Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tausi FC inakuja kuwashika au kupita kama wengine?

TAUSI Pict

Muktasari:

  • Bahati nzuri ni kwamba kuna majina mengi ya mastaa waliopita nchini na pia waliopo wanaoendelea kukiwasha, huku timu nyingi zikiwa zimecheza Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) tangu ilipoanzishwa. Jambo la kusitikisha zipo timu ziliwahi kung'ara, lakini hazikudumu katika mashindano hayo, ikiwamo Gets Program iliyotajwa kuwa ingeleta maajabu msimu ulioisha.

SOKA la wanawake limeanza kushika kasi nchini na duniani kwa ujumla, ambapo nyota kadhaa wa ndani na kimataifa wamekuwa wakishiriki kila mwaka mashindano ya ligi za ndani.

Bahati nzuri ni kwamba kuna majina mengi ya mastaa waliopita nchini na pia waliopo wanaoendelea kukiwasha, huku timu nyingi zikiwa zimecheza Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) tangu ilipoanzishwa. Jambo la kusitikisha zipo timu ziliwahi kung'ara, lakini hazikudumu katika mashindano hayo, ikiwamo Gets Program iliyotajwa kuwa ingeleta maajabu msimu ulioisha.

Tausi ni miongoni mwa timu zilizofanya vizuri kwenye mashindano ya Ligi Daraja la Kwanza (WFDL) msimu huu hadi ikafanikwa  kubeba ubingwa na hivyo kupanda WPL. Hata hivyo, swali linalokuja ni je itadumu katika mikikimikiki hiyo au itapita tu kama timu zingine?

Timu hiyo ilinyakua ubingwa huo baada ya kuchapa Bilo Queens kwa mabao 3-0 kwenye fainali iliyopigwa Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. Mashindano hayo yalishirikisha timu 16 zilizochuana kusaka mshindi.

Lakini, katika mashindano hayo Tausi imeandika rekodi ya kuchukua ubingwa bila kupoteza mchezo kwenye mechi tano ikianza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Maendeleo Queens, kisha ikaichapa mabao 8-0 Tanzania Prisons, halafu ikaifumua Bunda Girls  2-0 na nusu fainali ikaing'oa Geita Queens kwa mabao 2-0 na kutinga fainali.

Katika mashindano hayo mshambuliaji wa timu hiyo, Adama Congo ameibuka mfungaji bora baada ya kutupia kambani mara 14  katika mechi hizo ikiwa ni wastani wa kufunga mabao matatu kwa kila mchezo. Nyuma ya kufanya vizuri kwenye mashindano hayo ni pamoja na kujiandaa mapema na kufanya usajili wa maana.

Timu hiyo kabla ya kuitwa Tausi ilifahamika kama Ukerewe Queens iliyokuwa na makazi yake jijini Mwanza, ambapo ilinunuliwa na mmoja wa matajiri aliyewekeza mkwanja wa maana kuhakikisha inafanya vizuri na kuleta ushindani kabla ya kupanda daraja. Baada ya kununuliwa imetoka Mwanza na makazi yake yatakuwa Dar es Salaam.

Mwanaspoti linakuletea kikosi cha timu hiyo kinachotarajia kucheza Ligi Kuu msimu ujao sambamba na Bilo, Ruangwa Queens na Geita Queens zilizopanda.

TAU 05

KOCHA MKUU

Maria Ruiz ndiye kocha mkuu aliyeiongoza kubeba ubingwa Daraja la Kwanza, akiwa ni kocha Mhispaniola mwenye mafanikio kwenye soka akiwahi kucheza kwa nyakati tofauti miaka ya nyuma, ambapo amecheza Marekani, Hispania na Russia. Pia Ligi ya UEFA ya Wanawake na alifanikiwa kushinda Kombe la Wanawake Hispania (Copa de la Reyna) akiwa na RCD Espanol De Barcelona, FC Indiana. Kule Russia alikipiga FK Zorky ilhali pia aliwahi kuisaidia Real Madrid kupanda Ligi Kuu Hispania.

Tangu amekuwa kocha amefundisha timu mbalimbali za vijana Hispania pamoja na Dux Internacional de Madrid za chini ya miaka 10, 12 na 18 kwa wasichana akiwa kocha mkuu na pia chini ya miaka 18 kwa wanawaume kama kocha msaidizi.

Kocha huyo mwenye leseni ya A ya UEFA hii ni mara yake ya kwanza kufundisha Afrika Mashariki na Tanzania na anakuwa kocha wa kwanza wa kigeni kuipandisha timu ikiwa haijapoteza mchezo kuanzia makundi hadi fainali.

TAU 03

WASAIDIZI

Katika benchi lake, kocha huyo anasaidiwa na nyota wa zamani wa Yanga, Mohammed Hussein 'Mmachinga' pamoja na nyota wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake 'Twiga Stars', Hilda Masanche.

Upande wa makipa kocha anatoke Nigeria, Alloy Agu, ambaye pia anafundisha timu ya taifa ya makipa nchini humo.

Agu ambaye ana sifa na uzoefu mkubwa akiwa mchezaji aliyetumikia timu taifa ya wanawake ya Nigeria na 2018 alicheza fainali za Kombe la Dunia la Wanawake nchini Russia huku pia akiwahi kushiriki michuano ya Afcon akiwa na nchi yake.

Wakati anacheza aliwahi kuzitumikia Enyimba, Nasarawa United, Nepa 1982/89, ACB Lagos 1990 za Nigeria. Pia kacheza MVV Maastricht ya Uholanzi 1990/92, RFC Liège ya Ugiriki 1992/94, Kayserispor ya Uturuki 1994/97 na Indiana ya Marekani kama kipa.

Upande wa tiba kuna Grace Banda ambaye ana uzoefu wa muda mrefu katika kuhudumia wachezaji wa mpira amewahi kuhudumu katika timu za Simba Queens, African Lyon, Ruvuma Queens na Fountain Gate Princess.

Mbali na huyo, pia klabu hiyo imemtambulisha aliyewahi kuwa meneja wa vifaa wa Yanga Princess, Mata Gwasa.

TAU 02

WACHEZAJI

Kwenye timu 16 zilizocheza Ligi Daraja la Kwanza msimu uliopita ni Tausi pekee iliyokuwa na nyota wanne wa kigeni waliocheza mashindano hayo na kuonyesha viwango bora.

Timu hiyo imesajili makipa watatu Watanzania wakiwa ni Khadija Thadeo na Batuli ilhali Ruth Aturo ni kutoka Uganda.

Khadija kabla ya kuichezea Tausi alipita Tanzanite Queens, Ruvuma Queens, Ilala Queens na Ceasiaa Queens.

Kwa Aturo hii ni mara yake ya kwanza kuicheza Ligi Kuu Bara kwani aliwahi kupita klabu kama vile Kawempe Muslim na UCU Lady Cardinals za Uganda, FC KTP ya Finland, Al-Shabab na Altaqadum za Saudia Arabia pamoja na Vihiga Queens ya Kenya.

Aturo ndiye nahodha wa timu ya taifa ya Uganda ambaye ana mafanikio makubwa akiwahi kunyakua tuzo mbalimbali ikiwemo mchezaji bora wa kike Uganda (2018), kipa bora wa mashindano ya Cecafa kwa wanawake (2018) na kipa bora wa CosafaA Women's Championship (2018).

TAU 04

Fatoumata Diara, huyu ni nyota raia wa Mali anayecheza nafasi ya kiungo na mshambuliaji, na kwenye Ligi Daraja la Kwanza katika mechi nne amefunga mabao matatu. Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Mali anakumbukwa 2004 kuwa alicheza mechi tano za kufuzu Wafcon na kufunga mabao matatu akitajwa kuwa miongoni mwa nyota waliofanya vizuri wakati huo.

Mshambuliaji huyo (38), aliifungia tena Mali mabao matatu kwenye michuano hiyo 2018 jambo ambalo limekuwa na mwendelezo kwake na msimu ulioisha kafunga mabao mawili kwenye mechi moja. Fatoumata amecheza Wafcon mara sita akiwa na Mali. 

Kabla ya kujiunga na Tausi alipita FC Amazones and AS Mande zote za nchini kwao. Mafanikio makubwa ya nyota huyo ni kubeba tuzo ya mchezaji bora mara tatu mfululizo kwenye fainali za Mali Cup, mchezaji bora upande wa wanawake wa mwaka mara mbili Mali, mchezaji bora mara mbili Ligi Kuu ya Wanawake Mali na mchezaji na mfungaji bora wa Champions League Kanda ya UFOA A iliyofanyika Cape Verde.

Ndani ya kikosi cha Tausi pia kuna Adama Congo ambaye ndiye mshambuliaji tegemeo wa timu ya taifa ya Burkina Faso na msimu huu aliingia kwenye kinyang'anyiro cha tuzo za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwenye kipengele cha goli bora la mwaka. Kabla ya kujiunga na Tausi alicheza AOEF, ASO, Djelgodji na Malabo Kings za Equatorial Guinea.

Adama anashikilia rekodi ya kuwa mshambuliaji wa kwanza katika historia ya timu ya taifa ya wanawake ya Burkina Faso kufunga bao la kwanza Wafcon na pia katika mashindano hayo liliibuka bao bora la michuano ya mwaka 2022.

TAU 01

Ni fundi haswa wa kufumania nyavu kwani kwenye Ligi Daraja la Kwanza Bara katika mechi nne alizocheza amefunga mabao 13 ikiwa ni  wastani wa kufunga mabao matatu kila mechi.Ubora wake umefanya hata kabla hajacheza Ligi Kuu baadhi ya timu zimeanza kupiga hodi klabuni hapo kupata saini yake.

Raia mwingine wa kigeni katika timu hiyo ni Addiaratou Coulibaly ambaye ni kiungo mwenye uwezo wa kucheza namba sita na nane akitumia miguu yote miwili, akiwa pia ndiye nahodha wa timu ya taifa ya Mali nchini ya umri wa miaka 20 na hivi karibuni ametoka kuchukua tuzo ya mchezaji bora chipukizi. Hii ni mara ya kwanza kucheza nje ya taifa lake na kabla ya kutambulishwa Tausi aliitumikia Super Lioness d'Hamdalaye ya Mali.

Pamoja na ubora wa kikosi cha Tausi, je itauweza mziki wa timu za Simba Queens, Yanga Princess na JKT Queens katika Ligi Kuu ya Wanawake Bara ambazo zimekuwa zikibadilishana ubingwa? Hilo ni suala la kusubiri na kuona!