Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waigizaji Mastaa hawa wa soka wameamua kugeukia filamu

LONDON, ENGLAND.HIVI karibuni staa wa zamani wa Manchester United Jesse Lingard ameweka wazi kwamba anafikiria kugeukia masuala ya uigizaji wa filamu mbali mbali baada ya kustaafu soka.

Hii imezua mjadala mkubwa kwa baadhi ya mashabiki wa soka ambao kila mmoja amekuwa na  mtazamo wake wengine wakidai kwamba ameishiwa na wengine wakimsifia.

Lakini Lingard sio mchezaji pekee wa soka atakayekuwa amecheza filamu baada ya kustaafu, huko nyuma kuna mastaa kibao wa soka ambao wamewahi kucheza filamu na wengine wanaendelea hadi sasa. Hawa hapa mastaa watano waliogeukia huko.

Vinnie Jones
Muandaaji wa filamu kutoka Uingereza ndio alimpa nafasi fundi huyu kuwa muigizaji kutokana na kipaji alichokiona ndani yake.
Staa huyu wa zamani wa Chelsea  ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 58 alianza kuigiza mwaka 1998 ambapo muvi yake ya kwanza iliitwa Lock, Stock and Two Smoking Barrels akiigiza kama Big Chris.

Baada ya muvi hiyo inadaiwa ameigiza muvi nyingine zisizopungua 109 na kubwa zaidi ni ile ya mwaka X-Men: The Last Stand ya mwaka 2006 akiwa na mastaa kama  Hugh Jackman na Patrick Stewart.
Muvi ya mwisho kuigiza ilikuwa ni mwaka jana iitwayo Bullet Proof.

Eric Cantona
Huyu alikuwa mmoja kati ya mastaa wa soka waliostaafu mapema. Cantona ambaye aliwahi kuichezea Man Utd kwa mafanikio.

Cantona mwenye umri wa miaka 56, baada ya kustaafu soka akiwa na miaka 30, aliigiza muvi yake ya kwanza iliyoitwa Eleven Men Against Eleven mwaka 1995 na muvi yake maarufu zaidi ni ile ya Elizabeth iliyotoka  mwaka 1998 ambapo alihudumu kama balozi wa Ufaransa.

Baada ya hapo alionekana kwenye muvi mbali mbali za Kifaransa na muvi yake ya mwisho ni ile ya mwaka 2020 iitwayo Inhuman Resources.

Zlatan Ibrahimovic
Kama unavyofahamu kwamba staa huyu anayeichezea AC Milan mbali ya soka ana uwezo mkubwa wa mapigano mbali mbali ikiwa pamoja na Karate.
Hiki kilikuwa kigezo kimoja wapo kilichomsaidia kupata shavu ya kucheza kwenye muvi iitayo  Asterix & Obelix: The Middle Kingdom iliyotoka mwaka huu.

Humu alicheza kama mmoja kati ya wanajeshi wa kikosi cha ngome ya Roma na akaonyesha uwezo mkubwa wa kupambana.
Ndani ya muvi hii pia yumo mshini wa tuzo ya Oscar  Marion Cotillard.

David Beckham
Huyu pia alipata shavu kupitia muandaaji wa filamu Muingereza Pal Guy Ritchie ambaye alimtumia kwenye muvi mbili.yakwanza ikiwa ile ya mwaka  2014 iliyoitwa  The Man from U.N.C.L.E. ambapo aliigiza kama mtu anayefanya kazi kwenye ukumbi wa sinema, kisha akaigiza kwenye muvi nyingine ya King Arthur: Legend of the Sword iliyotoka mwaka 2017 aliyoigiza kama  Trigger.

Pele
Wakati huu Pele alikuwa kwenye kilele cha mafanikio akiwa mmoja kati ya wachezaji bora sana Duniani, alipata shavu la kucheza muvi iliyoitwa Escape to Victory ambapo aliigiza kama mmoja ya mastaa.

Kwenye muvi hii jina lake aliitwa  Corporal Luis Fernandez na muvi hiyo ilikuwa ikihusu masuala ya vita ya pili ya Dunia.
Kwenye muvi hiyo alicheza na mastaa wengine wakubwa wa muvi kama Michael Caine na Sylvester Stallone(Rambo).

Muvi hiyo ilitoka mwaka 1981 na ndani yake kulikuwa na mastaa wengine wa soka kama  Bobby Moore na Ossie Ardiles ambao walionekana kwenye kipande kimoja cha mechi.