Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola alivyowafunika makocha wote kwa matumizi kwenye usajili

GUARDIOLA Pict

Muktasari:

  • Guardiola alirithi kikosi kilichozeeka msimu wa 2016–17 na mara moja alitumia zaidi ya Euro 190 milioni katika msimu wake wa kwanza, akisajili wachezaji kama Ilkay Gündogan, Leroy Sane, John Stones, Claudio Bravo na Gabriel Jesus.

MANCHESTER, ENGLAND: TANGU ajiunge na Manchester City mwaka 2016, Pep Guardiola amekuwa meneja aliyotumia fedha nyingi zaidi katika soka duniani, na kwa tofauti kubwa sana ukilinganisha na wengine.

Guardiola alirithi kikosi kilichozeeka msimu wa 2016–17 na mara moja alitumia zaidi ya Euro 190 milioni katika msimu wake wa kwanza, akisajili wachezaji kama Ilkay Gündogan, Leroy Sane, John Stones, Claudio Bravo na Gabriel Jesus.

Katika msimu wake wa kwanza, Man City ilimaliza nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu England bila kushinda taji lolote, lakini haikuchukua muda mrefu kwa Guardiola kupata mwendo wake nchini England.

GUAR 01

Katika msimu wake wa pili, alitumia tena takribani Euro 280 milioni, akisajili wachezaji kama Ederson, Bernardo Silva, Kyle Walker, Benjamin Mendy na Aymeric Laporte.

Hili linaweza kusemwa kuwa dirisha bora zaidi la usajili katika kazi ya Guardiola, kwani wengi wa wachezaji aliowasajili msimu huo waliendelea kuwa na mafanikio makubwa na ya muda mrefu ndani ya klabu.

Akiwa ameunda mhimili mpya wa kikosi, Man City ilitawala Ligi Kuu England kwa kishindo, ikitwaa ubingwa kwa rekodi ya pointi 100.

Baada ya msimu wa 2017–18, kikosi cha Guardiola kiliendelea kushinda mataji matano kati ya sita ya ligi yaliyofuata, na katika kipindi hicho walitumia zaidi ya Euro 970 milioni kuwanunua wachezaji wapya.

GUAR 03

Katika kipindi cha miezi 18 iliyopita, ni haki kusema kuwa Man City imeanza kukumbana na changamoto, lakini matumizi yao ya fedha yameendelea kuongezeka.

GUAR 02

Baada ya usajili wa hivi karibuni wa Antoine Semenyo na Marc Guehi, Guardiola angeweza, kinadharia, kuunda kikosi kamili cha kwanza chenye thamani ya Pauni 415 milioni, akitumia wachezaji pekee aliowasajili tangu Januari iliyopita.

Kwa mujibu wa Transfermarkt, Guardiola ametumia jumla ya Euro 2.05 bilioni tangu ajiunge na Man City, kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuliko kocha mwingine yeyote.

Kwa ujumla, amenunua wachezaji 67 katika kipindi chake klabuni hapo, kwa wastani wa gharama ya Euro 30.5 milioni kwa kila mchezaji.

GUAR 04

Kocha aliye karibu zaidi kufikia matumizi ya Guardiola katika kipindi hicho ni kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone, ambaye ametumia Euro 1.22 bilioni tangu msimu wa 2016–17.

Simeone pia ndiye kocha anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kwa sasa, na sehemu kubwa ya matumizi yake yamekwenda kwa wachezaji kama Joao Felix, Julian Alvarez na Thomas Lemar.

Pamoja na Guardiola na Simeone, kuna makocha wengine saba waliotumia zaidi ya Euro 1 bilioni tangu mwaka 2016. Makocha hao ni Antonio Conte, Massimiliano Allegri, Thomas Tuchel, Unai Emery, Mikel Arteta, Erik ten Hag na Eddie Howe.

GUAR 05

Kwa mshangao wa wengi, Nuno Espírito Santo anakamilisha orodha ya 10 bora, akiwa ametumia fedha nyingi zaidi kuliko makocha kama Jürgen Klopp, Mauricio Pochettino, Jose Mourinho na Luis Enrique tangu msimu wa 2016–17.

Hakuna ubishi kwamba Guardiola ndiye kocha bora wa kizazi chake, lakini pia ni kweli kwamba amepata msaada mkubwa wa kifedha kuliko makocha wengi.