Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanawake michezoni... Mabadiliko na staili za maisha

WANAWAKE Pict

Muktasari:

  • Mabadiliko haya yanaendana na mabadiliko makubwa katika jamii na inatambulika ni umuhimu wa afya, ustawi na uwakilishi wa kijinsia katika sekta mbalimbali, ikiwamo michezo.

KATIKA miaka ya hivi karibuni, kumekuwapo na mabadiliko makubwa katika mitindo ya maisha ya wanawake Tanzania. Ni dhahiri wanawake wanapata nafasi zaidi ya kushiriki katika michezo na shughuli za kimwili kama vile kwenda kwenye viwanja vya mazoezi kama gym, jogging na hata kushiriki katika mashindano ya soka.

Mabadiliko haya yanaendana na mabadiliko makubwa katika jamii na inatambulika ni umuhimu wa afya, ustawi na uwakilishi wa kijinsia katika sekta mbalimbali, ikiwamo michezo.

Hii ni tofauti na miaka ya nyuma, michezo karibu yote ilionekana ni ya wanaume tu, lakini kwa miaka ya hivi karibuni kutokana na mabadiliko na staili za maisha zimewalazimisha wanawake nao kujitosa michezoni kuanzia katika soka, ngumi ukiachana na jogging au kujifua gym kila uchao.

Hata hivyo, ingawa inaelezwa kwa miaka ya karibuni wanawake wengi wanajihusisha na michezo, lakini kuna baadhi wanatumia wanamichezo kujinufaisha na kujiingizia kipato kwa namna wanazozijua, ikiwamo kutoka nao kimapenzi.

Katika makala haya, tutachunguza jinsi wanawake wanavyojitokeza kwa wingi zaidi katika michezo, hasa soka na wanavyoitumia michezo.

WANA 01

INAVYOWANUFAISHA KIAFYA

Wanawake wengi Tanzania kwa sasa wanajivunia kushiriki katika michezo kwa sababu za afya, ustawi wa mwili na kujenga ujasiri.

Wapo wanaokwenda gym, jogging na kujishughulisha na michezo mingine, imekuwa ni sehemu muhimu ya maisha ya wanawake wengi. Wengi wao wanajivunia kutumia mazoezi kama njia ya kupambana na changamoto za kila siku za kijamii na kimwili.

"Nimeanza kwenda gym kila baada ya siku tatu kwa miezi sita sasa. Ni jambo ambalo limebadilisha maisha yangu kwa kiasi kikubwa. Nimejifunza kuwa siyo tu tunajenga mwili, bali pia tunajenga akili," anasema Amina Bilal.

Amina ambaye ni mkazi wa Tabata, Segerea anasema mazoezi ya mara kwa mara yamemsaidia kuboresha utendaji wake kazini na kujiamini zaidi katika michezo.

Wanawake wengi sasa wanakwenda gym kwa lengo la kuboresha afya zao, kupunguza uzito na kuongeza nguvu za mwili. Taaluma za mazoezi kama vile yoga, pilates, crossfit na aerobics zimekuwa maarufu miongoni mwa wanawake wengi. Hii ni ishara kuna uelewa mkubwa wa umuhimu wa afya ya mwili na wanawake wanajitahidi kudumisha afya bora, kuboresha ustawi wa akili na mwili na kujiongezea ujasiri.

Katika mitindo ya maisha ya kisasa, wanawake wanataka kuwa na maisha yenye usawa, ikiwamo kutunza mwili wao.

"Mimi najivunia kuwa na nguvu za kimwili na kiakili. Hii inanipa furaha na hali ya amani," anasema Tina, ambaye ni mama wa watoto wawili na mpenzi wa yoga na jogging.

Tina amepata muda wa kufanya mazoezi licha ya majukumu ya familia na kazi na anasisitiza wanawake wanapaswa kujua "kujilinda kimwili ni kujiwekea akiba ya afya kwa maisha ya baadaye."


WANA 02
WANA 02

MABADILIKO YA MTINDO WA MAISHA

Tofauti na zamani, wanawake walikuwa wanachukuliwa kama sehemu ya jamii inayoshiriki michezo kwa kiasi kidogo.

Kwa sasa, wanawake wanatambua michezo ni sehemu muhimu ya maisha yao na wanajivunia kuwa sehemu ya mabadiliko haya. Wanawake wengi, hasa vijana, wanapata hamasa kutoka kwa viongozi wa kisiasa, wanamichezo maarufu na jamii kwa jumla. Sasa kuna hamasa kubwa ya kuwaona wanawake wanashiriki katika michezo ya kimataifa na kitaifa, na wengi wao wanachukuliwa kama mfano wa kuigwa katika jamii.

"Nimekuwa nikijivunia kuwa sehemu ya mabadiliko haya. Nilikuwa na aibu kuingia gym awali kwa sababu ya mitazamo ya jamii, lakini sasa nafanya hivyo kwa furaha," anasema Zawadi.

Zawadi anasema kitendo cha kujiamini na kushiriki kwenye michezo kimebadilisha mtazamo wake kuhusu wanawake na michezo, hasa baada ya kuona wanawake wakiwa kwenye soka kwa ufanisi mkubwa.

Kwa mfano, soka imekuwa ni moja ya michezo inayovutia wanawake wengi. Wakati fulani, soka lilichukuliwa ni mchezo wa kiume, lakini sasa kuna mabadiliko makubwa. Timu za wanawake zinazoshiriki katika Ligi Kuu ya Wanawake, kama vile Yanga Princess na Simba Queens, zimekuwa zikifanya vizuri na kuonyesha uwezo wa juu. Wanawake hawa wanadhihirisha michezo siyo tu kwa wanaume, bali ni kwa wote na hii inaonyesha jinsi jamii inavyokubaliana na kubadili mitindo ya maisha ya wanawake.

Kocha Matty Msetti 'Mattydiola' ni mwanamke mwingine ambaye kutokana na michezo amepiga hatua kimaisha na anajivunia michezo kwani licha ya changamoto alizopitia hakukata tamaa.

Moja ya changamoto akiwa kocha ni kusaka timu ingawa kwa sasa amejiata akiwa anafundisha soka katika akademi moja nchini Dubai.

"Katika Akademia ninayofundisha ya Alliance Football Club nimesaini miaka miwili nipo spesho kwa watoto wa kike kuanzia wa umri wa miaka minne hadi 21."

Anasema hatua alizopiga kimaisha ni kumiliki mashamba, kuwekeza kwenye mfuko wa serikali (UTT), kumiliki Magari, Crown Athlet (Sunroof) ikiwa Tanzania na MG alilonunua Dubai na ndilo gari analoitumia kwa sasa.

"Malengo yangu nikurudi Tanzania, nataka kufungua kituo cha michezo kitakachosaidia kukuza vipaji vya watoto, naamini Mungu ataweka wepesi InshaAllah."

WANA 03

MABADILIKO YA KITAMADUNI

Pamoja na maendeleo haya, mitindo ya maisha ya wanawake pia imebadilika. Wakati fulani, wanawake walikuwa wanajitahidi kudumisha picha ya 'kijinsia' iliyojaa uzuri wa kimwili na kujali familia, lakini sasa wanawake wanabadilisha mtindo wa maisha yao kwa kushiriki katika michezo ya ushindani.

Wanawake wa sasa wanajivunia kuwa na afya bora, nguvu za mwili na kuwa na ujasiri wa kufanya shughuli za kimwili ambazo zilikuwa zikichukuliwa kama 'za kiume' hapo awali.

Mabadiliko haya pia yanaonekana katika jamii na familia nyingi zinajivunia kuwa na wanawake wanaoshiriki kwa nguvu katika michezo. Hii inadhihirisha jinsi wanawake wanavyotambua na kuthamini mchango wao katika jamii kupitia michezo na inaonyesha familia nyingi zinatambua umuhimu wa kuwaunga mkono wanawake wao.

"Sasa ni kawaida kwa wanawake kushiriki katika michezo. Hii ni fursa ya kukuza afya na maisha bora kwa wote. Ninajivunia kuwa na uwezo wa kuonyesha uwezo wangu mbele ya wengine," anasema Fetty Densa.


WANA 04

MABADILIKO YA KITAMADUNI

Pamoja na maendeleo haya, mitindo ya maisha ya wanawake pia imebadilika. Wakati fulani, wanawake walikuwa wanajitahidi kudumisha picha ya 'kijinsia' iliyojaa uzuri wa kimwili na kujali familia, lakini sasa wanawake wanabadilisha mtindo wa maisha yao kwa kushiriki katika michezo ya ushindani.

Wanawake wa sasa wanajivunia kuwa na afya bora, nguvu za mwili na kuwa na ujasiri wa kufanya shughuli za kimwili ambazo zilikuwa zikichukuliwa kama 'za kiume' hapo awali.

Mabadiliko haya pia yanaonekana katika jamii na familia nyingi zinajivunia kuwa na wanawake wanaoshiriki kwa nguvu katika michezo. Hii inadhihirisha jinsi wanawake wanavyotambua na kuthamini mchango wao katika jamii kupitia michezo na inaonyesha familia nyingi zinatambua umuhimu wa kuwaunga mkono wanawake wao.

"Sasa ni kawaida kwa wanawake kushiriki katika michezo. Hii ni fursa ya kukuza afya na maisha bora kwa wote. Ninajivunia kuwa na uwezo wa kuonyesha uwezo wangu mbele ya wengine," anasema Fetty Densa.


UPANDE WA PILI

Wakati wanawake wengi wanajikita katika michezo kwa ajili ya afya na ustawi wao, wengine wanachukulia kama njia ya kujipatia kipato, lakini kuna kundi la wanawake ambao wamekuwa wakitumia mazingira haya kama sehemu ya kujirahisisha kwa wanaume.

Hii ni hali ambayo imekuwa ikijitokeza kwenye viwanja vya michezo na maeneo ya mazoezi (gym), ambapo baadhi ya wanawake wanashindwa kuweka mipaka kati ya kujenga afya, ushabiki na kujiingiza kwenye masuala ya kimapenzi.

Wadada wengi wanakubaliana kuwa hali hii ni kikwazo kwao na wanaona kama inachafua picha ya wanawake wanaoshiriki michezoni kwa malengo ya kujenga afya na uwezo wa kimwili. Agnes Mwita, ambaye ni mpenzi wa gym na mazoezi, anasema.

"Sidhani kama wanawake wengi wanastahili kuhusishwa na tabia kama hizi. Michezo ni fursa nzuri ya kuboresha afya, lakini watu fulani wanageuza kila kitu kuwa shaghala baghala, wanajifanya kutafuta uhusiano badala ya kujijenga kimwili. Hii inawachafua wengine, na hatushindi kuonekana kama tunajali michezo, bali kama tunakuja kwa ajili ya 'kuvutia' wanaume."

Happy Kakozi ambaye ni mpenzi wa jogging, anaongeza. 

"Mimi ni mtu wa mazoezi, lakini kuna baadhi ya wanawake wanapoingia kwenye gym, jogging, viwanjani na hata zile marathon ni wazi kuwa wanatafuta njia ya kujirahisisha kwa watoa mafunzo au wachezaji. Hii inakuwa vigumu kwa sisi ambao tunahitaji kufanya kazi kwa bidii na kujijenga au kushabikia mpira."

WANA 05

MASTA GYM WAFUNGUKA

Kwa upande mwingine, watoa mafunzo katika gym nao wanakubaliana na changamoto hii, huku wakieleza jinsi inavyowaathiri katika kazi zao. John Kulwa ni mtaalamu wa mazoezi ambaye anafundisha mazoezi ya nguvu Mabibo jijini Dar es Salaam, anasema.

"Kwa bahati mbaya, hii imekuwa changamoto kubwa. Tunapofundisha mazoezi, tunakutana na wanawake wengi ambao hawajali kuhusu mazoezi, bali wanatafuta nafasi za kuzungumza na watoa mafunzo au wateja wengine. Hii inafanya kazi yetu kuwa ngumu." 

Kwa upande wake, Miriam Kizito ambaye ni msaidizi wa John, anaongeza, "Mimi pia nimejikuta nikikumbana na changamoto hii. Kuna wanawake wanakuja kwa mazoezi lakini wamejawa na malengo mengine. Ni vigumu kuwaelekeza kwa umakini kwenye mazoezi kwa sababu wanakuwa wanavutiwa na watoa mafunzo au wachezaji wakiwa kwenye gym. Inachosha sana kuona mtu akichanganya mazoezi na mambo yasiyohusiana na afya."


MASTAA WACHANGANYWA

Kwa sasa, mastaa wa Ligi Kuu Bara wamekuwa wakijikuta katika hali ngumu, wamekuwa wakinasa kwenye mtego wa mahusiano huko viwanjani na mwanamke mmoja bila ya kujua, jambo ambalo limekuwa likilete migongano miongoni mwao, hasa baada ya kubaini kuwa wanashirikiana na mwanamke mmoja.

Hali hii imekuwa ikichafua mazingira ya michezo na kuleta mkanganyiko mkubwa, hususani kwa wachezaji wanaojitahidi kuweka umoja katika timu zao.

Kinadada ambao wanakwenda viwanjani kama mashabiki wakiwa na mapenzi ya kweli na timu zao, wanaheshimu nafasi zao na kujua wajibu wao. Lakini, kuna wanawake ambao hupendelea kuvizia, na mara nyingi wanajikita kwenye njia zisizo sahihi za kumvutia mchezaji au staa, kwa lengo la kujirahisisha na kujipatia manufaa binafsi.

Hii imekuwa ni changamoto kubwa kwa mastaa na wachezaji wa timu mbalimbali, ambapo wanaume wengi wamejikuta wakifanya maamuzi ya kihisia ambayo yameathiri uhusiano wao ndani ya timu.

Inaelezwa, licha ya kuwa wachezaji hawana uhusiano na wanawake hao, lakini wengine hujikuta wakiwasiliana nao kutokana na wanawake hao kutafuta namba zao.

Namba hizo inaelezwa huzinunua kutoka kwa watu wa karibu na wachezaji hao na ndipo hutumia kuwatega wachezaji ili kuwa nao kimapenzi.

Mmoja wa wanawake waliowahi kununua namba kwa ajili ya kuwasiliana na wachezaji anasema; "Kuna watu wapo karibu na wachezaji wanatuuzia hizo namba. Hasa wachezaji wa kigeni na ukibahatika kuwapata wanatoa pesa nyingi kwa sababu huwa hawazijui vizuri pesa za Tanzania."

Wengine inaelezwa wanavamia kwenye mitandao ya wachezaji na kuwatega kwa kuwatumia picha na wanajikuta wakiingia kwenye mtego na kutoka nao kimapenzi.

Wengine wanatumia fursa kama kulipiwa nauli na kuendeshewa maisha wawapo katika safari za kimichezo. Mfano ni timu zinaposafiri kucheza mikoani, wengi hukuta hawana nauli na wanategemea kutoka kwa wanaume na inaelezwa wengine wakifika mikoani hutafuta namna nyingine ya kupata pesa ikiwamo kutumia miili yao.

Mmoja wa viongozi wa msafara wa timu za Ligi Kuu Bara anafunguka jinsi changamoto ya wanawake inavyokuwa wakiwa safarini.

"Kuna wanawake ambao kusafiri na timu wanaenda kufanya biashara ya kuuza jezi na wanajiheshimu, lakini wengine wanasafiri tena kwa kulipiwa nauli na wakifika huko ndio wanaenda kujiuza kwa wachezaji au watu wengine."

Kuna kisa kinachohusisha mastaa wawili wa klabu maarufu za soka nchini. Shuhuda ambaye alihitaji kuhifadhiwa jina lake, anaeleza jinsi wanamichezo hao wawili wa kigeni walivyochanganywa na mwanamke mmoja, na baadaye kugundua kuwa wanashea mwanamke huyo, jambo ambalo liliingiza mvutano.

"Tuliona wachezaji wawili wa timu yetu wakichangia mwanamke mmoja, na kila mmoja alijua kuwa yuko peke yake, lakini aligundua kwamba mwenzake alikuwa akimpenda pia. Hali hii ilileta mivutano mikubwa. Si tu katika uhusiano wao wa kimapenzi, bali pia ilikosekana umoja wa timu," anasema.

Kwa mfano, kuna skendo moja msimu uliopita inayohusisha timu maarufu tunaipa jina Z. Wachezaji wake wawili wote kutoka Afrika Magharibi walibaini kuwa na uhusiano na mwanamke mmoja ambaye walimtengenezea mtego na kuamua kutembea naye kwa wakati mmoja.

Mmoja wa wachezaji katika timu hiyo anasema, "Tulijua kuwa ni mchezo wa kimapenzi, lakini hatukufikiria kuwa hii ingeleta matatizo kwenye timu. Ilikuwa ni kizaazaa kabisa, na kwa bahati mbaya mwanamke huyo aliamua kuwashtaki kwa kumdhalilisha. Hata hivyo, kesi hiyo ilifungwa haraka sana ili kulinda heshima ya timu yetu."

Hii ni hali ambayo ina madhara makubwa kwa ufanisi wa timu. Wachezaji wanaposhiriki katika vita vya kiume kwa sababu ya mwanamke mmoja, ni wazi kuwa timu inakosa umoja, na ufanisi uwanjani unapungua.


WANAICHUKULIAJE MICHEZO

Kuwepo kwa uwekezaji mkubwa katika soka la Tanzania kumekuja na mafanikio makubwa, hasa kwa wanawake. Serikali ya Tanzania na mashirika mbalimbali, pamoja na timu za soka kubwa kama Yanga na Simba, wamewekeza fedha na kwa ajili ya kuendeleza timu za wanawake.

Huu ni mfano mzuri wa jinsi sekta ya michezo inavyojidhihirisha kama njia mojawapo ya kujenga ustawi wa wanawake na kukomesha vikwazo vya kijinsia katika michezo.

"Kwa miaka mingi, soka lilikuwa linachukuliwa kama mchezo wa wanaume tu, lakini sasa mambo yamebadilika. Timu za wanawake zinapata nafasi ya kuonyesha uwezo wao kimataifa na hii imetufanya tuwe na motisha zaidi," anasema. Mwanahamisi Omary 'Gaucho', nyota wa Simba Queens. Gaucho anaamini kwa uwekezaji mkubwa uliofanywa na mashirika, timu za wanawake zimepambana na changamoto nyingi na kufika mbali zaidi.

Mmoja wa washiriki maarufu katika kuhamasisha michezo ya wanawake ni Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambalo limetunga mipango na mikakati ya kuboresha Ligi ya Wanawake, kuhakikisha wanawake wanapata fursa ya kushiriki na kupata mafunzo ya kisasa. Uwekezaji huu umeanza kuzaa matunda kwa kuwa sasa kuna idadi kubwa ya wanawake wanaoshiriki katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Kwa mfano, Ligi Kuu ya Wanawake iliyoanzishwa na TFF imeshuhudia timu nyingi za wanawake zikichuana kwa nguvu na hili linathibitisha jinsi uwekezaji katika michezo ya wanawake unavyosaidia kukuza vipaji vyao. Timu kubwa kama Simba Queens na JKT Queens zimeshiriki mashindano ya kimataifa na baadhi ya wachezaji wamepata nafasi ya kucheza nje ya nchi. Hii ni ishara ya maendeleo makubwa na uwekezaji wa kweli katika soka la wanawake.