Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spurs dah! Chelsea, Liverpool hazichekani

SPURS Pict

Muktasari:

  • Hiki ni kipigo cha 15 ikiwa nyumbani dhidi ya Nottingham Forest, jambo linalowaweka katika hatari ya kushuka daraja na Kocha msaidizi wa timu hiyo, Bruno Saltor alisema kupoteza kwa mabao 3-0 kumeongeza presha kubwa kwa Spurs kuelekea mwisho wa msimu.

LIVERPOOL, ENGLAND: HAKUNA namna zaidi ya kupigana hadi tone la mwisho. Ndiyo, Spurs ili isalie Ligi Kuu England msimu ujao, ina kazi ya kufanya kuhakikisha inashinda mechi zake zilizosalia kwa asilimia kubwa ili kujinasua na mtego wa kushuka daraja hadi Championship.

Iko hivi, kwa sasa Spurs inakamata nafasi ya 17 ikiwa na pointi 30 baada ya kucheza mechi 31 na imesaliwa na saba tu za kuamua hatima yao.

Baada ya kuonekana kuanza kuimarika baada ya kuizuia Liverpool wikiendi iliyopita mechi ya EPL kwa sare ya bao 1-1 na kuichapa Atletico Madrid mabao 3-2 nyumbani katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, mashabiki walijitokeza kwa wingi kwenye uwanja wao wa nyumbani na hata kuahirisha maandamano dhidi ya wamiliki wa klabu hiyo, hali ilikuwa mbaya na kukubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Nottingham Forest. Katika mchezo huo, Spurs ilionyesha kiwango kibovu na kusababisha mashabiki kuzomea.

SPU 01

Hiki ni kipigo cha 15 ikiwa nyumbani dhidi ya Nottingham Forest, jambo linalowaweka katika hatari ya kushuka daraja na Kocha msaidizi wa timu hiyo, Bruno Saltor alisema kupoteza kwa mabao 3-0 kumeongeza presha kubwa kwa Spurs kuelekea mwisho wa msimu.

Saltor, aliyekiongoza kikosi hicho kutokana na Kocha Mkuu, Igor Tudor kupata matatizo ya kifamilia, alisema bado kuna matumaini kutokana na kiwango kizuri walichokionyesha kipindi cha kwanza katika mechi hiyo na hata mbili zilizopita.

Alisema vita kubwa inayowakabili nyota wake kwa sasa ni ya kubaki kwenye ligi na kuepuka kumaliza nafasi za chini kama msimu uliopita na ilimaliza nafasi ya 17 na pointi 38.

SPU 02

Wakati hali ikiwa hivyo kwa Spurs, wikiendi iliyopita ilikuwa chungu pia kwa vigogo wengine wa ligi hiyo, Chelsea na Liverpool zilizokutana na vichapo ugenini kila moja.

Liverpool ikiwa American Express, ilichapwa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wao, Brighton huku Chelsea ikitandikwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Hill Dickinson jijini Liverpool dhidi ya Everton, kikiwa ni kipigo cha nne mfululizo kwa matajiri hao wa London.

Licha ya matokeo hayo, Chelsea yenye pointi 48  na Liverpool yenye 49 zimeendelea kusalia katika nafasi ya tano na sita, Aston Villa yenyewe inaisogelea Manchester United ambayo ilitoa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Bournemouth, Ijumaa wiki iliyopita na sasa tofauti yao ya pointi ni moja, Villa ilipunguza tofauti hiyo baada ya kuinyuka West Ham mabao 2-0.

SPU 03

KWINGINEKO

Wakati hali ikiwa hivyo Ligi Kuu England, huko Ufaransa, PSG imeendelea kujikita kileleni baada ya kuichapa Nice mabao 4-0 na kufikisha pointi 60. Lens nayo imeendelea kukabana koo na wababe hao baada ya kushinda mabao 5-1 dhidi ya Angers na sasa ina pointi 59 ikiwa nafasi ya pili.

Kwenye Ligi ya Ujerumani, Bundesliga, Bayern Munich hana mpinzani na imeweka gepu la pointi 12 kati yake na inayomfuata baada ya kuichapa Union Berlin mabao 4-0. Harry Kane aliendeleza fomu yake akipachika bao lake la 31 msimu huu kwenye ligi hiyo na ndiye kinara wa ufungaji.

SPU 04

Wakati Inter Milan ikisinzia katika mechi ya pili mfululizo katika ligi ya Italia kwa kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Fiorentina, Como ya Cesc Fabregas imesogea hadi nafasi ya nne kwenye ligi hiyo baada ya kushinda mechi ya tano mfululizo kwa kuichapa Pisa mabao 5-0.  

Como kwa sasa ina pointi 57 na utofauti wake na AC Milan iliyo nafasi ya pili ni pointi sita tu na vijana hao wa Fabregas ni timu pekee kati ya nne za juu ambayo haijadondosha pointi katika mechi tano zilizopita za Serie A.