Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Timu zenye uwezo wa kushinda mataji zaidi ya matatu msimu huu wa 2025/26

UBINGWA Pict

Muktasari:

  • Bado kuna timu 10 katika ligi tano kubwa barani Ulaya (Bundesliga, Ligue 1, Ligi Kuu England, La Liga na Serie A) ambazo kihesabu bado zinaweza kushinda mataji yote makubwa yanayopatikana msimu wa 2025–2026.

LONDON, ENGLAND: REAL Madrid, Paris Saint-Germain na Liverpool ni miongoni mwa vigogo wa soka barani Ulaya ambao hawataweza kushinda mataji matatu (treble) au manne (quadruple) ya kihistoria msimu huu, baada ya tayari kuondolewa kwenye mashindano ya makombe.

Bado kuna timu 10 katika ligi tano kubwa barani Ulaya (Bundesliga, Ligue 1, Ligi Kuu England, La Liga na Serie A) ambazo kihesabu bado zinaweza kushinda mataji yote makubwa yanayopatikana msimu wa 2025–2026.

Hizi hapa timu 10 za Ulaya ambazo bado zinaweza kukamilisha mkusanyiko kamili wa mataji (aidha treble au quadruple), kuanzia zilizo na nafasi ndogo hadi kubwa zaidi.


11. Chelsea

Kwa kweli, unaweza kuwapa Chelsea tathmini fupi sana hapa. Kwa kuzingatia uwezo wao wa kukabiuliana na timu kubwa (PSG, Arsenal, Barcelona), si jambo lisilowezekana kabisa kwa Chelsea kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya tatu. Mara mbili zilizopita pia zilionekana hazitawezekana katika hatua hii ya msimu. Taji moja lingekuwa mafanikio makubwa kwa Liam Rosenior msimu huu. Mawili yangekuwa bora sana. Matatu au manne? Basi anaweza kusema lolote linaweza kutokea kwa sababu soka imeundwa kwa maajabu.


10. Monaco

Les Monegasques walikuwa vibaya kupita kiasi katika kichapo cha mabao 6-1 dhidi ya Real Madrid. Hawako karibu kabisa, jambo linalodhihirishwa na nafasi yao ya tisa kwenye Ligue 1, wakiwa nyuma kwa pointi 20 dhidi ya vinara wa kushangaza, Lens. Na bado, kwa namna fulani, wana nafasi kubwa zaidi ya kukamilisha mkusanyiko kamili wa mataji kuliko Chelsea.


9. Marseille

Uliwaona Marseille dhidi ya Liverpool? Kikosi cha Roberto De Zerbi hakishindi Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hata hivyo, wanaweza kusemwa kuwa ni wagombea wakuu wa Coupe de France baada ya PSG kutolewa kwa kushangaza na majirani zao Paris FC. Lakini hatuoni wakifidia pengo la pointi saba dhidi ya PSG kwenye Ligue 1. Hata hivyo, Marseille ni moja ya timu ambayo bazo zipo kwenye michuano mingi.


8. Napoli

Kutoka sare baada ya kuongoza dhidi ya FC Copenhagen iliyokuwa na wachezaji 10 ni sehemu nyingine ya mfululizo wa maswali: “Kwa nini Antonio Conte hana mafanikio Ulaya?” Napoli si timu ya kuchukuliwa kwa uzito kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mabingwa watetezi wa Serie A wako nje ya nafasi 24 bora za Ligi ya Mabingwa na wanakutana na Chelsea kwenye mchezo wa mwisho. Kuna uwezekano mkubwa wakaangusha kabisa. Lakini, hadi sasa bado wapo kwenye orodha ya timu zinazoweza kushinda taji zaidi ya moja msimu huu.


7. Juventus

Juve hatimaye imeonyesha dalili za maendeleo mazuri uwanjani. Ni timu ya kuangalia Ulaya. Ushindi safi wa mbao 2-0 dhidi ya Benfica ya Jose Mourinho ulionyesha ufanisi wao wa kimya kimya, na kumaliza ndani ya nane bora inaonekana inawezekana. Luciano Spalletti ana uzoefu mkubwa, lakini kufidia pengo la pointi 10 dhidi ya Inter ni kazi ngumu sana kwenye mchakamchaka wa ligi ya ndani licha ya kwamba bado ina mataji mengi ya kushindania.


6. Atletico Madrid

Ni nusu ya kwanza ya msimu yenye misukosuko tena kwa kikosi cha Diego Simeone, lakini kikiwa kwenye ubora wake kinaweza kuwasumbua wapinzani wowote.

Ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Real Madrid ulikuwa ishara ya mwanzo wa mwisho kwa Xabi Alonso, tukitazama nyuma. Lakini tunajua kitakachofuata, watakutana na wapinzani wao wa jiji kwenye robo fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya, watapoteza kwa namna ya kuumiza na ya kuchekesha kwa pamoja na safari itaishia hapo. Lakini, kinachovutia bado wapo kwenye mashindano mengi msimu huu.


5. Man City

Baada ya kuifunga Nottingham Forest 2-1 mwishoni mwa Desemba, Manchester City ilionekana kuanza kasi ya kutisha. Lakini ikaangukia kwa Sunderland, Chelsea, Brighton, Manchester United na Bodeo/Glimt katika matokeo ya aibu Ulaya. Baada ya ushindi mara nane mfululizo kumalizia 2025, kikosi cha Pep Guardiola kimeanza 2026 bila kuonekana kama mashine isiyozuilika. Tungepata mshangao kama Man City wangemaliza msimu wa pili mfululizo bila taji. Wako karibu na fainali ya Kombe la Ligi na bado wapo kwenye mashindano manne. Lakini kwa sasa, hawaonekani kama mabingwa wanaosubiriwa.


4. Inter Milan

Inter inaongoza Serie A, ikiwa na faida ya pointi sita dhidi ya Napoli na nafasi yao ya hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imeshahakikishwa.

Wakiifunga Borussia Dortmund wiki ijayo huenda wakaepuka raundi ya mchujo. Lakini bado kuna shaka. Imepita zaidi ya mwaka tangu wafunge timu za kiwango cha juu Italia. Wanaweza kutawala mashindano ya ndani, lakini lazima waongeze kiwango sana ili kuwa tishio barani Ulaya.


3. Barcelona

Sasa tunaingia kwa wagombea wa kweli. Pep Guardiola aliipa Barcelona treble ya kwanza. Luis Enrique ya pili. Je, Hansi Flick ataleta ya tatu?

Mwanzo wa msimu Barca ilionekana dhaifu, mstari wao wa juu wa ulinzi ukipitwa kirahisi. Lakini kurejea kwa Raphinha kumewasaidia kurejea kwenye ubora. Wana kikosi kipana zaidi (Marcus Rashford) na kipa bora zaidi (Joan Garcia). Wanaongoza La Liga, ni wagombea wakuu wa Copa del Rey, na wanaonekana kuingia nane bora za Ligi ya Mabingwa Ulaya.


2. Arsenal

Hakuna timu katika historia ya soka la England iliyowahi kushinda mataji manne kwa msimu mmoja. Itakuwa ajabu kwa timu isiyoshinda taji kubwa kwa miaka mitano kuwa ya kwanza kufanya hivyo, lakini Arsenal wanaonekana imara kwenye mashindano yote manne. Wamehakikisha nafasi ya juu kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, wanaongoza Ligi Kuu England kwa pointi saba, wanaongoza nusu fainali ya Kombe la Ligi, na wana kikosi kirefu zaidi nchini.

Kila kitu kinaenda sawa kwa Arsenal. Huenda wakateleza sehemu moja, lakini huu unaonekana kuwa mwaka wa kumaliza ukame wa mataji. Adui wao mkubwa anaweza kuwa wao wenyewe.


1. Bayern Munich

Ikilinganishwa na Arsenal, kampeni ya Bayern haina matatizo mengi, lakini hiyo ndiyo sababu wako kileleni mwa orodha. Tayari wameshinda trebles mbili. Wametwaa mataji 11 ya ligi mfululizo hivi karibuni. Nao ndio timu pekee isiyopoteza katika ligi tano kubwa Ulaya.

Ushindi mara 16, sare 2, vipigo 0. Mabao 71, wakifungwa 14 tu. Ni kama mzaha. Wanakaribia kushinda Bundesliga na wana nafasi kubwa ya kutwaa DFB Pokal.

Swali kubwa ni Ulaya. Lakini kwa sasa, Bayern ya Vincent Kompany inaonekana kuwa timu imara zaidi barani humo.