Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Casemiro: Fundi mwingine wa boli aliyevuka bahari

Muktasari:

  • Mabosi wa Yanga wametua Zanzibar kwa ajili ya kukamilisha usajili wa nyota anayekipiga katika timu ya Mlandege ambao ndio mabingwa wa Ligi Kuu visiwani humo msimu uliosha.

MOJA ya nafasi ambayo Yanga msimu ujao lazima kuwe na ingizo jipya ni nafasi ya kiungo mkabaji ambayo inaelezwa kuwa hesabu zimeanzia kwa kiungo wa Mlandege.

Mabosi wa Yanga wametua Zanzibar kwa ajili ya kukamilisha usajili wa nyota anayekipiga katika timu ya Mlandege ambao ndio mabingwa wa Ligi Kuu visiwani humo msimu uliosha.

Inaelezwa kuwa tayari wameanza mazungumzo na kiungo mkabaji Abdulnassir Mohammed Abdallah maarufu kama Casemiro.

Mwanaspoti limepifanya mahojiano na nyota huyo ambaye amezungumza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumtaja Khalid Aucho kuwa ndiye kiungo wake bora Ligi Kuu Bara.


AUCHO DARASA

Kuna viungo wengi bora waliopita Ligi Kuu Bara, lakini Casemiro humwambii kitu kuhusu Aucho anayemtaja ndiye kiungo wake bora anayemtazama na kujifunza maujanja.

"Kuna viungo wengi wanafanya vizuri, lakini navutiwa zaidi kumtazama Aucho. Ni mchezaji ambaye anajiamini. Ni mpambanaji na haogopi mpinzani," anasema mchezaji huyo na kuongeza:

"Ukiondoa hilo pia ni mchezaji ambaye mpira anaufanya uonekane mwepesi kutokana na anavyouchukulia. Hana mambo mengi. Hatumii nguvu, yeye anatumia akili na amekuwa akifanya vizuri licha ya kuzungumzwa kuwa umri wake umeenda."

Nyota huyo anaongeza kuwa mbali na Aucho, pia amekuwa akivutiwa na Feisal Salum 'Fei Toto' anayemtaja kuwa mchezaji wa kuigwa upande wa Zanzibar kutokana na kucheza kwa mafanikio tangu aondoka huko na kutua Bara.

"Fei Toto ni kiungo ambaye ameuchukulia mpira kama kazi na sio kipaji kama ilivyo kwa nyota wengi wa Kizanzibari. Tangu amevuka maji kuja kucheza Bara kwenye soka la ushindani amemudu na kuendeleza kipaji tofauti na nyota wengine."


MECHI 30 ULAJI YANGA

Casemiro ni sehemu ya kikosi kilichoipa Mlandege ubingwa wa ligi msimu wa 2024/25 akitumika katika mechi zote 30 zilizochezwa na timu hiyo ikishinda 18, sare nane na vipigo vinne, huku ikifunga mabao 67, ikiruhusu 21 na kukusanya pointi 62.

"Haikuwa rahisi, lakini naweza kusema msimu huu umekuwa bora sana kwangu. Nimepigana kwa jasho na damu kuipambania Mlandege kufikia malengo na hatimaye tumetwaa taji nikicheza mechi zote 30," anasema.

"Huenda ubora niliouonyesha ndio milango yangu ya mafanikio imeanza kufunguka. Nilikuwa bora, sijisifu kujitunza na kusikiliza nini natakiwa kufanya kutoka kwa kocha wangu. Nafikiri hiyo ndio siri ya mafanikio niliyoyapata msimu huu."

Nyota huyo alijiunga na Mlandege katika dirisha dogo msimu wa 2023/24 akiitumikia kwa msimu mmoja na nusu baada ya ulioisha kucheza bila kukosa mechi hata moja.


MSOMI, NDOTO KUKIPIGA BARA

Si nyota wengi ambao wanakipiga ligi mbalimbali wamepita shule na kuendeleza vipaji, kwani wengi wamekatisha elimu  ili kuwekeza kwenye mpira kitu ambacho ni tofauti kwa Casemiro ambaye anasoma huku anacheza soka.

Mbali ya kufanya kazi vizuri uwanjani, lakini Casemiro pia ni mwanafunzi wa Chuo kikuu Cha Zanzibar anayesomea kozi ya Utawala wa Biashara.

Casemiro ni miongoni mwa wachezaji wachache ambao wametoka moja kwa moja katika ligi za vijana na kuingia katika kikosi cha kwanza cha timu yake na hapa anasemalicha ya kupenda mpira ambao ameupa kipaumbele, lakini amewekeza pia kwenye elimu.

"Wazazi wangu wanafurahishwa na ninachokifanya uwanjani, lakini wao pia wamekuwa sehemu ya kunisimamia ili niweze kufikia malengo kwenye masomo ambapo pia nimewekeza juhudi zangu huko," anasema na kuongeza:

"Nasoma mambo ya utawala wa biashara. Kuna maisha baada ya kuachana na soka, natafuta kitu kingine cha ziada anmbapo kitaweza kunipa fedha ya kuendesha maisha yangu."


KWA NINI CASEMIRO?

Nyota wa Zanzibar wana bahati ya kupewa majina kutokana na kufananishwa na mastaa wakubwa duniani kama ilivyokuwa kwa Nadir Haroub 'Cannavaro'. Hicho ndicho kilichomtokea kiungo huyo wa Mlandege ambaye anatajwa kutua Yanga.

"Mimi naitwa Abdulnasir Mohamed Abdallah ndio majina yangu niyopewa na wazazi, lakini Casemiro ni la utani nililopewa na mashabiki wangu ambao wamekuwa wakifananisha aina ya uchezaji wangu na staa mkubwa wa Manchester United - Carlos Henrique Casimiro," anasema kiungo huyo ambaye amebainisha kuwa safari yake ya soka ilianzia katika timu za mtaani kwao na baadae akajiunga na timu ya vijana ya Real Kids iliyopo Kikwajuni.

Casemiro anamtaja Lionel Messi, mchezaji wa zamani wa FC Barcelona, PSG ambaye kwa sasa anaichezea Inter Miami ya Marekani kuwa ndiye aliyemvutia akapenda soka.