Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasomi: Ulingoni imo, shule imo

Wasomi Pict
Wasomi Pict

Muktasari:

  • Kwenye soka na michezo mingi imetawaliwa na vipaji. Kutokana na maisha magumu waliopitiua wachezaji wengi wakiwa vijana wadogo, waliona vipaji ndivyo vitawaokoa na kuamua kuonyesha uwezo wao. LAeo hii wanakula matunda ya vipaji vyao.

MICHEZO ni moja ya kazi zinazoingiza pesa nyingi sana kwa sasa. Hata wasomi nao wamehamia kwenye michezo.

Miaka ya nyuma ilikuwa ni ngumu watu walioko shule au waliosoma kujihusisha na michezo. Wengi walifanya kazi kutokana na taaluma zao hata kama walikuwa na vipaji.

Kwenye soka na michezo mingi imetawaliwa na vipaji. Kutokana na maisha magumu waliopitiua wachezaji wengi wakiwa vijana wadogo, waliona vipaji ndivyo vitawaokoa na kuamua kuonyesha uwezo wao. LAeo hii wanakula matunda ya vipaji vyao.

 Lionel Messi, Cristian Ronaldo, Sadio Mane na Samuel Etoo ni mfano tu wa waliosota na maisha wakiwa waddogo na kuibuka kuwa matajiri kupitia michezo hasa soka.

Mkongwe Mike Tyson, Flody Mayweather,  Manny Pacquiao na hata Muhammad Ali wote wamepita pagumu kabla ya kuibukia kwenye ndondi na sasa ni matajiri.

Hata hivyo, wapo ambao wamesoma na kushiriki michezo na kote wametoboa.

Achana na mataifa makubwa ambako ni rahisi kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja, shule na michezo, kama ilivyo kwa nyota wa Barcelona, Yamile Jamal, Juan Mata na wegine, wamesoma na soka wanapiga.

Kwenye masumbwi nako hasa Tanzania, kuna mabondia ambao mbali na kupambana ulingoni lakini shule nako imo.

Ngumi za kulipwa, mabondia wengi wamefanikiwa kutokana na vipaji na juhudi zao pasipo kuwa kuwa hata na diploma ya kitu chochote katika vichwa vyao.

Hata hivyo, wasomi ni wa kuwatafuta kwa tochi kwa kuwa wengi wao wamebebwa na vipaji vyao kama Francis Cheka ‘SMG’, Maneno Oswald ‘Mtambo wa Gongo’ Rashid Matumla ‘Snak Boy’, Karim Mandonga.

Wengine ni Ibrahim Class, Dullah Mbabe, Twaha Kiduku, Hassan Mwakinyo.

 Mwanaspoti limefanya uchunguzi juu ya mabondia wa Tanzania ambao wamefika angalau kidato cha sita au vyuoni katika fani mbalimbali licha ya sasa lipo kundi la ambao wamefika hadi kidato cha nne.


Jamal Kunoga

Mmoja kati ya mabondia wanaokuja kwa kasi katika ngumi za kulipwa akiwa chini ya Twaha Kiduku na rekodi ya kucheza jumla ya mapambano 13, ameshinda tisa kati ya hayo mawili ni kwa Knockout, amepigwa mara mbili kati ya hayo moja ni Knockout huku akiwa ametoka sare mara mbili.

Bondia huyo anayechezea uzani wa Super Bantam, mwaka 2016 alimaliza elimu ya Sekondari katika shule ya Goba kisha akajiunga kidato tano na sita kwenye shule Kigurunyembe mkoani Morogoro aliyomaliza mwaka 2019.

Kunoga alitumia muda wake wa ziada kuendelea  na harakati za ngumi huku akishiriki baadhi ya mapambano na kufanya vizuri.

Bondia huyo anaeleza, kidato cha tano na sita alisomea mchupuo wa HKL ambao unajumuisha,  Historia, Kiswahili na Language na mwenyewe ana sisitiza kwa mchepuo huo alipaswa kusomea ualimu au sheria lakini havikuwa chaguo lake badala yake akaweka nguvu zaidi kwenye mchezo wa ngumi.


Cosmas Cheka

Kaka yake ni Francis Cheka ambaye ni bingwa wa zamani wa Dunia katika mkanda wa WBF, Cosmas ndiye kijana aliyefuata  nyayo za kaka yake baada ya kumaliza masomo yake ya uhasibu katika ngazi ya diploma kwenye Chuo cha Uhasibu TIA baada ya kumaliza kidato cha nne.

Cheka mwenye rekodi ya jumla ya mapambano 58 akiwa ameshinda 29 kati ya hayo saba ni kwa Knockout na amepigwa mara 21kati ya hizo tisa ni Knockout huku akitoka sare mara nane.

Cheka anaeleza kuwa katika maisha yake elimu aliipa nafasi kubwa na kusababisha  ashindwe kutimiza ndoto zake za kuwa mchezaji mkubwa wa soka kama ilivyokuwa kwa rafiki zake aliosoma nao Kinondoni, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Jonas Mkude ambao wameishia kidato cha nne tu.


Joh Babai

Katika mchezo wa ngumi anatambulika kwa majina ya Joh Babai lakini majina yake halisi ambayo amapewa na wazazi wake ni Ramadhan Ramadhan.

Bondia huyo kwa sasa yupo chini ya manejimenti ya Mafia Boxing Promotion akiwa na rekodi ya kucheza jumla ya mapambano matano tu katika ngumi za kulipwa.

Babai ameshinda mapambano manne kati ya hayo mawili ni kwa Knockout huku akitoka sare pambano moja katika uzani wa middle.

Bondia huyo anaeleza safari yake ya elimu ilianzia katika shule ya sekondari ya Mbweni Teta ambayo alisoma hadi kidato cha nne.

Lakini bondia huyo hakutaka kuishia hapo katika upande wa shule kwani alijiunga na Chuo cha Bandari ambacho kipo chini ya Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA kusomea kozi ya Shipping and Port Operations Management ngazi ya cheti na baadaye diploma.


Kisua Mwabaka

Licha ya kutokuwa na rekodi ya kuvutia katika mchezo wa ngumi za kulipwa nchini kutokana na  kuchapika katika mapambano mawili aliyocheza hadi sasa lakini ndiyo bondia mwenye rekodi kubwa elimu ya juu hadi sasa.

Kisua anayechezea uzani wa Walter, kabla ya ngumi za kulipwa alianzia kucheza mchezo wa karate lakini baadaye aliingia kwenye ngumi akifundishwa na walimu mbalimbali nchini.

Bondia huyo anaeleza kwenye ngumi amepita chini ya mikono ya Hassan Mzonge ambaye ni kocha wa Seleman Kidunda, George Bonabucha na Ismail Galiatano lakini pia Hamisi Mwakinyo pamoja na Ally Bakari ‘Champion’ katika vipindi tofauti wameweza kumpa madini ya kutosha kwenye mchezo wa ngumi.

Lakini katika upande wa shule, Kisua amepata elimu yake nchini Kenya kuanzia msingi, sekondari hadi chuo, akisoma katika chuo kikuu cha Umma na alisomea Bachelor Degree in Business Administration.

Bondia huyo hakuishia kwani aliendelea kubaki darasani  kasoma tena Certified Public Accountant ‘Mhasibu wa Umma aliyeidhinishwa’ daraja la kwanza na lipi lakini akaongeza cha cheti ya ualimu.


Sarafina Bela

Huenda Sarafina Bela akawa ndiyo bondia pekee mwanamke katika ngumi za kulipwa mwenye hatua kubwa ya kuelimu kutokana na kufika kidato cha sita.

Bondia huyo mwenye rekodi ya kucheza mapambano 14 akiwa ameshinda sita kati ya hayo manne ni kwa Knockout, amepigwa mara saba kati ya hizo tatu ni kwa Knockout na ametoka sare mara moja.

Bela anatajwa kuwa bondia pekee ambaye amefikia kiwango hicho cha elimu licha ya mwenyewe mara nyingi kugomea kuongelea suala hilo kwa upande wake.


Allen Kabungo

Ni mmoja kati ya mabondia wataratibu na wenye nidhamu kubwa ndani na nje ya uringo akiwa na rekodi ya kucheza mapambano 11 akiwa ameshinda  tisa kati ya hayo saba ni Knockout na amepoteza mapambano mawili tu.

Kabungo ni mmoja kati ya mabondia ambao wamefikia elimu ya kidato cha sita aliyoipata mkoani Mbeya kabla ya kujikita kwenye mchezo wa ngumi kutokana na changamoto mbalimbali alizokutana nazo.