dodoma Jiji, Anuary Jabir hatimaye sasa amewageukia wapinzani wa kiatu cha mfungaji bora wa msimu, kufuatia kasi yake kali ya upachikaji mabao aliyokuja nayo.

Mabao saba aliyofunga kwenye mechi nne alizocheza kuanzia raundi ya pili ikiwa zote alifunga katika mechi dhidi ya JKT Tanzania, Coastal Union, Polisi Tanzania na Kipigwe FC na kumfanya afikishe idadi hiyo ndani ya mechi nne.

Ukiachana na mabao matatu aliyonayo kwenye Kombe la Shirikisho, Anuary hivi sasa ana mabao manne huku akiweka lengo la kufunga zaidi mabao kwenye mechi zijazo hadi awafikie wanaoongoza kwa ufungaji Ligi Kuu Bara.

Kabla ya mechi za jana Jumatano, John Bocco na Meddie Kagere ndio walikuwa wamefungana kwa mabao tisa, ambapo nyota hao wanaichezea timu ya Simba wakati Prince Dube wa Azam, Meshack Abrahamwa wa Gwambina na Adam Adam wa JKT Tanzania walifunga mabao saba kila mmoja.

Akizungumzia hilo, Anuary alisema amepanga kila mchezo ujao wa ligi atumie kila nafasi atakayoipata ili kufunga zaidi mabao kwani anatarajia awe mpinzani wa ufungaji bora dhidi ya kina Bocco na Kagere wanaoongoza.

‘‘Kila bao ninalofunga namshukuru Mungu na timu yangu kwa ujumla, ushirikiano wa pamoja ndio unaonifanya nipate nafasi ya kufunga mabao hayo, hivyo nimepanga kila nafasi nitakayopata nifunge bao ili kutimiza lengo la kuwa mfungaji bora msimu huu,’’ alisema.

Kwa misimu miwili wa Ligi Kuu Bara, Kagere ametwaa kiatu cha mfungaji bora.


IMEANDIKWA NA MATEREKA JALILU