Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SPOTI DOKTA: Sababu Rodri kuwa nje msimu wote, jeraha lake lipo hivi

Muktasari:

  • Rodri (28) ambaye wiki mbili zilizopita alitajwa kuwania tuzo ya mchezaji bora duniani ya Ballon D’ora alipata majeraha mabaya ya goti la mguu wa kulia katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal na kutolewa nje katika mchezo huo wa sare ya mabao 2-2.

KIUNGO fundi wa Manchester City na timu ya Taifa ya Hispania, Rodrigo Hernández ataukosa mechi zote za msimu huu zilizobaki tangu aumie baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.

Rodri (28) ambaye wiki mbili zilizopita alitajwa kuwania tuzo ya mchezaji bora duniani ya Ballon D’ora alipata majeraha mabaya ya goti la mguu wa kulia katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal na kutolewa nje katika mchezo huo wa sare ya mabao 2-2.

Baadaye baada ya uchunguzi wa kitabibu wa vipimo vya skani zilionyesha mchezaji huyo amepata majeraha mabaya yajulikanayo kitabibu kama Anterior Cruciate ligament tears.

Majeraha ya aina hii ni moja ya majeraha mabaya kwa wachezaji wa soka, ndiyo sababu wanasoka hukaa nje muda mrefu ili kupona na kuwa timamu kama awali.

Ligament hii ni mojawapo kati ya kuu nne zinazounda ungio la goti ikiwa eneo la katikati ya goti kuunganisha mfupa mkubwa wa paja na chini ya goti.

Ligament hii iliyo na umbile kama hefu X, ndiyo inayopokea shinikizo kubwa la mwili kutokana na kuwepo katikati ili kuhakikisha ungio la goti linafanya mijongeo rafiki ya goti bila kujijeruhi.

Katika mechi za ligi za EPL na Ligi ya Mabingwa Ulaya (Uefa) wiki iliyopita klabu yake imejitahidi kucheza bila kiungo huyo lakini ubora wake na mafanikio aliyosaidia pengo lake linaonekana.

Kukosekana kwake huko ni kama pia kumezipa klabu pinzani nafuu katika harakati za kuwania ubingwa wa EPL kwani mchezaji huyo ndiye kinara katika ubora katika klabu yake.

Katika taarifa ya klabu hiyo ambayo imekuwa ikiuhishwa mara kwa mara katika mtandao wa klabu hiyo na kocha wao Pep Guardiola alitoa taarifa kwa wanahabari kwa masikitiko Rodri hataweza kuwa nao kwa msimu wote uliobaki.

AlielezaSeptemba 23, Jumatatu asubuhi alifanyiwa upasuaji wa kisasa wa matundu kwa ajili ya kukarabati ligamenti hiyo pamoja na kifupa bapa cha Meniscus.


Jeraha hili liko hivi

Guardiola lieleza kiungo huyo alipata jeraha la kukatika ligament  na kujeruhi kujifupa bapa kilichopo katikati ya goti hali iliyosababisha kufanyiwa upasuaji wa goti matundu.

Ligament ya katikati ya goti iliyochanika linajulikana kitabibu kwa kifupi kama ACL na kile kijifupa bapa kilicho kama plastiki ngumu kitabibu cartilage hujulikana kama meniscus.

Kujeruhiwa kwa tishu hizi kunaweza kuanishwa kwa aina takribani tatu ikiwamo aina ya kwanza ni kuvitika sana kwa ligament pasipo kukatika au kuchanika.

Aina hii huwapata wanasoka mara kwa mara hutumia muda wa siku 3-7 kupona.

Aina ya pili ni kuvutika sana na kuchanika bila kuachana pande mbili, huweza kupona kuanzia wiki mbili mpaka miezi mitatu.

Aina ya tatu ndiyo jeraha baya kuliko yote kwani inahusisha kuchanika kwa kina au kukatika na huku ikiachana pande mbili au pia kukatika na kuchomoka katika mfupa ilipokuwa imechimbia.

Jeraha la Rodri linaangukia katika aina ya tatu ya jeraha ambalo limehusisha kuchanika na kuchomoka na kijifupa bapa katika goti chenye kazi ya kuzuia mifupa kusuguana na hunyonya shinikizo la uzito wa mwili.

Pale nyuzi hii inapochomoka huweza kuchoma na kipande cha mfupa huku kikining’inia katika ligamenti hiyo. Aina hii huwapata mara chache wanasoka lakini ndiyo inayowaacha na ulemavu wa kudumu hatimaye kushauriwa kuachana na soka.

Kijumla ligament zote huwa na kazi za kuunganisha mifupa inayotengeneza ungio na kuituliza katika eneo lake usiende uelekeo hasi ili ungio kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Katika goti zipo ligament nne zinazounda ungio lijukanalo kitabibu kama knee joint.

Ligament ya ACL ipo eneo la katikati ikiunganisha mfupa mkubwa wa paja na mfupa mkubwa goti. Kazi yake ni kuzia uelekeo hasi wa mbele wa mfupa wa ugoko na kudhibiti kujizungusha.

Ndiyo kinara kwa kujeruhiwa mara kwa mara ukilinganisha na zingine, dalili ya kipekee ya kujeruhiwa kwa ligament hii ni kutokea kwa mlio mara baada ya kujeruhiwa.

Posterior Cruciate ligament-PCL ipo upande wa nyuma ikizuia uelekea hasi wa nyuma wa mfupa wa ugoko.

Medial collateral ligament-MCL ipo pembeni uelekeo wa nje ya mwili ikiwa na kazi ya kuimarisha mifupa usiende uelekeo hasi ndani ya goti.

Lateral collateral ligament-LCL ipo uelekeo wa ndani ya mwili ikitoa uimara nje ya goti.

Mara nyingi hupata majeraha pale mchezaji anapojipinda uelekeo hasi na kulazimisha nyuzi hizi kwenda uelekeo usio wake na kuvutika kupita kiasi na hata kukatika au kuchanika.

Hapa tunapata picha namna tishu hizi zilivyo muhimu katika ungio la goti pamoja na kazi zake. Goti ndio humwezesha mchezo kupiga mashuti kupiga chenga kutulia mpira na kunyumbulika.

Goti ndio linabeba shinikizo la uzito wa mwili eneo kuanzia gotini kwenda juu, hii inalifanya eneo hili kuwa katika hatari ya kupata majeraha kirahisi.

Kazi za ungio la goti ndio zinamwezesha mwanasoka kucheza kwa ufanisi, kupata jeraha maeneo haya ndiko kunaweza kumfanya asicheze soka kwa ufanisi hatimaye kumlazimu kuacha soka.

Eneo analocheza Rodri ni kiungo mkabaji, mchezeshaji na huku pia akinyumbulika kushambulia. Eneo hili linamfanya kuwa na majukumu mengi hivyo kuwa katika hatari ya kupata majeraha.