Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wikiendi hii hatucheki na yeyote

Hatucheki Pict

Muktasari:

  • Hakuna asiyejua kile kinachotokea uwanjani wakati timu hizo nne zinapovaana, lakini kule England kuna kazi kwelikweli kuanzia leo Jumamosi hadi kesho Jumapili wakati Tottenham Hotspur na Liverpool zitakapohitimisha mechi za Ligi Kuu nchini humo maarufu kama EPL.

HII ni wikiendi ya kibabe. Yaani kuanzia hapa nyumbani Tanzania hadi kule Ulaya hakuna anayecheka na mtu. Wanajua wakicheka na yeyote itakula kwao. Ndio katika Ligi Kuu Bara wikiendi hii kuna mechi mbili za kibabe, leo kule mjini Bukoba, Simba itakuwa kwenye Uwanja wa Kaitaba kumalizana na wenyeji wao, Kagera Sugar katika mechi ya Ligi Kuu Bara, kisha kesho Jumapili itakuwa ni zamu ya Yanga kuwa wenyeji wa TZ Prisons.

Hakuna asiyejua kile kinachotokea uwanjani wakati timu hizo nne zinapovaana, lakini kule England kuna kazi kwelikweli kuanzia leo Jumamosi hadi kesho Jumapili wakati Tottenham Hotspur na Liverpool zitakapohitimisha mechi za Ligi Kuu nchini humo maarufu kama EPL.

Ujerumani katika Bundesliga kuna mechi za maana baada ya jana usiku Beyern Munich kumalizana na RB Leipzig, huku Hispania kuna mechi ya kibabe kwa leo wakati Barcelona itakuwa wenyeji wa Atletico Madrid, wakati Ufaransa na kwingine nako hakuna atakayechezeka na mtu, ni kukunja sura tu kusaka pointi tatu za maana uwanjani.


HATU 07

KAGERA v SIMBA

Zile hesabu za kocha wa Simba, Fadlu David za kukusanya pointi 40 za duru la kwanza za Ligi Kuu ili imalize kileleni mwa msimamo zinaendelea leo ugenini mjini Bukoba dhidi ya Kagera Sugar katika mechi itakayopigwa kuanzia saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Kaitaba.

Simba inayoshika nafasi ya pili katika msimamo ikiwa na pointi 31, mbili  pungufu ya ilizonazo Azam inayoongoza kwa alama 33, inakabiliana na Kagera iliyo kwenye hali mbaya tangu kuanza kwa msimu huu.

Kagera iliyoshuka uwanjani mara 14, leo inahitimisha mechi za duru la kwanza za ligi hiyo, ikihitaji ushindi ili ijiondoe katika mstari mwekundu wa hatari ya kushuka daraja.

HATU 06

Katika mechi 14 ilizocheza, wenyeji wana pointi 11, huku wakiwa hawana matokeo mazuri tangu kuanza kwa ligi hali iliyowafanya kubadilisha benchi la ufundi kwa kumuondoa kocha mkuu, Paul Nkata, nafasi yake ikachukuliwa na Melis Medo aliyefichua kwamba dirisha hili dogo la usajili anataka mashine nne za kujiimarisha zaidi hasa eneo la ulinzi.

Timu hiyo iliyoshinda mechi mbili pekee kati ya 14 huku ikipoteza saba na sare tano, imeruhusu mabao 14 ikionekana kuwa na tatizo eneo la ulinzi, lakini katika ushambuliaji pia hawapo vizuri wakifunga mabao nane tu.

Hesabu za Kagera ni kushinda mchezo huu ili kufikisha pointi 14 ambazo zinawatoa kwenye mstari mwekundu lakini hawatakuwa salama zaidi kitu ambacho kitawafanya mzunguko wa pili kujirekebisha ili kuepuka kushuka daraja.

Kocha Medo alisema: “Tunahitaji kupata matokeo mazuri, kisha tukiingia mzunguko wa pili tupige hesabu nyingine vizuri kuhakikisha tunakuwa salama hadi mwisho wa msimu.”

Wakati hesabu za Kagera zikiwa hivyo, Simba iliyotoka kuifunga KenGold mabao 2-0, ina mechi tatu zenye pointi tisa kukamilisha mzunguko wa kwanza kwani hadi sasa imeshuka dimbani mara 12.

HATU 05

Katika mechi hizo tatu, Fadlu anahitaji kushinda zote ili kumaliza mzunguko wa kwanza na pointi 40 zitakazowafanya kukaa kileleni.

Ukiachana na hilo, mchezo wa leo kama Simba itashinda, basi itarejea kileleni kwa kufikisha pointi 34 na kuishusha Azam kwa tofauti ya pointi moja.

“Tuna mechi mfululizo kumalizika mzunguko wa kwanza, tunahitaji kufanya vizuri licha ya kwamba tunaamini haitakuwa rahisi,” alisema Fadlu akizungumzia mechi hizo zinazofuata dhidi ya Kagera Sugar (ugenini), JKT Tanzania (nyumbani) na Singida Black Stars (ugenini).


MPANZU NDANI

Usajili mpya, Elie Mpanzu huenda leo akacheza mechi yake ya kwanza ya kimashindano ndani ya Simba baada ya taarifa kubainisha kwamba masuala yake yamekamilika.

Mpanzu aliyetambulishwa Simba Septemba 30 mwaka huu akitokea AS Vita, hajacheza mechi yoyote ya kimashindano tangu atue huku ikitarajiwa angeweza kucheza dhidi ya KenGold Jumatano wiki hii baada ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa Desemba 15, 2024 lakini haikuwa hivyo baada ya kutokamilika kwa baadhi ya vibali.

HATU 04

“Mpanzu ana asilimia 99.99 za kucheza kwani masuala yake yote ya usajili yamekamilika,” alisema Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally huku nyota huyo akisafiri na timu kwenda Kagera kwa ajili ya mchezo huo. Hata hivyo Simba ni lazima imteme mchezaji mmoja wa kimataifa ili Mpanzu acheze kwa sababu Sima tayari ina wachezaji 12 wa kigeni kama kanuni inavyosema.

   

KAGERA WABISHI

Ubishi wa Kagera mbele ya Simba upo wazi hasa wanapokuwa uwanja wao wa nyumbani kwani rekodi zinaonyesha kwamba katika misimu mitatu mfululizo 2021-2022, 2022-2023 na 2023-2024, haijapoteza kwao dhidi ya Simba.

Mara ya mwisho Kagera kufungwa na Simba nyumbani kwao ilikuwa msimu wa 2020-2021 ilipochapwa 2-0. Baada ya hapo, imeshinda moja na sare mbili.

HATU 03

Licha ya ugumu huo walionao Kagera, lakini takwimu zao kwa mechi sita za mwisho msimu huu zinawaweka kwenye mtihani mzito kwani wameshinda mechi moja tu, sare tatu na kupoteza mbili.

Simba katika mechi zao sita zilizopita za ligi msimu huu, imeshinda zote bila ya kuruhusu bao kitu kinachowafanya kuingia kwenye mchezo huu ikiwa na matumaini makubwa.


HATU 01

CAMARA YUPO IMARA

Lango la Simba kuna kipa Moussa Camara ameonekana kuwa imara zaidi kwani ndiye kipa anayeongoza kwa clean sheet nyingi akifikisha 10 akicheza mechi 12, akiruhusu mabao matatu pekee, mawili dhidi ya Coastal Union katika sare ya 2-2 na moja mbele ya Yanga walipofungwa 1-0.

Kwa upande wa Kagera Sugar, safu yao ya ulinzi haipo vizuri kwani katika mechi 14 imeruhusu mabao manne, kipa wao namba moja, Ramadhan Chalamanda akiwa na clean sheet tatu.


HATU 02

WAKALI

Peter Lwasa ndiye nyota anayeonekana kuibeba zaidi Kagera Sugar, kwani katika mabao manane yaliyofungwa na timu hiyo yeye amepachika manne ikiwa ni nusu ya kikosi kizima.

Kwa upande wa Simba, Jean Charles Ahoua ndiye amehusika kwenye mabao mengi kikosini hapo akifunga matano na kuasisti manne, huku Leonel Ateba akifunga matano na asisti moja.


HIYO KESHO SASA

Mara baada ya Simba kumalizana na Kagera, kesho Jumapili itakuwa ni zamu ya watetezi wa ligi hiyo, Yanga kuwa wenyeji wa maafande wa Tanzania Prisons ambao nao hawana msimu mzuri hadi sasa kwani wanapumulia mashine kutokana na kuanza msimu kichovu.

Ikielezwa imewaweka kando makocha Mbwana Makatta na msaidizi wake Renatus Shija, hivyo kesho itaivaaa Yanga ikiwa na sura mpya za kukomaa na watetezi hao waliotoka kupata ushindi wa 3-2 dhidi ya maafande wengine wa Mashujaa kwenye Uwanja wa KMC Complex, utakaotumika kwa mchezo wa leo pia.

Prisons ipo nafasi ya 15 katika msimamo ikikusanya pointi 11 kama ilizonazo Kagera Sugar, lakini zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa, maafande hao wakiwa ndio wenye mabao machache zaidi hadi sasa wakifunga sita tu katika mechi 14 walizocheza, wakiwa wanafanana kila kitu na Kagera isipokuwa kwenye mabao tu.

Kama ilivyo Kagera inayoumana na Simba mjini Bukoba, pia Prisons katika mechi 14 ilizocheza, imeshinda mbili tu, kutoka sare tano na kupoteza saba, huku ikifungwa mabao 13 na kufunga sita, wakati wenzao wamefunga manane na kufungwa 14 na zote zinapumulia mashine sambamba na waburuzia mkia, Ken Gold yenye pointi tisa tu katika mechi 15 ilizocheza hadi sasa, ikishinda mchezo mmoja na kupata sare tatu ikipoteza mechi 11.

Yanga iliyopo nafasi ya tatu katika msimamo ikiwa imekusanya pointi 30 baada ya mechi 12, itakuwa na kiu ya kuendelea ilipoishia tangu iwe chini ya kocha Sead Ramovic aliyeiongoza katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara na zote imeshinda tangu alipompokea Miguel Gamondi aliyetimuliwa baada ya timu hiyo kupoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Azam FC na Tabora United.

Ikiendelea kumtegemea Prince Dube aliyeanza kuwa mtamu kama mcharo baada ya juzi kufunga hat trick ya kwanza katika msimu huu wa ligi, wakati wakiizamisha Mashujaa, Yanga itakuwa na kila sababu ya kuendeleza rekodi tamu iliyonayo mbele ya maafande hao wa Prisons.

Mbali na Dube, Yanga itawategemea Pacome Zouzoua, Clement Mzize na wakali wengine, japo itawakosa nyota kadhaa akiwamo kipa Diarra Djigui ambaye pengo lake lilionekana juzi wakati Abubakar Khomeiny aliyeanzishwa langoni alipotunguliwa mabao mawili na David Ulomi na Idriss Stambuli kwa mashuti ya mbali na kumtibulia.

Kabla ya mechi hiyo na Mashujaa, Khomeiny alikuwa amecheza mechi tatu mfululizo, zikiwamo mbili za Ligi Kuu Bara na moja ya Ligi ya Mabingwa Afrika, bila kuruhusu bao na pengine kocha Ramovic kama amemaindi matokeo ya juzi, anaweza kumuanzisha Abutwalib Mshery.