Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UEFA: Arsenal yafuzu mtoano, Man City hoi

Muktasari:

  • Kipigo cha Manchester City dhidi ya Bodo/Glimt mapema hiyo Jumanne kilimaanisha kuwa Arsenal tayari walikuwa wamefuzu rasmi kwa hatua ya 16 bora. Hata hivyo, ushindi dhidi ya vigogo hao wa Italia ulithibitisha hadhi yao kama timu bora zaidi kwenye mashindano hadi sasa.

MILAN, ITALIA: ARSENAL imeweka rekodi mpya ya klabu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wao wa saba mfululizo, baada ya kuifunga Inter Milan 3-1 katika Uwanja wa San Siro usiku wa Jumanne.

Kipigo cha Manchester City dhidi ya Bodo/Glimt mapema hiyo Jumanne kilimaanisha kuwa Arsenal tayari walikuwa wamefuzu rasmi kwa hatua ya 16 bora. Hata hivyo, ushindi dhidi ya vigogo hao wa Italia ulithibitisha hadhi yao kama timu bora zaidi kwenye mashindano hadi sasa.

Ili kuonyesha ubora wao zaidi, Arsenal sasa ni timu ya pili tu katika historia ya mashindano kushinda mechi saba za Ulaya kwa tofauti ya mabao mawili au zaidi. Timu nyingine ni Bayern Munich msimu wa 2019/20, walipokuja kushinda taji Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huo.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, aliiambia Amazon Prime: "Tulifikia kiwango kingine, na kufanya hivyo San Siro dhidi ya moja ya timu bora barani Ulaya ni jambo la kipekee."

Kwa kufunga mabao mawili kwa mara ya kwanza kwa Arsenal ndani ya zaidi ya mwaka mmoja, Gabriel Jesus alikuwa nyota wa mchezo huo nchini Italia, akifunga bao la kwanza kwa ustadi wa hali ya juu na la pili kutoka mpira wa adhabu ndogo.

Kati ya mabao hayo, bao la kusawazisha la Petar Sucic kwa mkwaju wa kupinda liliipa Arsenal wasiwasi kidogo, lakini hatimaye Gunners walistahili ushindi wao wa kwanza nchini Italia tangu 2008. Walikuwa wamepoteza mechi nne kati ya tano zilizopita kwenye ardhi ya Italia.

Straika Viktor Gyokeres, alihitimisha ushindi huo kwa bao la mbali dakika tano za mwisho, lilikuwa bao lake la tatu katika mechi tano za Ligi ya Mabingwa.

Arsenal walianza kwa kasi San Siro, wakipiga mashuti mawili ndani ya sekunde 20 za mwanzo, jambo lililoweka mwelekeo wa mchezo.

Hawakusubiri muda mrefu kupata bao la kwanza, baada ya jaribio lililokosa mwelekeo la Jurrien Timber kumkuta Jesus aliyefunga bao lake la kwanza Ulaya tangu arejee baada ya jeraha refu la goti. Bao la kusawazisha la Sucic liliwatikisa Arsenal kwa muda mfupi, lakini Jesus alifunga tena, safari hii kutoka kona baada ya Leandro Trossard kugusa mpira kwanza karibu na lango kabla ya kumrudisha kwa Jesus aliyekuwa wazi.

Mabao ya 25 na 26 ya Mbrazili huyo katika mashindano hayo yalikuwa kilele cha ushindi mkubwa kwa Gunners na mwenyewe alisema: "Ni usiku wa ndoto. Kuwa katika uwanja huu na kufunga hapa kunanifanya nitokwe na machozi kwa sababu siku zote niliota kuwa hapa."

Rekodi ya Jesus katika Ligi ya Mabingwa bado ni ya kipekee. Akiwa na michango 34 ya mabao katika mechi 53, wastani wake wa mchango wa bao 1.03 kwa dakika 90 unazidiwa tu na Kylian Mbappe mwenye 1.08.


Spurs washinda Dortmund

Tottenham Hotspur ilifikisha mechi 24 bila kupoteza nyumbani barani Ulaya baada ya kuifunga Borussia Dortmund waliobaki na wachezaji 10 kwa mabao 2-0.

Timu ya Thomas Frank imekuwa ikihangaika nyumbani kwenye Ligi Kuu England msimu huu, ikipoteza mechi sita kati ya 11 kwenye Uwanja wa Tottenham Hotspur. Kuanza kwake kwa mara ya kwanza msimu huu kulimletea Dominic Solanke bao lake la kwanza, akifunga kwa karibu baada ya nahodha Cristian Romero kuifungia Spurs bao la kwanza. Kichwa cha Romero kutoka kona dakika ya 14 kilikuwa zawadi ya mwanzo mzuri wa Spurs waliokuwa wakisukuma Dortmund kwa presha kubwa.

Kati ya mabao hayo mawili, Dortmund walipunguzwa wachezaji baada ya Daniel Svensson kuoneshwa kadi nyekundu kwa kumkanyaga Wilson Odobert.

Spurs sasa ndiyo timu pekee ambayo haijaruhusu bao nyumbani kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, wakishinda mechi zote nne bila kuruhusu bao.

Kocha Thomas Frank alisema: "Hii ni mechi ya nane mfululizo tunafanya mambo mengi sawa. Sasa tunatazamia matokeo mazuri tena Jumamosi."

Solanke akawa mchezaji wa tano kufunga katika mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa Spurs na Mwingereza wa pili baada ya Peter Crouch mwaka 2010.


Man City yapata kipigo Norway

Manchester City ilikuwa na usiku mbaya katika Uwanja wa Aspmyra, ikipoteza 3-1 dhidi ya Bodoe/Glimt na kuwa timu ya kwanza ya England kupoteza dhidi ya klabu ya Norway. Ilikuwa pia ushindi wa kwanza wa Bodoe katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku Man City wakipoteza mechi mbili mfululizo mara ya tatu msimu huu. Mabao mawili ya haraka ya Kasper Hogh yaliweka msingi wa ushindi wa kihistoria, huku Jens-Petter Hauge akiongeza bao la tatu. Ingawa Rayan Cherki alipunguza tofauti, Rodri alitolewa kwa kadi nyekundu muda mfupi baadaye.

Kocha Pep Guardiola alisema: "Matokeo tangu mwisho wa 2025 hayajawa mazuri. Lazima tubadilishe hali haraka."

Man City sasa wanajiandaa kucheza dhidi ya Wolves kabla ya kuwakaribisha Galatasaray katika Ligi ya Mabingwa Ulaya uwanjani Etihad.


Mechi nyingine

Katika matokeo ya mechi nyingine za Jumanne, Kairat Almaty ikiwa nyumbani ilikubali kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Club Brugge, FC Copenhagen ilitoshana nguvu na Napoli baada ya kufungana 1-1, wakati Olympiacos iliichapa Bayer Leverkusen 2-0, Real Madrid iliangusha kipigo kizito cha mabao 6-1 kwa AS Monaco, Sporting CP iliitandika Paris Saint-Germain 2-1 na Ajax ikishinda ugenini 2-1 dhidi ya Villarreal.